📌Kamati ya kitaifa yakutana kwa ajili ya maandalizi na kutoa mwelekeo wa ushirikiano wa Wizara 📌Maliasili yajipanga kuleta wanyama hai na kutangaza vivutio vya Utalii Dodoma 📌Taasisi zajipanga kutoa huduma bora kwa wananchi Na Neema Chalila Mbuja, Dodoma KAMATI ya kitaifa ya Kuratibu maandalizi ya Sikukuu ya Wakulima (Nanenane) kwa Wizara ya Maliasili na Utalii na taasisi zake imekutana leo Julai 21,2026 Jijini Dodoma na kuazimia kutoa huduma bora kwa wananchi ili watambue kazi na majukumu ya Wizara na taasisi zake. Akizungumza na kutoa maelekezo ya namna ya kuboresha ushiriki wa Wizara ya Maliasili na Utalii na taasisi zake kwenye maonesho ya nanenane, Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Utalii, Richard Wandwi amesema, ushiriki wa Wizara kwa mwaka huu unapaswa kuwa wa kiubunifu na kutangaza maeneo ya vivutio vya utalii kwa Mkoa wa Dodoma kama ilivyoainishwa kwenye mkakati wa uendelezaji utalii kwa mkoa wa Dodoma uliozinduliwa na Waziri Mkuu, Mhe Dkt Mwigulu Nchemba. ‘’ Naomb...
Marato tv - Sauti ya Jamii