Skip to main content

Posts

Showing posts from February 7, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Bashungwa Ampokea Rais Yoweri Museveni Dar Es Salaam

 Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Innocent Bashungwa (Mb.) amempokea Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Museveni aliyewasili nchini Tanzania kushiriki Mkutano wa Dharura wa Pamoja wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika Februari 8, 2025. Jumuiya zote mbili zinakutana kujadili kwa lengo la kupatia ufumbuzi hali ya ulinzi na usalama katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Majaliwa Mgeni Rasmi Kilele Cha Wiki Ya Anwani za Makazi

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Februari 08, 2025 ni mgeni rasmi katika maadhimisho ya Kilele cha Wiki ya Anwani za Makazi inayofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete (JKCC). Utekelezaji wa oparesheni ya mfumo wa anwani za makazi nchini umewezesha ukusanyaji wa taarifa milioni 12.3 za anwani za makazi ambazo zimehifadhiwa katika mfumo wa kidijitali unaojulikana kwa jina la National Physical Addressing (NaPA). Mfumo wa anwani za makazi ni daftari la kidijitali la wakazi na makazi kwa ajili ya ambalo linawezesha kuharakisha na kurahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii na kuimarisha masuala ya ulinzi na usalama, kuchochea ukuaji wa uchumi, kuwezesha biashara mtandao na kufanyika kwa ufanisi pamoja na kuimarisha uwezo wa kukabiliana na majanga. kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni *“tambua na tumia anwani za makazi kurahisisha utoaji na upokeaji wa huduma”.*

Tra Mkoa wa Mara yavuka Lengo Kwa Kukusanya Mabilioni Kwa Mwaka 2023-2024

 Na Ada Ouko ;Musoma. MAMLAKA ya mapato mkoa wa Mara imefanikiwa kukusanya shilingi 142.98 bilioni kati ya shilingi 113.51 bilioni iliyolenga kupata kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2023/ 2024. Sababu za kufikia lengo hilo zimetajwa kuwa ni mazingira mazuri ya biashara yaliyowekwa na serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi thabiti wa Raisi Dk Samia Suluhu Hassan na ushirikiano mzuri kutoka kwa wafanyabiashara, sambamba na uboreshaji wa mifumo ya tehama ambao umerahisisha ukusanyaji wa mapato hayo ya serikali. "Kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2023/2024 tulikuwa na lengo la kukusanya kiasi cha shilingi 113.51 bilioni na tulifanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi 142.98 bilioni ambayo ni sawa na ufanisi wa asilimia 126 ya lengo" Hayo yamebainishwa na Meneja wa Mamlaka hiyo mkoani hapa Nasoro Ndemo leo february 7 mwaka huu 2025 kwenye maadhimisho ya siku ya walipa kodi yaliyofanyika katika ukumbi wa MK kata ya Mwisenge Manispaa ya Musoma. Aidha, pamoja na mafanikio hayo Nasoro ame...

Jwtz Kushiriki Mazoezi Mawili Makubwa Kijeshi Kwa Kuhusisha Marekani Na Nchi Nyingine Kumi na Mbili

 

Wasira Awataka Wavuvi Ziwa Victoria Kuvua Kwa Kuheshimu Mipaka ya Nchi

 Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania bara, Stephen Wassira amesema ili kutoingiza taifa kwenye migogoro kutokana na malalamiko ya wavuvi katika ziwa victoria upande wa wilaya ya Rorya mkoani Mara,ameshauri wavuvi kuvua kwa kuzingatia mipaka ya nchi na nchi. Makamu mwenyekiti huyo wa CCM Tanzania bara, ametoa kauli hiyo februari 7,2025 wilayani Rorya, katika mwendelezo wa ziara yake mkoani Mara baada ya kufanya ziara kama hiyo mkoa wa Geita na wilaya nyingine za mkoa wa Mara siku chache tu baada ya kushika wadhifa huo mkubwa katika hicho tawala. Amewashauri wavuvi katika ziwa victoria wilayani humo na wilaya nyingingine kanda ya ziwa wanapofanya shughuli zao za uvuvi katika ziwa hilo, kuchukua tahadhari kwa kuacha kuingia kwenye mipaka ya nchi zingine ili kujiepusha na magogoro inaweza kuvuruga mahusiano na nchi jirani. Wasira ametoa tahadhari hiyo baada ya kutolewa kwa taarifa matukio 12 ya wavuvi kuporwa na kunyang'anywa Mali zao ikisababisha na changamoto ya ...

Balozi Dkt Nchimbi Akutana Na Mzee Joseph Butiku

 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Mzee Joseph Butiku, baada ya Balozi Nchimbi kufika ofisini kwa Mzee Butiku kwa ajili ya kumjulia hali na kutembelea taasisi hiyo inayohusika na kuendeleza urathi wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, hasa katika masuala ya amani, umoja na maendeleo ya watu, leo Ijumaa, tarehe 7 Februari 2025, jijini Dar Es Salaam.

Rais Samia Ashusha Neema Umwagiliaji

-Nirc Yasaini Mikataba Ya Ununuzi Mitambo Ya Kuchimba Visima Virefu Nchi Nzima  *NIRC Dar es Salaam.*  Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji,   imesaini mkataba wa ununuzi wa mitambo ya kuchimba visima virefu na kampuni ya utengenezaji mitambo hiyo ya Uturuki iitwayo Acarkardesler, ambapo mitambo hiyo itagharimu Dola za Kimarekani 2,821,028.  Akizungumza wakati ya utiaji saini wa makubaliano hayo Mkurugenzi Mkuu Tume yaa Taifa ya Umwagiliaji (NIRC), Raymond Mndolwa, amesema mitambo hiyo inatarajia kuwasili nchini ndani ya miezi miwili na kisha kuanza kazi.  Mndolwa amesema lengo la Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan,  ni kuhakikisha sekta ya kilimo cha Umwagiliaji inakua nchini na kuchangia ukuaji wa uchumi na Pato la Taifa.  Pia ametia saini mkataba na kampuni ya Garnite Co. Limited kwa ajili ya ununuzi wa mitambo aina nya Support Trucks, inayotumika kubeba vifaa vya uchimbaji visima, amb...

Wananchi Ntunduwaro wanufaika na Makaa ya Mawe

-      _Wajengewa barabara, Zahanati_ -      _MILCOAL yatoa fursa za ajira_ UZALISHAJI   wa madini ya makaa ya mawe katika kijiji cha Ntunduwaro kata ya Ruanda wilayani Mbinga  ni  chanzo kikubwa cha mapato ya Serikali na  maendeleo  ya wananchi wa kata hiyo. Akizungumza katika mahojiano maalum, Meneja wa mgodi wa Market Insight Limited (MILCOAL),  Atit Mehta amesema kwa mwaka wa fedha 2023/2024 mgodi huo umeweza  kuilipa serikali Shilingi  Bilioni 5.2 kutokana na mrabaha, tozo na ada mbalimbali. Kuhusu Kampuni hiyo kuwajibika kwa jamii inayozunguka mradi kwa maana ya CSR, Mehta amesema wamekuwa wakitekeleza kwa uaminifu  Sera ya Madini inayotambua uwajibikaji wa Kampuni  kwa jamii zinazozunguka miradi na mgodi wao wameweza kujenga barabara ya kutoka Ntunduwaro mpaka Liyumbi yenye urefu wa Kilomita 23. “Kwa sasa tunamalizia mchakato wa mwisho na viongozi wa Serikali akiwemo Mganga Mkuu wa Mkoa (RMO) tuw...