Skip to main content

Posts

Showing posts from April 16, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais Mwinyi:Tutangaze Fursa za Uwekezaji na Kuzingatia Diplomasia ya Uchumi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi amewasisitiza Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika Nchi mbalimbali kuzingatia Diplomasia ya Uchumi na Kuzitangaza fursa za Uwekezaji ziliopo. Rais Dkt, Mwinyi ameyasema hayo   alipozungumza  na Mabalozi wa  Tanzania wa Nchi za Rwanda,Zimbabwe ,Sweden na Msumbiji Waliofika Ikulu kumuaga  kabla ya kwenda katika Vituo vyao vya Kazi Baada ya kuteuliwa hivi karibuni. Amewahimiza Mabalozi  hao kufanya Juhudi Maalum za kuitangaza Sera ya Uchumi wa Buluu na Utalii katika Mataifa hayo Ili kuvutia Wawekezaji Zaidi kuwekeza  Nchini. Amesema Zanzibar bado inahitaji Wawekezaji wengi Hususan katika Sekta hizo Kuu za kipaumbele kutokana na kuwepo kwa fursa nyingi ikiwemo Uvuvi,Utalii na Mafuta na Gesi. Halikadhalika Rais Dkt, Mwinyi ameeleza kuwa  Suala la Mahusiano ya Kimataifa hivi sasa limeelekezwa zaidi katika Uchumi hivyo wanapaswa kuzingatia zaidi Kuimarisha Uhusiano wa Kiuchu...

Waziri Aweso aelekeza kufanyika utafiti wa kina wa upatikanaji wa maji Dodoma Jiji

  ▪️Aagiza kuongezwa mitambo zaidi ya uchimbaji visima Dodoma Jiji ▪️Akagua miradi ya Maji eneo la Nala na Nkuhungu ▪️Miradi ya visima vinavyochimbwa kuzalisha maji lita 32m ▪️Hatua hizi kupunguza ukali wa mgao wa maji Jijini Dodoma Waziri wa Maji Mh. Jumaa Aweso amewataka wataalamu wa Wizara ya Maji kuhakikisha wanaongeza nguvu ya utafiti wa kina wa maji katika Jiji la Dodoma ili kusaidia upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wa Jiji la Dodoma. Waziri Aweso ameyasema hayo wakati akikagua miradi ya maji wa Nala unaogharimu Tsh 3.8 bn na Uchimbaji wa Visima katika kata ya Nkuhungu na maeneo mengine ya Jiji mradi wenye thamani ya Tsh 41bn. “Ni maelekezo ya Mh Rais Dkt. Samia S . Hassan kuhakikisha tunatatua changamoto ya maji Jijini Dodoma na ndio maana zimetolewa fedha zaidi ya Tsh 45bn kupelekea upatikanaji wa maji. Ninaelekeza wataalamu wa wizara kuhakikisha unafanyika utafiti wa kina wa upatikanaji wa maji Dodoma Jiji kwa kuchimba visima virefu maeneo mbalimbali. Ninael...

Rais mstaafu Jakaya Kikwete awasilisha ujumbe wa Rais Samia kwa Rais wa Niger

  Rais Mstaafu wa Tanzania na Mjumbe Maalum wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amefanya mazungumzo na Rais wa Niger, Mhe. Jenerali Abdourahamane Tchiani katika Ikulu ya Niamey April 16, 2025. Katika mazungumzo hayo, Mhe. Kikwete ambaye ni mwanadiplomasia nguli aliwasilisha Ujumbe Maalum wa Rais Samia kwa Jenerali Tchiani Aidha, katika mazungumzo hayo, Mhe. Kikwete aliwasilisha salamu za Rais Samia ambapo alielezea kufurahishwa na uhusiano mzuri wa kidiplomasia uliopo kati ya Tanzania na Niger na kusisitiza umuhimu wa kukuza na kuuimarisha zaidi katika nyanja za biashara, uwekezaji na utalii.  Alisisitiza umuhimu wa nchi za Afrika kubadilishana uzoefu na ujuzi ili utajili mkubwa wa maliasili uliopo uweze kuvunwa na kuendelezwa kwa faida ya wananchi wa bara hilo.

