Skip to main content

Posts

Showing posts from January 17, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Steven Wasira amrithi Abdulrahman Kinana Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara

  Mwenyekiti wa Chama Chamapinduzi(CCM)Rais Samia Suluhu Hassan amewasilisha katika Mkutano Mkuu wa CCM Jina la Mwanasiasa Mkongwe nchini Steven Wasira kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Tanzania Bara. Wasira anatarajia kumrithi Abdulrahman Kinana aliyeomba kupumzika nafasi hiyo mwezi Julai Mwaka Jana. Kupitia mkutano huo mkuu maalum wa CCM,Wajumbe 1924 wa mkutano huo wanatarajia kupiga kura za ndio au Hapana ili kupitisha Jina hilo la Wasira.  

Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Samia aongoza kikao cha NEC Mjini Dodoma

  MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 17 Januari 2025, ameongoza Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kilichofanyika Dodoma, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM utakaofanyika tarehe 18 na 19 Januari 2025, jijini Dodoma.

Afisa Madini mkazi mkoani Shinyanga kortini

Na Mwandishi Wetu, Shinyanga. MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoani Shinyanga   imetoa nakala ya wito wa kufika  mahakamani kwa Afisa Madini Mkazi Mkoani hapa Daniel Mapunda ili kutoa ushahidi kuhusiana na shauri la madai namba 9/2023. Madai hayo ni Kati ya Kikundi cha Tushikamane Gold Mine kilichopo Kitalu namba 4 katika Kijiji cha Nyaligungu Kata ya Mwakitoryo Wilaya ya Shinyanga, ambapo wadaiwa ni Kampuni ya Kichina yaTIAMTIN Investment Co LTD na wenzao wanaodaiwa kuwa ni waasi wa Tushikamane Gold Mine Kabla ya maagizo hayo Wakili msomi Paul Kaunda anayewakilisha wadai (Tushikamane Gold Mine) aliiomba mahakama kuwa wakati wa maandalizi ya wito huo ni vema  ukaeleza bayana kuwa anayetakiwa mahakamani ni Afisa Madini Mkazi  mwenyewe Mapunda na si kuwakilishwa na mtu mwingine. Maoni hayo ya wakili yalikuja kutokana na Mapunda kuwakilishwa na mtumishi mwenzake mahakamani hapo siku ya Januari, 15, 2025, Jambo ambalo sio matakwa ya sheria. Aidha katika shauli hilo wakili...

Serikali yasisitiza umuhimu vitabu na machapisho kuhifadhiwa maktaba kuu ya taifa

Na Mwandishi Wetu SERIKALI kupitia Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania (TLSB), imesema itaendelea kuhifadhi machapisho ya vitabu vya ajili ya kukuza maarifa na elimu kupitia vitabu kwa vizazi vya sasa na vijavyo. Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya TLSB, Profesa Rwekaza Mukandala, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wachapishaji na waandishi wa vitabu. Mkutano huo wa siku mbili wa wachapishaji na waandishi wa vitabu uliandaliwa na bodi ya huduma za maktaba Tanzania na kufanyika kwenye ofisi za Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam. Alitaja mada mbili zilizojadiliwa kuwa ni utekelezaji wa sheria ya amana kwenye maktaba mtandao jumuishi ya taifa na umuhimu wa ununuzi wa vitabu kwaajili ya ukuzaji wa soko la ndani. Profesa Mukandala alisema Sheria ya amana ya mwaka 1975 inasisiza umuhimu machapisho yote yanayochapishwa ndani ya nchi kuhifadhiwa kwenye maktaba kuu ya taifa ili kulinda na kuhifadhi urithi wa kitamaduni na kiakili kwaajili ya vizazi vya s...