Skip to main content

Posts

Showing posts from August 12, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

BALOZI KHAMIS OMAR: MBEYA TUMIENI FURSA ZENU KUINUA UCHUMI WA TAIFA

 MWaziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amesema Mkoa wa Mbeya na kwa ujumla Nyanda za Juu Kusini una uwezo mkubwa wa kuongeza mchango wake katika uchumi wa Tanzania, akisisitiza umuhimu wa kuongeza uzalishaji, kuchakata mazao na kuimarisha uwekezaji katika viwanda. Mhe. Balozi Omar ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja mkoani Mbeya, ambapo alitembelea Ofisi za Mkoa za Chama cha Mapinduzi (CCM), jijini Mbeya. Amesema Nyanda za Juu Kusini zinachukua takribani asilimia 20 ya eneo lote la Tanzania, lakini mchango wake katika Pato la Taifa bado haujaakisi kikamilifu ukubwa wa eneo hilo na utajiri wa fursa zilizopo. Amesema hali hiyo inatoa nafasi kwa Serikali, sekta binafsi na wadau wengine kuongeza uwekezaji katika kilimo, madini, viwanda na sekta nyingine za uzalishaji ili kuongeza tija na mapato ya wananchi pamoja na Taifa kwa ujumla. “Bado tuna fursa kubwa sana ya kuimarisha mchango wetu katika pato la Taifa uendane na eneo tulilonalo, na si kwa s...

KATIBU MKUU CCM AFUNGUA TAWI LA CHAMA KIBUTENI

 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Asha-Rose Migiro, amefungua rasmi Tawi la CCM Kibuteni, Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja, leo tarehe 12 Agosti 2026. Tawi hili lina historia kubwa tangu nyakati za ASP na TANU, na ni jambo la kujivunia kuona sasa lina sura mpya inayokwenda sambamba na mahitaji na hadhi ya Chama. Dkt. Migiro amewahimiza viongozi na wanachama kuhakikisha Tawi hilo linakuwa kituo cha uhai wa Chama, mshikamano, mafunzo, vikao na utekelezaji wa shughuli za Chama. Pia, Katibu Mkuu amewashukuru wana-CCM wa Kibuteni kwa mapokezi mazuri, upendo na zawadi.

RAIS DKT. MWINYI: TAMASHA LA KIZIMKAZI NI JUKWAA LA UTAMADUNI, UTALII NA FURSA ZA UWEKEZAJI

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Tamasha la Kizimkazi limeendelea kuwa jukwaa muhimu la kutangaza utamaduni, utalii, biashara na fursa za uwekezaji zilizopo Zanzibar, sambamba na kuchochea maendeleo ya wananchi. Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 12 Agosti 2026, alipokuwa akizindua rasmi Tamasha la Kizimkazi 2026 lenye kaulimbiu “KIZIMKAZI Kumenoga!” katika Mkoa wa Kusini Unguja. Amepongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa maono ya kuasisi Tamasha hilo, ambalo limekuwa likichangia kuhifadhi mila na utamaduni, kukuza utalii na kufungua fursa za kiuchumi kwa wananchi. Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amesisitiza umuhimu wa kutumia Tamasha hilo kutangaza fursa za uwekezaji katika utalii, uvuvi, mwani na Uchumi wa Buluu, huku Serikali ikiendelea kuimarisha mazingira ya uwekezaji na miundombinu ya uzalishaji. Amesema Tamasha la Kizimkazi linaunga mkono dhamira ya Serikali ya kuongeza ...

MSAJILI WA HAZINA,FITCH RATINGS WATATHMINI MAGEUZI YA TAASISI ZA UMMA

 Na Mwandishi wa OTR ; Dar es Salaam.  Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR) Jumanne, Agosti 11, 2026, ilifanya mazungumzo na kampuni ya Fitch Ratings Ltd ikiwa ni sehemu ya mapitio ya pili ya mwaka 2026 ya tathmini ya Fitch Ratings, katika mchakato unaohusisha taasisi mbalimbali za Serikali. Mazungumzo hayo yanalenga  kuwapa wachambuzi wa Fitch Ratings fursa ya kupata taarifa za kina kuhusu mwenendo wa uchumi wa Tanzania, utekelezaji wa sera za kibajeti na fedha, pamoja na mikakati ya Serikali katika usimamizi wa deni la Taifa.  Kwa upande wa OTR, mjadala ulijikita katika utendaji wa taasisi za umma, mageuzi yanayoendelea, vihatarishi vya kifedha, pamoja na mtiririko wa fedha kati ya Serikali na taasisi za Umma. Mapema mwaka huu, Fitch Ratings iliendelea kuipa Tanzania daraja ‘B+’ kwa hadhi ya ulipaji wa madeni ya muda mrefu ya fedha za kigeni, ikitaja mwelekeo imara wa ukuaji wa uchumi na uwezo wa Serikali kukabiliana na changamoto za kifedha baada ya Uchaguzi Mkuu wa m...

