Skip to main content

Posts

Showing posts from August 1, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

MICHEZO YAIMARISHA USHIRIKIANO TANZANIA NA CHINA

Sekta ya michezo  imekua daraja la kuimarisha urafiki, mshikamano na ushirikiano kati ya Tanzania na China kupitia ushirikiano kwenye sekta hiyo ikiwemo uwekezaji katika  miundombinu, biashara na elimu. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali,  Gerson Msigwa, leo Agosti 1, 2026, wakati akifungua Mashindano ya 13 ya Mpira wa Kikapu ya Chama cha Wafanyabiashara wa China (Tanzania) katika viwanja vya Don Bosco, Oysterbay, Dar es Salaam. Msigwa amesema, Tanzania na China zina ushirikiano wa muda mrefu, ambao umeleta maendeleo kwa nchi hizo, huku akiishukuru Serikali ya China kwa mchango wake katika  sekta ya michezo nchini na kuhimiza uwekezaji zaidi kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Kwa upande wake Balozi wa China hapa  Bi. Chen Mingjian, alisema michezo inaendelea kuimarisha uhusiano wa kihistoria kati ya Tanzania na China, huku Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa China nchini Tanzan...

RAIS SAMIA ATOA WITO KWA BARA LA AFRIKA KUJITEGEMEA ΚΑΤΙΚΑ MASUALA YA AFYA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa wito kwa mataifa ya Afrika kuwekeza katika huduma za afya za kibingwa ili kupunguza gharama na utegemezi wa matibabu nje ya Bara hilo. Rais Dkt. Samia amesema hayo leo tarehe 01 Agosti, 2026, jijini Luanda baada ya kufungua Hospitali ya Rais Julius Nyerere ya Matibabu ya Majeraha ya Moto, akiambatana na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Angola, Mheshimiwa João Manuel Gonçalves Lourenço. Amesema hospitali hiyo ni ushahidi kuwa ndoto ya Angola ya kubadilisha sekta ya afya kwa kuboresha upatikanaji wa huduma za kisasa za afya ndani ya nchi, inaendelea imetimia. Aidha, ameipongeza Angola kwa kuimarisha huduma za matibabu ya kibingwa, ikiwemo matibabu ya majeraha makubwa, majeraha ya moto, macho na maeneo mengine yanayohitaji teknolojia na utaalamu wa kiwango cha juu. Rais Dkt. Samia amesema uwekezaji huo utaongeza uwezo wa Angola kutibu wananchi wake ndani ya nchi na kupunguza gharama za kuwapeleka wa...

MBUNGE SURATI AIKABIDHI TANESCO GARI, AKAGUA MRADI WA UMEME WA BILLIONI 3.9 SERENGETI

 MBUNGE wa Jimbo la Serengeti, Mheshimiwa Mary Daniel Surati, amekabidhi gari kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Wilaya ya Serengeti ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha utendaji wa shirika hilo na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa miradi ya kusambaza umeme kwa wananchi. Makabidhiano hayo yaliyofanyika Julai 31, 2026, yanatarajiwa kusaidia TANESCO kuwafikia wananchi kwa haraka zaidi katika utekelezaji wa miradi ya umeme pamoja na kuboresha huduma kwa wakazi wa Serengeti. Baada ya hafla hiyo, Mbunge Surati alikagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Umeme cha Nyamongo Mugumu (Nyamongo Mugumu Power Station), mradi wenye thamani ya shilingi bilioni 3.9 unaotekelezwa kwa lengo la kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika wilayani humo. Akiwa eneo la mradi, ameeleza kuridhishwa na hatua iliyofikiwa huku akisisitiza umuhimu wa kuhakikisha kazi zinakamilika kwa wakati ili wananchi waanze kunufaika na huduma bora ya umeme. Mradi huo unatarajiwa kukamilika ifikapo Agosti 30, 202...

VIJANA WAPIGA DEBE MKATA WAVUNJA REKODI, WANUNUA COASTER KWA MKOPO WA HALMASHAURI

 Na Mashaka Mhando, Handeni HATUA ya Serikali ya Awamu ya Sita kuwezesha makundi maalum kiuchumi imeanza kuzaa matunda makubwa Wilayani Handeni, baada ya kikundi cha vijana waliokuwa madereva, makondakta, na wapiga debe eneo la Mkata kufanikiwa kununua gari la abiria aina ya Toyota Coaster. Mafanikio hayo makubwa yamefikiwa kupitia mkopo wa Shilingi Milioni 90 utokanao na asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kwa mwaka wa fedha 2025/2026. Taarifa ya mafanikio ya vijana hao imetolewa Leo Augosti 1, mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Tanga, wakiongozwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Bw. Mohammed Salim, waliokuwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo. Akiwasilisha taarifa ya mradi huo unaomilikiwa na kikundi hicho cha vijana cha Mkata, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Saitoti Stephen, alisema mradi mzima unagharimu Shilingi Milioni 100.  Saitoti alifafanua kuwa, kati ya fedh...

MAMA MARIA APONGEZWA KWA ZAWADI YA PICHA YA MWALIMU

 Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere akipokea zawadi ya picha ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere baada ya hafla ya uzinduzi wa Hospitali Kuu ya Rufaa ya Rais Julius Nyerere (Hospital dos Queimados Presidente Julius Nyerere) iliyopo Kilamba, jijini Luanda, Angola, tarehe 01 Agosti, 2026.

