BAADHI ya manifesto ambazo aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Amolo Odinga alitumia katika kampeni zake za urais zitakuwa sehemu ya masomo katika Chuo cha Uongozi na Utawala cha Raila Amolo Odinga kinachoanzishwa chini ya Chuo cha Serikali Kenya (KSG). Chuo hicho, kilichozinduliwa Jumanne na Rais William Ruto wakati wa maadhimisho ya miaka 100 ya KSG, kinalenga kuhifadhi na kufundisha falsafa za Raila kuhusu utawala bora, demokrasia, huduma kwa umma na maendeleo ya bara Afrika. Mkurugenzi Mkuu wa KSG, Profesa Nura Mohamed, alisema kundi la kwanza la wanafunzi linatarajiwa kuanza masomo mwezi Septemba. Alisema mtaala wa chuo hicho utajengwa juu ya nguzo tano kuu zilizotawala maisha ya kisiasa ya Raila; umoja wa Afrika, uongozi ushirikishi, utawala bora, elimu na ubunifu, pamoja na amani na haki. “Alipokuwa akiwania urais alikuwa na manifesto mbalimbali, na baadhi yake zitajumuishwa katika masomo ya chuo hiki ili maono yake yaweze kutekelezwa,” alisema. Profesa Mohamed alisema walipol...
Marato tv - Sauti ya Jamii