TREASURY REGISTER'S OFFICE HOLDS TALKS WITH RATINGS

 By the OTR Reporter  Dar es Salaam. The Office of the Treasury Registrar (OTR) on Tuesday, August 12, 2026, held talks with Fitch Ratings Ltd as part of the rating agency’s second 2026 Sovereign Credit Rating Review of Tanzania, one of a series of engagements with Government institutions under the review.  Discussions at OTR focused on the performance of public institutions, ongoing reforms, fiscal risks, and financial flows between the Government and state-owned enterprises. Earlier this year, Fitch Ratings reaffirmed Tanzania’s long-term foreign-currency issuer default rating at ‘B+’ with a stable outlook, citing the country’s robust growth trajectory and fiscal resilience following the 2025 General Election. The affirmation follows a similar move by Moody’s Ratings in February, which maintained Tanzania’s rating at ‘B1’ with a stable outlook, signalling broadly consistent assessments by major international credit rating agencies of the country’s economic outlook. Fitc...

JARIBIO LA KWANZA LA ZAO LA VIAZI MVIRINGO MKOANI DODOMA LAONYESHA MAFANIKIO MAKUBWA

 Dodoma Jaribio la kwanza la Mbegu ya viazi mviringo lililotafitiwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) limeonesha mafanikio makubwa mkoani Dodoma katika shamba la Makamu wa Rais Mstaafu Mhe. Dkt Philip Mpango lililopo Kijiji cha Mayamaya, Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma. Jaribio hilo lililochukua siku 104 za majaribio shambani hadi kuvuna limedhihirisha kuwa zao la viazi mviringo linaweza kustawi katika mazingira ya Mkoa wa Dodoma na kuufanya Mkoa huo kuwa na fursa mpya ya zao la chakula na biashara ambalo linaweza kuwasaidia wananchi wa mkoa huo kuondokana na umasikini. Akiongelea kuhusu jaribio hilo na matokeo yake, Makamu wa Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Philip Mpango, ameishukuru TARI kwa kusimamia jaribio hilo ambalo kwa mara ya kwanza limeonyesha mafanikio katika Kijiji cha Mayamaya na kuwataka wakazi wa Mkoa wa Dodoma kuchangamkia fursa ya kulima zao hilo pindi utafiti utakapokamilika. “ Wakazi wa Dodoma sasa tuanze kuchangamkia hii fursa na TARI wako tayari kutus...

SURATI AWATAKA WAZAZI SERENGETI KUJITOKEZA KLINIKI MAALUMU YA AFYA BURE KWA WATOTO

 Mbunge wa Jimbo la Serengeti, Mheshimiwa Mary Daniel Surati, amewahimiza wazazi na walezi katika Wilaya ya Serengeti kutumia fursa ya Kliniki Maalumu ya Uchunguzi, Vipimo na Matibabu Bure kwa watoto wenye umri wa miaka 15 na chini. Kliniki hiyo maalumu imeandaliwa kwa lengo la kuwawezesha watoto kupata uchunguzi na huduma za afya mapema, hususan kwa magonjwa ya Sickle Cell, figo na ini. Kwa mujibu wa taarifa ya Mheshimiwa Surati, watoto watakaohudhuria kliniki hiyo watapatiwa uchunguzi, vipimo, dawa na matibabu bila malipo, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuhakikisha watoto wanapata huduma muhimu za afya kwa wakati. Mheshimiwa Surati amewataka wazazi na walezi kutokosa fursa hiyo, akisisitiza umuhimu wa kuwapeleka watoto wao kwa ajili ya uchunguzi wa afya hata pale ambapo hawajaonesha dalili kubwa za ugonjwa. “Ninawasihi wazazi na walezi wenye watoto wanaokidhi kigezo hiki kutumia fursa hii muhimu ya kupata uchunguzi, vipimo na matibabu bila gharama,” amesema. Ameeleza kuwa afya bo...