Skip to main content

Posts

Showing posts from December 8, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Ngorongoro Wathibitisha Kuachana na Kuni inawezekana

📌Wajitokeza kwa wingi kujipatia majiko ya gesi ya ruzuku Wakazi wa Wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha wameitikia wito wa kutumia Nishati Safi ya Kupikia ikiwa ni hatua ya kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kulinda afya na kutunza mazingira. Hayo yamedhihirika Desemba 8,2024 Wilayani Ngorongoro wakati wa utekelezaji wa mradi wa usambazaji wa majiko ya gesi yanayotolewa kwa bei ya ruzuku ya 50% na Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa ushirikiano na Kampuni ya Lake Gas wilayani humo. Akizungumza wakati wa zoezi la usambazaji na uuzwaji wa majiko hayo ya ruzuku wilayani humo, Msimamizi wa Mradi wa REA Kanda ya Kaskazini (Kilimanjaro na Arusha), Mhandisi Gift Kombe aliwasisitiza wananchi kuzingatia elimu inayotolewa ya matumizi sahihi ya majiko hayo ili yaweze kuleta tija inayokusudiwa ikiwa na kuendelea kujaza mitungi hiyo pindi inapoisha. Wananchi wilayani humo kwa nyakati tofauti walishukuru kwa kufikiw...

Utiifu na Uchapakazi Vyaendelea Kumbeba Bashungwa

  Ni waziri kijana myenyekevu na msikivu ambaye tayari ameweka rekodi ya kuhudumu Wizara nyingi kama Waziri hapa nchini Mh Bashungwa huwezi mkuta anaropoka ropoka ovyo kwenye vyombo vya habari kufanya usanii katika majukumu yake,ni mtu anayeamini jambo na kulisimamia. Mfano nzuri juzi juzi wakati mvua zimekata mawasiliano ya mikoa ya Kusini,waziri huyu wa ujenzi ambaye sasa anaenda mambo ya ndani alikesha kwa msiku na mchana kuhakikisha daraja la muda linajengwa na mawasiliano yanarejea,huyu si waziri wa kujitapa Huwezi mkuta ana ugomvi na wenzie hata siku moja,ana heshimu mkubwa na mdogo Lakini ndio Waziri anaonekana kupitia Wizara zote nyeti na zile zinazoonekana zinachangamoto. *Huu ni mfano mzuri kwetu kama Vijana kuishi maisha ya mh Bashungwa  Endelea kuwa na moyo huo katika kulitumikia taifa lako kwa kumsaidia mh Rais kila anapoona unastahili kumsaidia

Rais Samia afanya Uteuzi wa Kimkakati

 Rais Dokta Samia Suluhu Hassan amefanya Uteuzi  na Mabadiliko ya Viongozi mbalimbali akiwemo Profesa Palamaganda Kabudi ambaye ameteuliwa kuwa waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Mhe.Jerry Slaa ameteuliwa kuwa waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.  Wengine ni Mhe. Abdalah Ulega ameteuliwa kuwa waziri wa Ujenzi huku Mhe.Innocent Bashungwa akiteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt.Moses Kusiluka,Gerson Msigwa ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa serikali, Kamishna wa Polisi CP Suzan Kaganda ameteuliwa kuwa Balozi na atapangiwa Kituo cha Kazi. Aidha Profesa Mohamed Yakub Janabi ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais wa Masuala ya afya na Tiba,Pamoja na Uteuzi huo Profesa Janabi ataendelea kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili

Rais Mwinyi:Tufanye Mazoezi Kuimarisha afya zetu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amefahamisha kuwa Tafiti zimeonesha kuwa  Mazoezi yanasaidia kwa kiasi kikubwa  kujenga Afya ya  Mwili ,afya ya akili  na kuondosha Msongo wa Mawazo na kusisitiza jamii kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi kila siku Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza  baada ya Kuongoza matembezi ya Afya  yalioandaliwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Taasisi ya Pharm  Access ikiwa ni kampeni maalum ya kudhibiti Maradhi yasioambukiza  kwa jamii  yalioanzia Kiembe Samaki kwa Boutros hadi Uwanja Mao Tse Tung Wilaya ya Mjini. Aidha Rais Dk.Mwinyi amesema Serikali itaendelea  kuchukua juhudi  maalum  kuhakikisha inapunguza kasi ya ongezeko la Maradhi yasiombukiza hapa nchini Rais Dk.Mwinyi   ameeleza kuwa  Takwimu za  Wizara ya Afya  zimeeleza kuwa  kuna Ongezeko la Maradhi Yasioambukiza kwa kiwango kikubwa ikwemo Kisukari, Presha ...

Mtendaji Mkuu Tarura akagua Miundombinu Dodoma

  -Ni maeneo yaliyoathiriwa na mvua katika jiji la Dodoma  -Atoa wiki mbili Kwa Mkandarasi kufanyia kazi mapungufu aliyoyabaini. Dodoma Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor Seff amefanya ziara ya kutembelea baadhi ya maeneo yaliyoathiria na mvua zilizonyesha kwa siku mbili. Katika ziara hiyo Mhandisi Seff alitembelea barabara ambazo zipo kwenye Mradi wa Uendelezaji wa Miji Tanzania Bara (TACTIC) katika maeneo ya Mkalama, Ilazo, Medeli na Swaswa-Mpamaa na kubaini mapungufu kadhaa.  Mradi huo wa TACTIC kwa Mkoa wa Dodoma unajenga barabara Km.10.19 na Mkandarasi 'China Geo Engineering Corporation' ambapo ilionekana amechelewa kutekeleza mradi huo na kusababisha athari eneo la Mkalama ambapo kuta za nyumba zimeanguka baada ya mvua kunyesha. “Hadi sasa ni zaidi ya miezi 11 tangu aanze kazi hii lakini maendeleo ya kazi ni 35% badala ya 70%,namuagiza awasilisha mpango kazi wake na endapo sitoona mabadikiko ndani ya wiki mbili ...