Na Hamida Ramadhan, Dodoma Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Xavier Daudi amesema Wananchi walio wengi wamekuwa wakitumia mitandao ya Kijamii kufikisha malalamiko yao kwenye Taasisi za Serikali kutokana na baadhi ya Watumishi wa Umma kuvujisha siri za wateja wao pindi wananchi hao wanapotumia mifumo rasmi kutoa mrejesho Amesema vitendo hivyo vimekuwa vikiwakatisha tamaa Wananchi wenye nia njema ya kuona Serikali inakuwa kinara wa kutoa huduma bora kwa wananchi wake. Daudi ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo maalum ya siku tatu kwa Maafisa Mrejesho kuhusu uendeshaji wa mfumo wa e-Mrejesho katika Ofisi za Umma Amewataka Maafisa hao kutunza siri za wateja wao ili kuwafanya Wananchi kuwa huru kuwasilisha changamoto zinazowakabili wakati wowote na mahali popote pasipo kulazimika kutumia mitandao ya kijamii Amesema kuwa, Mfumo wa e-Mrejesho unampa fursa mwananchi kut...
Marato tv - Sauti ya Jamii