Na Beda Msimbe,TBN, aliyekuwa Urusi IJUMAA Juni 5, 2026 ilikuwa siku ya kihistoria na ya kipekee, wakati Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, alisipomama mbele ya viongozi wa dunia katika Jukwaa la Kimataifa la Uchumi (St. Petersburg International Economic Forum) na hoja nzito zenye mashiko, akibeba sauti ya Watanzania wote na kuweka wazi fursa zinazopatyikana Tanzania ikiwa na pamoja na mwelekeo mpya wa nchi katika kutengeneza uchumi wa kisasa. Jukwaa hilo lilikuwa sehemu muhimu ya ziara ya Rais Samia ambayo haikuwa tu ya itifaki, bali ya kueleza milango wazi ya fursa za kiuchumi na kijamii. Jinsi Rais Samia alivyopokewa na kukirimiwa nchini Urusi katika shughuli zoye zilizomhusu, ilionesha taswira ya urafiki wa dhati na cheko tupu kati yake na mwenyeji wake, Rais Vladimir Putin. Ziara hiyo ilirudisha historia, ikaweka wazi haja ya sasa baada ya ukombozi wa kisiasa kusaidiana kupatikana kwa ukombozi wa kiuchumi na ustawi wa jamii zote mbili. Akiwa katika jukwaa la kiuchumi, akizungu...
Marato tv - Sauti ya Jamii