Skip to main content

Posts

Showing posts from October 17, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt.Nchimbi Awasalimia Wananchi Wa Mikumi Akielekea Kilombero

Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwasalimia na kuwahutubia Wananchi wa kata ya Kidoma,Mikumi wakati akielekea kwenye mkutano wake mwingine wa kampeni katika kata ya Mwaya,Kilombero mkoani Morogoro leo Oktoba 18,2025. Baada ya kuwasalimia Wananchi wa eneo la Mikumi,Dkt. Nchimbi alitumia nafasi hiyo kumuombea kura za ushindi wa kishindo mgombea Urais wa chama hicho,Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na kumnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Mikumi,Ndugu Dennis Lazaro LONDO pamoja na Madiwani. Balozi Nchimbi anafikia mkoa wa 25 sasa tangu kuzinduliwa kwa kampeni hizo Agosti 28,2025 jijini Dar es Salaam,akiendelea kusaka kura za ushindi wa kishindo za mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi,Dkt.Samia Suluhu Hassan,Wabunge na Madiwani.

Dkt.Nchimbi Awasili Morogoro Kuendelea Na Mikutano yake ya Kampeni

Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emmanuel John Nchimbi amewasili  mkoani Morogoro leo Oktoba 18,2025 kuendelea na mikutano yake ya hadhara ya kampeni ya kusaka kura za ushindi wa Kishindo za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan,Wabunge na Madiwani.  Kwa mujibu wa ratiba ya leo,Dkt.Nchimbi atafanya mikutano mitatu. Mkutano wa kwanza utakuwa ni wa kuwasalimia Wananchi katika kata ya Kidoma,Mikumi na mkutano mwingine  utafanyika kata ya Mwaya,Kilombero na wa tatu utakuwa Mtimbira,Malinyi.

Dkt.Nchimbi Aomba Kura Dodoma Mjini, Leo Kuanza Kampeni Morogoro

MGOMBEA Mwenza  wa urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amesema miongoni mwa mipango ya chama hicho kwa miaka mitano ijayo kikirudi tena madarakani ni kujenga Maktaba ya Taifa mkoani Dodoma. Dkt. Nchimbi ameyasema hayo leo Oktoba 17, 2025, katika mkutano wake wa hadhara wa kampeni za CCM uliofanyika Wilaya ya Dodoma Mjini alipokuwa akimuombea kura mgombea urais wa chama chake Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na wagombea ubunge na udiwani ikiwa zimesalia siku 12 kabla ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025. “Maktaba hiyo itahifadhi kumbukumbu, nyaraka na maandiko mbalimbali ya kitaifa, na itatumiwa na watafiti, wanafunzi na wananchi kwa ujumla kwa maslahi ya taifa.” Aidha Dkt.Nchimbi ameeleza kuwa Serikali ya  CCM pia imedhamiria kujenga shule mpya za msingi 21 na sekondari 16, madarasa 150, maabara 15 za sayansi na mabweni 17 ili kuboresha mazingira ya elimu na kupunguza msongamano darasani. Hata hivyo baada ya kufanya mkutano wa kampeni katika Wila...

Balozi Dk. Nchimbi Ahitimisha Kampeni Mkoa wa Dodoma, Akitaja Uimara wa Ccm

#HABARI :  MGOMBEA Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Emmanuel Nchimbi, leo Oktoba 17, 2025, amehitimisha kampeni zake katika Mkoa wa Dodoma, ambapo maelfu ya wananchi walijitokeza kumsikiliza akiwasilisha sera na ahadi zilizomo katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM. Katika ziara yake ya kampeni mkoani humo, Dk. Nchimbi amefanya mikutano mikubwa katika wilaya za Mpwapwa, Kongwa, Kondoa na Dodoma Mjini, akisisitiza dhamira ya CCM kuendeleza utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo katika sekta za afya, elimu, kilimo, maji na miundombinu, ikiwemo ujenzi wa barabara na reli ya kisasa (SGR) kutoka Dodoma–Kigoma na Dodoma–Mwanza, endapo wananchi watakipatia chama hicho ridhaa ya kuendelea kuongoza kwa miaka mitano ijayo. Amesema, Serikali ya CCM pia imepanga kukamilisha ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato, pamoja na ujenzi wa uwanja mkubwa wa mpira wa miguu jijini Dodoma, ambao utatumika kwa mashindano ya AFCON 2027, ikiwa...

Wasira: Miaka Mitano Ijayo ni Neema ya Uchumi Kwa Mara

Na Mwandishi Wetu, Serengeti MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amewaeleza wananchi wa Mkoa wa Mara kuwa, Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2025-2030,  imebeba matumaini makubwa kupitia miradi ya maendeleo ambayo itafungua uchumi na kukuza uchumi. Amesema miongoni mwa miradi mikubwa ambayo imeahidiwa na ilani kujengwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo ni bandari ya Musoma na uwanja wa ndege wa Serengeti. Wasira ameeleza hayo leo Oktoba 17, 2025 katika mji wa Mugumu wilayani Serengeti Mkoa wa Mara, alipokuwa akizungumza na viongozi wa CCM kumwombea kura mgombea urais wa CCM, Dk. Samia Suluhu Hassan, wagombea ubunge na udiwani waliosimamishwa na Chama kwa uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, mwaka huu. "Tunataka kujenga uchumi shirikishi na kuweka miundombinu itakayofanya uchumi ukue, moja tunajenga kiwanja cha ndege katika mji wa Mugumu, cha kisasa na kazi imeshaanza ya kufanya 'survey' ya kile kiwanja na kwenye ilani tumeyaandika, mimi mwenyewe ...