Skip to main content

Posts

Showing posts from June 9, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mhandisi Seff Atoa Maagizo Kwa Wakandarasi Miradi Ya Dharura (Serc)

#Awataka kukamilisha kazi kwa wakati  Dar es Salaam Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor Seff amewataka makandarasi wanaotekeleza kazi za ukarabati na matengenezo ya barabara vivuko na madaraja  katika maeneo yaliyoharibiwa na mvua za El nino nchini kutekeleza mikataba yao kwa wakati huku wakizingatia masuala ya msingi ikiwemo usalama mahali pa kazi pamoja na utunzaji wa mazingira. Mhandisi Seff ameyasema hayo wakati wa kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam kati ya TARURA na Makandarasi hao wanaotekeleza miradi hiyo nchi nzima. “Hakikisheni katika utekelezaji wa miradi yote mnakamilisha kwa wakati pia mnazingatia masuala yote ya usalama na mazingira kama ilivyoainishwa kwenye makubaliano ya jumla ya miradi hii”Alisisitiza. Naye, Mratibu wa miradi ya Benki ya Dunia kutoka TARURA Mhandisi Humphrey Kanyenye amesema kwamba wao kama waratibu wa miradi hiyo wapo tayari kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha kila mkand...

Wananchi Walioanza Kujenga Shule Kwa Nguvu zao Kujiji Cha Muaanja Wapongzwa wa na Rc Mtambi

Na Shomari Binda-Musoma  MKUU wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi amezindua rasmi shule ya sekondari Muhoji iliyoanza kujengwa kwa nguvu za wananchi. Shule hiyo ameizindua jana juni 9,2025 Kijijini Muhoji Kata ya Bugwema huku akiwapongeza wananchi na mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo kwa kuanza ujenzi kwa kutumia nguvu na kuchangia fedha zao. Hii ni sekondari ya pili ya Kata hiyo yenye vijiji vinne vya Bugwema, Kinyang'erere, Masinono na Muhoji. Akizungumza kwenye uzinduzi huo mkuu huyo wa mkoa ambaye alikuwa mgeni rasmi amewaeleza wananchi wa Kata ya Bugwema dhamira nzuri na yenye manufaa makubwa ya Rais  Dkt.Samia Suluhu Hassan ya uwekezaji mkubwa anaoufanya kwenye sekta ya elimu. Amesema kuendelea kuwekeza huko ni kuhakikisha shule zinajengwa karibu na wananchi kuhakikisha wanafunzi hawatembei umbali mrefu kwenda shuleni. Kanali Mtambi amesema hakuna urithi ulio bora kama elimu na kutoa wito kwa wanafunzi kusoma kwa bidii na wazazi na walezi kusima...

Mzee Wasira Amesema Ccm Inasubiri Kipenga...

  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema hakitaahirisha uchaguzi ng'o kwa sababu kiliomba ridhaa ya kuongoza nchi kwa miaka mitano na kimeongoza vizuri kwa kuleta maendeleo chini ya serikali iliyoongozwa na Rais Dk.  Samia Suluhu Hassan Hayo yameelezwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira alipokuwa akiwasalimia wanachama, wapenzi wa Chama na wananchi waliofika ofisi za CCM Mkoa wa Ruvuma kumlaki akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani humo. "Tuliomba ridhaa ya kuongoza Tanzania kwa miaka mitano, tumeiongoza Tanzania, tumefanya kazi yetu vizuri halafu unatuambia tuahirishe, ahirisha wewe mambo yako sisi hatuwezi ng'o, sisi tunagombea, tumeshaweka wagombea, tumemuweka Daktari Samia Suluhu Hassan (mgombea urais kupitia CCM), tumemuweka Dk. Emmanuel Nchimbi (Mgombea Mwenza wa CCM). "Sasa wako rafiki zangu wale wa 'tone tone' wao wanapita wanawaambia tusifanye uchaguzi na mimi nawauliza tukiacha kufanya uchaguzi nchi itakuwa inaongozwa na...

Wajumbe wa Mkutano Mkuu kata ya Bugogwa wapongreza utelezaji wa ilani ya uchaguzi

  Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni mjumbe wa halmashauri kuu ya Taifa ya chama cha Mapinduzi CCM mh Angelina Mabula,ameshiriki katika Mkutano Mkuu wa CCM Kata ya Bugogwa kwaajili ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa CCM katika Kata ya Bugogwa Kwa kipindi Cha 2020/2025.  Mkutano wakati wa Mkutano huo ambao Mhe Mabula alikuwa Mgeni rasmi amewapongeza viongozi wa Kata hiyo kwa kutekekeza kwa vitendo ilani ya CCM hukusimamia miradi ya maendeleo iliyoelekezwa na serikali katika kata hiyo. " Naomba niwaongezee sanaa Wana CCM wa Kata ya Bugogwa kwani utekelezaji wa Ilani hii ambayo leo tunaipokea hapa kutoka kwa Mhe Diwani umetokana na kujenga Mkubwa na muunganiko uliopo baina ya wenyeviti wa serikali za mitaa ,Mhe Diwani , Mimi mwenyewe pamoja kama Mbunge pamoja na Mhe Rais wetu Dk Samia Suluhu Hassan.  Pamoja na hayo Mhe Mbunge alitumia nafasi hiyo kuwashukuru sana wa Kata ya Bugogwa Kwa kuendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi kwani huu ndio umepel...

Makamu wa Rais Aomba Ushirikiano Katika Kudhibiti Uchafuzi wa Mazingira

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa Mataifa kuhakikisha kunakuwa na hatua za pamoja, mshikamano wa kimataifa, na uwekezaji endelevu ili kuhakikisha uchumi endelevu wa bahari, kupunguza uchafuzi wa mazingira pamona na kulinda bioanuwai ya baharini. Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati akihutubia Mkutano wa Tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Bahari (UNOC3) akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano huo unaofanyika Jijini Nice nchini Ufaransa. Amesema hapana budi kuwa na hatua za ujasiri zikazoratibiwa kwa ufanisi ili kuhakikisha maendeleo makubwa katika uendelevu wa bahari. Makamu wa Rais ameongeza kwamba ni muhimu kuongeza ufadhili katika kushughulikia changamoto za bahari, kwa kuzingatia zaidi kusaidia nchi za kipato cha chini na nchi zinazoendelea za Visiwa Vidogo, ambazo zinakabiliwa na ufinyu wa bajeti na mizigo ya madeni inayokwamisha kufikia ahadi zilizofanywa za utekelezaji...

Waziri Mkuu:Serikali Yatenga Shilingi Bilioni 43 Kuimarisha Michezo Shuleni

_▪️Azindua mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA Iringa_ WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetenga sh. bilioni 43 ili kuimarisha michezo katika shule mbalimbali nchini na kati ya hizo, sh. bilioni 32 ni kwa ajili ya kuimarisha Chuo cha Michezo Malya. Amesema shilingi bilioni 11 zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza mpango wa kuboresha miundombinu ya michezo katika shule za sekondari 10 ambazo ni miongoni mwa shule teule 56 za michezo nchini. Ametoa kauli hiyo leo (Jumatatu, Juni 9, 2025) wakati akifungua mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi na Sekondari Tanzania (UMITASHUMTA na UMISSETA) kwenye viwanja vya Kichangani vilivyoko Kihesa, mkoani Iringa. Akielezea mikakati ya Serikali ya kuendeleza michezo na sanaa nchini, Waziri Mkuu amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejipanga kuimarisha Chuo cha Michezo Malya ili kiendelee kutoa mafunzo kwa kuzingatia utaalam na kuimarisha ufundishaji wa masomo ya michezo shu...