Skip to main content

Posts

Showing posts from January 9, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Jokate awapa Tano Vijana Kwa Maandalizi Mazuri ya Mkutano Mkuu Ccm

Na Mwandishi Wetu KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM)Jokate Mwegelo amesema jumuiya hiyo imeridhishwa na kazi kubwa na nzuri iliyofanywa na vijana wa chama hicho ya kuandaa ukumbi kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa CCM . Mkutano huo unatarajia kufanyika Januari 18 hafi 19 mwaka huu jijini Dodoma na utaongozwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa,Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.  Akizungumza leo Januari tisa jijini Dodoma baada ya kukagua kaz iliyofanywa na vijana wa jumuiya hiyo kuandaa ukumbi , Katibu Mkuu Jokate Mwegelo amesema wao kama vijana wa chama wameridhishwa na maandalizi ya mkutano huo. “Tumekuja kukagua na kujionea kazi iliyofanywa na vijana wetu wa mkoa wa Dodoma wakiongozwa na Mwenyekiti wa Mkoa na Katibu wa mkoa . “Chama chetu kina vijana wenye fani tofauti tofauti na wamedhihirisha kwa kazi waliyoifanya katika kufanya maandalizi kuelekea Mkutano Mkuu, hivyo sisi kama viongozi tumeridhishwa na kazi kubwa na nzuri iliyofanywa na vijana ...

Dkt Gwajima aagiza Kuundwa Kamati za Ulinzi wa Watoto

Na Allan Kitwe, Tabora SERIKALI imeelekeza shule zote nchini kuhakikisha zinaunda Kamati za Ulinzi wa Watoto ili kukabiliana na vitendo vya ukatili na maadili yasiyofaa kwa watoto ambayo hupelekea kuiga tabia mbaya hivyo kushindwa kutimiza ndoto zao. Agizo hilo limetolewa jana na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Dkt Doroth Gwajima alipokuwa akiongea na wakazi wa Jimbo la Ulyankulu, Wilayani Kaliua katika siku ya 1 ya ziara yake Mkoani hapa. Amesema kuwa serikali ilishatoa Mwongozo wa kuundwa Kamati za Ulinzi wa Watoto katika shule zote hivyo ni muhimu sana Kamati hizo zikaanzishwa shule zinapofunguliwa ili watoto wanasome na kumaliza wakiwa na maadili mazuri. Waziri Gwajima amesisitiza kuwa Kamati hizi zitasaidia sana kumlinda mtoto na vitendo vya ukatili ikiwemo kumwepusha kujiingiza katika michezo michafu ya ulawiti, usagaji, ushoga na mingineyo. Aidha amewataka wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kukaa na watoto wao vizuri, kuwafundisha maadili mema n...

Rais Samia amefanya Mazungumzo na Wakuu wa Misheni za Uangalizi wa Chaguzi za SADC (SEOM)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na mmoja wa Wakuu wa Misheni za Uangalizi wa Chaguzi za SADC (SEOM) Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mizengo Pinda, katika Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar tarehe 09 Januari 2025.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na mmoja wa Wakuu wa Misheni za Uangalizi wa Chaguzi za SADC (SEOM) Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anna Makinda na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo katika Ikulu Ndogo ya Tunguu, Zanzibar tarehe 09 Januari 2025. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na mmoja wa Wakuu wa Misheni za Uangalizi wa Chaguzi za SADC (SEOM) Mhe. Jaji Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mohammed Chande Othman na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo...

Bashungwa Kuzindua Mikakati ya Mawasiliano ya Wizara ya Mambo ya Ndani na Vyombo vyake Vya Usalama

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amewasili Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Msalato Dodoma ambapo atazindua Mikakati 6 ya Mawasiliano ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Vyombo vya Usalama ambavyo Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Idara ya Uhamiaji pamoja na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), leo tarehe 09 Januari 2025. Aidha, Bashungwa atafungua Kikao Kazi cha Mwaka, cha Wasemaji wa Vyombo vya Usalama vya Wizara yaani Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.  Hafla hiyo imehudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ally Gugu, Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Maduhu Kazi na Wakuu wa Vyombo vya Usalama na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango afanya Mazungumzo na Viongozi wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akifanya mazungumzo na Viongozi wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Barke Sehel, mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 08 Januari 2025. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Barke Sehel (Watatu kutoka kushoto), mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 08 Januari 2025. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiagana na Viongozi wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Barke Sehel (wa kwanza kutoka kushoto), mara baada ya mazungum...

Dkt. Biteko aagiza Kituo cha Huduma kwa Wateja Tanesco Kusukwa Upya

📌Akerwa na kusuasua kwa utendaji wa Kituo hicho 📌Awataka watendaji kuondokana na kufanya kazi kwa mazoea 📌Ahoji sababu za kutelekezwa kwa maelekezo yake ya 2024 *Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishti* Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameagiza kufumuliwa kwa Kituo cha Huduma kwa Wateja  cha Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO) kufuatia kituo hicho kushindwa kuwahudumia Wananchi kwa viwango vinavyotarajiwa. Ametoa agizo hilo leo tarehe 9 Januari,  2025 jijini Dar es Salaam baada ya kutembelea kituo hicho pamoja na mambo mengine kufuatilia utekelezaji wa maelekezo yake aliyoyatoa mwezi Aprili, 2024. Dkt. Biteko ameshangazwa na hatua ya TANESCO kuweka kando maelekezo ya mwezi Aprili 2024 yaliyolitaka Shirika hilo kuondokana na  matumizi ya namba za kulipia kwenye utoaji wa huduma na kuomba namba ya bure ya huduma (free toll number) kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania -TCRA ili kuwapa unafuu wananchi wanaohitaji huduma za TANESCO. "...