*#Wanachama 2,439 wa ACT wajiunga na CCM* Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Hussein Ali Mwinyi amezisisitiza Jumuiya za Chama Cha Mapinduzi kuwahamasisha Wanachama na Wananchi kujiandikisha na kujitokeza kwa Wingi kupiga Kura ili CCM ishinde kwa Kishindo. Dkt. Mwinyi ambae ni Mgombea Mteule wa Urais wa Zanzibar kwa Tiketi ya CCM ameyasema hayo alipozungumza na Wanachama na Wananchi Mauwani, Kiwani Mkoa wa Kusini Pemba Katika Mkutano Maalum wa Mapokezi yake baada ya Kuteuliwa hivi Karibuni kuwa Mgombea wa Urais wa Zanzibar. Dkt.Mwinyi amesema kumekuwa na tabia ya baadhi ya Wana CCM kutojitokeza kupiga kura wakati wa Uchaguzi jambo linaloipunguzia Kura za Ushindi Chama hicho. Aidha, Rais Dkt. Mwinyi ameipongeza UWT kwa kazi nzuri walioifanya ya Uhamasishaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura na kuiagiza kuendelea na mwamko huo. Hali kadhalika Dkt.Mwinyi amewapongeza na kuwakaribisha Wanachama 2,439 wa Chama cha ACT Wazalendo kwa Uamuzi wa Kujiunga na CCM...
Marato tv - Sauti ya Jamii