Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza limeendelea kuimarisha hali ya ulinzi na usalama katika maeneo yote majini na nchi kavu kupitia doria na misako inayo endelea. Kupitia misako hiyo iliyofanyika siku mbili tarehe 15 na 16 mwezi huu zaidi ya watuhumiwa 30 wa makosa mbalimbali wamekamatwa katika visiwa vya Soswa, Chembaya, Chamagati na Nyamango katika Halmashauri ya Buchosa, wilaya ya Sengerema. Akizungumza na wananchi wa Kisiwa cha Soswa Januari 16.2025 kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Wilbrod Mutafugwa ameonya vikali baadhi ya watu wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu katika maeneo ya visiwani wakiwemo baadhi ya viongozi wa vijiji wanaoshindwa kutoa ushirikiano na kuwaficha wahalifu katika maeneo yao. "Viongozi wa vijiji mnawajibu wa kusaidia kuundwa kwa vikundi vya ulinzi shirikishi ili kudhibiti vitendo vya uhalifu vinavyoanza kuchipuka kwenye maeneo yenu na sio kuwaficha wahalifu" ameonya kamanda Mutafugwa Kamanda Mutafungwa, amesema kuwa oper...
Marato tv - Sauti ya Jamii