Wafanyabiashara ya ngono Nchini Kenya wahofia maisha kufuatia uhaba wa kondomu

  UHABA mkubwa wa kondomu na dawa za kuzuia maambukizi ya virusi vya Ukimwi kabla ya mtu kuambukizwa (PrEP) katika jiji la Nakuru na miji mingine unahatarisha vita dhidi ya Ukimwi na magonjwa mengine ya zinaa nchini Kenya. Huduma za bure katika hospitali na vituo vya afya kusaidia makundi maalum kama wafanyabiashara wa ngono zimekwama baada ya bidhaa hizo muhimu kukosekana. Uhaba huo umeweka hatarini afya na maisha ya zaidi ya wafanyabiashara wa ngono 4,000 wanaofanya kazi katika barabara kuu ya Nairobi-Nakuru-Eldoret — hususan maeneo ya Mai Mahiu, Longonot, Naivasha, Gilgil, Kikopey, Pipeline, Salgaa na Sachangwan. Barabara hii ni kiungo muhimu katika usafiri katika Barabara Kuu inayounganisha Kenya na mataifa kama Uganda, Sudan Kusini, Rwanda na Burundi. Kwa sababu hiyo, mtangusano wa madereva wa malori na wafanyabiashara wa ngono huongeza hatari ya maambukizi ya Ukimwi. Mwenyekiti wa kundi la  Smart Ladies , linalowakilisha wafanyabiashara wa ngono katika eneo hilo, Bi Dais...

Serikali Itamuenzi Mhandisi Nyamo-hanga

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko leo tarehe 16 Aprili, 2025 amewaongoza waombolezaji katika mazishi ya Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Boniphace Gissima Nyamohanga yaliyofanyika katika eneo la Mikungani, Wilaya ya Bunda.  Akizungumza katika mazishi hayo, Mhe. Biteko amesema Mhandisi Nyamohanga alikuwa ni hazina kubwa ya mipango inayopimika ndani ya Serikali na amefanya kazi kubwa ndani ya TANESCO, REA na Wizara ya Nishati kwa ujumla.  Mhe. Biteko amesema kazi kubwa alizozifanya kuwa ni pamoja na ukamilishaji wa mradi wa Bwawa la kuzalisha umeme la Nyerere na uanzishaji na utekelezaji wa mpango wa Tanzania kuanza kuuza umeme katika nchi ya Zambia.   “Sahihi yake aliyoiweka wakati wa kufunga mkataba kati ya Tanzania na Zambia itaendelea kuwepo katika mkataba huo muda wote kutukumbusha Kazi kubwa aliyoifanya Mhandisi Nyamohanga katika sekta ya Nishati” amesema Mhe. Biteko.  Naibu Waziri Mkuu...

Tamisemi Yaomba Trilioni 11.78 Bajeti 2025/2026

OR-TAMISEMI  OFISI ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)  imewasilisha bungeni makadirio ya mapato kwa mwaka 2025/26 yenye takribani Shilingi trilioni 11. 783 kwa ajili ya wizara na taasisi zilizo chini yake. Bajeti hiyo imeongezeka kutoka Shilingi trilioni 10.125  zilizotengwa mwaka 2024/25 hadi kufikia Shilingi trilioni 11.783 na kuwa na ongezeko la   zaidi ya Sh trilioni 1.66. Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa iamesema Shilingi trilioni 3.95 zinaombwa kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo ambapo kati ya fedha hizo Shilingi trilioni 2.5 ni fedha za ndani, ikijumuisha Shilingi bilioni 613.44 za mapato ya ndani ya halmashauri na Shilingi trilioni 1.45 ni fedha za nje. Pia amesema Shilingi trilioni 7.84 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida yanayojumuisha mishahara Shilingi trilioni 6.3 na matumizi mengineyo Shilingi trilioni 1.53 ikijumuisha Shilingi trilioni 1. 067 za mapato ya nd...

Wanawake Kuwezeshwa Katika Matumizi ya Tehema - Naibu Katibu Mkuu Mpanju

Na WMJJWM - Dodoma  Serikali ya Tanzania inaendelea kushirikiana na Serikali ya Ujerumani katika uhamasishaji wa wanawake kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano ili kukuza ujuzi pamoja na kujijenga wenyewe na kuleta usawa wa kijinsia. Hayo yamesemwa Aprili 16, 2025 jijini Dodoma na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wakili Amon Mpanju, wakati wa kikao kazi na wawakilishi kutoka Ubalozi wa Ujerumani kujadili mashrikiano katika mradi wa kuhamasisha wanawake kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA), kwa maendeleo yao. Wakili Mpanju amesema lengo la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Mhe. Dkt. Samia Hassan Suluhu ni kuhakikisha Wanawake wanapata fursa sawa za kidigitali, usawa wa kijinsia ikiwa ni pamoja na kushiriki ipasavyo katika matumizi ya teknolojia ya Tehama.  Amesema kwamba ,Wizara ipo katika maandalizi ya kuingia makubaliano na Serikali ya Ujerumani juu ya kuwezesha wanawake na wasichana k...