Skip to main content

Posts

Showing posts from November 14, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu Mwigulu Akipongezwa Na Waziri Mkuu Mstaafu Kassim Majaliwa

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba akipongezwa na Waziri Mkuu Mstaafu Kassim Majaliwa baada ya uapisho uliofanyika Chamwino Ikulu jijini Dodoma Novemba 14, 2025.

Dhahabu Yenye Thamani ya Trilioni 8.8 Yachimbwa Mara

🔸Mafanikio Makubwa ya Sekta ya Madini chini ya Serikali ya Awamu ya Sita Mara MKOA wa Mara umeweka rekodi mpya katika uzalishaji wa madini baada ya kuzalisha dhahabu yenye uzito wa tani 67.41, ikiwa na thamani ya Shilingi Trilioni 8.881 katika kipindi cha miaka minne, kuanzia mwaka 2021 hadi Oktoba 2025. Akizungumza kwa niaba ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mara, Afisa Mazingira, Byalugaba Chakupewa, hivi karibuni alisema mauzo ya dhahabu hiyo yamechangia mapato ya Serikali zaidi ya Shilingi Bilioni 605.86 kupitia mrabaha, ada za ukaguzi na tozo mbalimbali. Aidha, Chakupewa alisema kuwa Serikali kupitia Tume ya Madini mkoani Mara imekusanya maduhuli ya Shilingi Bilioni 78.7 katika robo ya kwanza ya mwaka, sawa na asilimia 37.48 ya lengo la mwaka la Shilingi Bilioni 210.3. Kwa mujibu wake, ofisi hiyo pia imetoa leseni 2,478 za shughuli za madini, hatua iliyosaidia kuongeza ajira, kuchochea uwekezaji na kuimarisha mapato ya halmashauri. Alibainisha kuwa mafanikio hayo yanatokana na usi...

Rais Dkt. Samia Amuapisha Dkt. Mwigulu Kuwa Waziri Mkuu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika hafla iliyofanyika Chamwino Ikulu jijini Dodoma Novemba 14, 2025.