Skip to main content

Posts

Showing posts from October 27, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Tuhuma za rushwa zamkimbiza mgombea kura za maoni ccm musoma mjini

Na Ada Shadrack;Musoma. MWANYA wa rushwa umetajwa kuwa kichocheo cha kushinda uchaguzi wa kura za maoni kwa baadhi ya wagombea nafasi ya mwenyekiti wa serikali ya  mtaa   Mjini Musoma mkoani Mara. Hayo yamebainishwa na aliyekuwa mgombea nafasi hiyo kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (ccm) kata ya kitaji 'A' mzee Ally Z. Rajabu wakati akizungumza na waandishi wa habari. Mzee Ally z. Rajabu amesema uchaguzi huo umefanyika octoba 23 mwaka huu ambapo mgombea mwenzake Salma Ally alipata kura 97 akawa wa kwanza na kwamba yeye alipata kura 91 na kushindwa kinyang'anyiro hicho. Aidha baada ya kushindwa kupata nafasi hiyo Ally Z Rajabu aliamua kuhama chama hicho na kwenda chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) huku akiwa na nia ya kugombea tena nafasi hiyo kupitia chama hicho. " Baada  ya kukaa na kulinganisha vyama mbalimbali nikaapa sitakuwa na tajiri yoyote wa kumtegemea kunipa nguvu ya fedha ili nishiriki uchaguzi sipendi kabisa yawezekana pesa inaweza kunisaidia ...

Rais Mwinyi achangia millioni 100 ukarabati wa kanisa katoliki Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Hussein Ali Mwinyi  amesema Serikali itaendelea kuimarisha Uhuru wa Kuabudu  na  kuziagiza taasisi za Kidini kuendelea kuiombea nchi Amani na Umoja.  Rais Dk,Mwinyi amefahamisha kuwa  taasisi za Kidini  zina wajibu mkubwa wa kushirikiana na Serikali  na kuunga  Mkono  juhudi za  kuleta Amani,Umoja  na Mshikamano  wa Watanzania. Rais Dk, Mwinyi  ameyasema hayo leo tarehe 27 Oktoba 2024 alipozungumza  katika Maombi maalum  ya kumpongeza Askofu Agustino Shao  kwa utume wake  katika Kanisa Katoliki Jimbo la Zanzibar  na  maombi kwa Taifa  iliyofanyika Viwanja vya Mao Tse Tung Mkoa wa Mjini Magharibi. Rais Dk , Mwinyi  amesisitiza kuwa Serikali inathamini mchango mkubwa unaotolewa na Kanisa katoliki Jimbo la Zanzibar   kwani  umekuwa msaada muhimu  wa kuimarisha  ustawi wa jamii katika nyanja mbalimbali. Ak...

Waziri mkuu awataka watanzania kulinda utamaduni wetu kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania wahakikishe wanalinda utamaduni na kujenga misingi ya kuhamasisha vijana na vizazi vijavyo kutambua na kuenzi historia na urithi wa Mtanzania. Amesema kuwa ni wajibu wa kila Mtanzania kutunza utamaduni, mila na desturi kwa sababu utamaduni ni nguzo ya utambulisho wa jamii husika na ni muhimu kwa kizazi kijacho. Amesema hayo leo (Jumapili, Oktoba 27, 2024) wakati akifungua Tamasha la Buhaya 2024 ‘Buhaya Festival’ lililofanyika katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam. “Katika siku za sasa, ambapo teknolojia na utandawazi vinazidi kuimarika, ni rahisi kupoteza mila na desturi zetu, hivyo tunaposhiriki tamasha hili, tunajifunza na kuhamasisha jamii zetu kuhusu umuhimu wa urithi wetu wa kiutamaduni.” Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa amewaasa wazazi, jamii na madhehebu ya dini kuendelea kuhimiza utunzaji wa maadili kwa kuzingatia mila na desturi ili kuepuka mmomonyoko wa maadili kwa vijana na jamii kwa ujumla.  “Watanzania wote t...

Waziri mkuu mgeni rasmi buhaya festival

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Oktoba 27, 2024 ni mgeni rasmi katika Tamasha la Buhaya ‘Buhaya Festival’ linalofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Lengo la tamasha hilo ni kutangaza na kutambulisha fursa za vivutio vya utalii na uwekezaji vinavyopatikana mkoani Kagera. Aidha, Tamasha hilo pia linalotoa fursa ya kuenzi na kuendeleza mila na desturi za jamii ya Wahaya kutoka ndani na nje ya Mkoa wa Kagera.