MBUNGE SURATI AZINDUA AWAMU YA PILI YA SAMIA UTHUBUTU AWARDS

 MBUNGE wa Jimbo la Serengeti, Mheshimiwa Mary Daniel Surati, amehitimisha kwa mafanikio awamu ya kwanza ya programu ya Samia Uthubutu Awards na kuzindua rasmi awamu ya pili ya mpango huo unaolenga kuibua vipaji, kukuza ubunifu na kuwajengea wanafunzi uwezo wa kufikiri kwa ubunifu ili kuwa sehemu ya maendeleo ya Taifa. Programu hiyo ilitekelezwa katika shule 30 za sekondari, zikiwemo shule 25 za Wilaya ya Serengeti na 5 za Wilaya ya Tarime, ambapo wanafunzi walishindana kupitia mawazo na bunifu mbalimbali zilizoonesha uwezo wao wa kutatua changamoto za kijamii na kiuchumi. Katika mashindano hayo, Makundusi Sekondari iliibuka mshindi wa kwanza na kujinyakulia Shilingi 1,000,000, kombe, vyeti vya ushindi pamoja na fursa ya kipekee ya kutembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mheshimiwa Mary Surati amesema yeye mwenyewe atawaongoza washindi hao katika ziara hiyo ya kielimu ili kuwapa nafasi ya kujifunza shughuli za Bunge na uongozi wa nchi. Nafasi ya pili ilikwenda kwa SEDE...

STANBIC BANK PUMPS TZS 30 MILLION INTO 13TH CHINA ENTERPRISES BASKETBALL TOURNAMENT

 Msigwa, Amb. Chen lead opening ceremony in Dar By Prosper Makene  Dar es Salaam, Tanzania – Saturday, August 1, 2026: Stanbic Bank Tanzania_ has reaffirmed its commitment to community engagement and bilateral trade with a TZS 30 million sponsorship of the 13th Annual Chinese Enterprise Association (Tanzania)'s Basketball Tournament, which officially kicked off on Saturday at Don Bosco Grounds, Oysterbay. The sponsorship was announced as Gerson Msigwa, Permanent Secretary, Ministry of Information, Culture, Arts and Sports who is also government spokesperson, officially declared the tournament open in the presence of _Her Excellency Chen Mingjian, Ambassador of the People’s Republic of China to Tanzania, senior government officials, and representatives of major Chinese-funded companies operating in Tanzania. The tournament, organized by the Chinese Enterprise Association (Tanzania), brings together Chinese enterprises in the country and will run from August 1 to August 8, 2026...

MSIGWA: SERIKALI INAIPONGEZA STANBIC KWA KUUNGA MKONO MICHEZO

 Na Prosper Makene  Dar es Salaam, Tanzania – Jumamosi, 1 Agosti 2026: Serikali imeipongeza Stanbic Bank Tanzania kwa mchango wake wa muda mrefu katika kuunga mkono michezo nchini, hususan kupitia udhamini wa Mashindano ya 13 ya Mpira wa Kikapu ya Jamii ya Wachina. Pongezi hizo zimetolewa na Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Gerson Msigwa wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo yaliyofanyika katika Viwanja vya Don Bosco, Namanga. Mashindano hayo yamedhaminiwa na Stanbic Bank kwa Shilingi milioni 30. Msigwa alisema ushiriki wa sekta binafsi katika michezo ni muhimu kwa kuwa unasaidia kukuza vipaji, kuimarisha afya ya jamii na kujenga mahusiano baina ya watu. "Naipongeza Stanbic Bank kwa kuendelea kudhamini mashindano haya kwa miaka mingi. Ushirikiano wa namna hii kati ya sekta binafsi na jamii unachangia kuimarisha mahusiano kati ya wananchi wa mataifa yetu mawili na kudhihirisha urafiki wa kudumu uliopo kati ya China na Tanzania," alisema Msigwa. H...

DKT. MWIGULU: TUBORESHE VIWANGO KWENYE BIDHAA*

WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba ametoa wito kwa wazalishiaji mbalimbali nchini waboreshe bidhaa zao ili zimudu ushindani wa kimataifa na ziweze kushindana kila siku na siyo wakati wa maonesho tu. “Bidhaa ambazo tuko nazo zisiwe kwa ajili ya maonesho, bali ndiyo iwe standard ya bidhaa zetu katika maisha yetu. Tukishafikia hatua hiyo, tutakuwa tumetatua mambo mengi kwa mpigo ikiwemo kujihakikishia kwamba bidhaa zetu zinapata soko, ni lazima tuendelee kuoanisha uzalishaji na vigezo vya kimataifa vya masoko,” amesema. Waziri Mkuu amesema hayo leo (Jumamosi, Agosti Mosi, 2026) wakati akizungumza na mamia ya wananchi waliohudhuria ufunguzi wa Maonesho ya 33 ya Kitaifa ya Wakulima (Nanenane), yaliyofunguliwa rasmi katika Viwanja vya Dkt. John John S. Malecela, Nzuguni, jijini Dodoma. Amesema kufanya hivyo kutawezesha bidhaa zinazozalishwa kupata masoko popote duniani kutokana na ubora utakaokuwa nazo. “Tutengeneze bidhaa zetu za kila siku kama vile za kwenda kwenye maonesho. Katika maeneo me...