Msama: * Atoa kauli nzito akiwasihi GEN-Z, viongozi wa dini *Ampongeza Rais Samia kwa kuunda tume huru kuchunguza matukio ya Oktoba 29 MKURUGENZI wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama amesema kilichotokea Oktoba 29, kisijirudie na watanzania wote tuseme inatosha kwani sio utamaduni wetu Msama amesema hayo leo wakati akitoa maoni yake kuhusu tume iliyoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuchunguza matukio ya vurugu za Oktoba 29, siku ya uchaguzi mkuu mwaka huu. Tume hiyo inayoogozwa na Jaji Mkuu Mstaafu, Othoman Chande, ilizinduliwa na Rais Samia, katika hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino, mjini Dodoma. Vurugu hizo ambazo hadi leo lengo lake hazijulikani, zimesababisha vifo, uharibifu wa miundombinu, mali za Serikali na watu binafsi . Msama ambaye alikuwa mgombea Ubunge jimbo la Ukonga (CCM), alisema huu sio muda wa kunyoshena kidole kwamba nani alikosea na nani alikuwa sahihi bali ni wakati wa kutafakari na kusema imetosha. Kwa mujibu wa Msama, Rais Samia anastaili pon...
Marato tv - Sauti ya Jamii