Skip to main content

Posts

Showing posts from October 10, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Majaliwa Mgeni Rasmi Siku ya Mwalimu Duniani Bukombe 2024

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Octoba 11, 2024 amewasili mji mdogo wa Ushirombo, Wilayani Bukombe mkoani Geita ambapo atakuwa Mgeni Rasmi katika Siku ya Mwalimu Duniani kwa mwaka 2024. Maadhimisho hayo yanafanyika kwenye Viwanja vya shule ya Sekondari Ushirombo ambapo pamoja na mambo mengine Mheshimiwa Waziri Mkuu atakabidhi vifaa vya kujifunza na kujifunzia kwa walimu na wanafunzi wilayani humo. Mheshimiwa Majaliwa amepokelewa na Mwenyeji wake Mbunge wa Jimbo la Bukombe, ambaye ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mheshimiwa Dkt. Doto Biteko.

Dkt.Stergomena Tax azuru kaburi la hayati Mkapa

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt Stergomena Lawrence Tax (Mb) tarehe 09 Oktoba 2024 amefanya ziara na kutoa heshima zake katika Kaburi la aliyekuwa Rais wa Awamu ya 3 wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Benjamin Wiliam Mkapa, na kuwasamilia baadhi ya wanafamilia,  katika Kijiji cha Lupaso, Wilaya Masasi Mkoa wa Mtwara. Akiongea katika tukio hilo, Waziri Tax aliyeambatana na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala na ujumbe wa mkoa, Waziri  Tax, amemzungumzia Hayati Benjamin Mkapa  aliyewahi kufanya kazi naye kwa karibu, kama Kiongozi mahiri na mchapakazi  wakati wa uhai wake na mfano wa kuigwa.

Balozi Nchimbi atoa uelekeo chaguzi zijazo

_Asisitiza waliobora wapate nafasi_ _Akemea viongozi wanaojigeuza miunguwatu, badala ya kutumikia watu_ _Asisitiza kila mwanachama wa CCM ana haki sawa na mwingine_ Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amewataka viongozi wa CCM kutenda haki kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Novemba mwaka huu. Akizungumza na viongozi na wanachama mbalimbali wa CCM Wilaya ya Kahama leo, tarehe 10 Oktoba 2024, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Shinyanga, akiambatana na Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Ndugu Amos Gabriel Makalla, na Katibu wa NEC - Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ndugu Rabia Hamid Abdalla. Balozi Nchimbi amesema kila mwanachama wa CCM ana haki sawa na mwingine, akisisitiza kuwa ni kinyume cha maadili ya CCM kumnyima mtu mwenye sifa bora nafasi ya uongozi kutokana na chuki binafsi. “Tunakoelekea kwenye chaguzi zetu, utekelezaji wa haki unatakiwa. Acheni kupanga safu. Viongozi bora ndio wapitishwe. Ni kosa...

Bukombe waunga mkono Jitihada za Rais Samia kuhusu nishati safi ya kupikia

📌ZAIDI YA MITUNGI 1,500 YATOLEWA KWA BEI YA RUZUKU  📌DC BUKOMBE AMSHUKURU RAIS SAMIA NA AIPONGEZA REA Wananchi kote Nchini wametakiwa kuendelea kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kutumia Nishati Safi ya Kupikia ili kuimarisha afya zao sambamba na kutunza mazingira. Wito huo umetolewa Oktoba 10, 2024 Wilayani Bukombe na Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Jadidifu na Mbadala kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Advera Mwijage wakati wa Semina maalum ya Nishati  Safi ya Kupikia kwa wakazi wa Wilaya hiyo. "Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kinara wa ajenda ya Nishati Safi ya kupikia na anafanya kila linalowezekana  kuhakikisha kila mwananchi anapata bidhaa za Nishati Safi za kupikia kwa gharama nafuu", alisema Mhandisi Mwijage. Akizungumza wakati wa Semina hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Mhe. Paskasi Muragili alimshukuru Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa ruzuku kwenye bidhaa za nishati safi za kupikia suala ambalo alisema ...

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan ameongoza kikao cha Baraza la Mawaziri

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 10 Oktoba, 2024.