Skip to main content

Posts

Showing posts from March 21, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Magufuli Alinipigia Simu Saa 8 Usiku Kwamba Haoni Ninachofanya Katika Wizara - Mpina

"Nakumbuka alivyokuwa mfuatiliaji makini wa utekelezaji wa majukumu ya Wizara, nilipokuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira na nilipokuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi simu za usiku na mchana na vikao vingi sana ilikuwa hakuna kulala ni Kazi tu. Nakumbuka siku ameniteua na kuniapisha kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi siku hiyo hiyo usiku saa 8 akanipigia simu akilalamika kwamba haoni ninachofanya katika wizara hiyo. Nilistaajabu sana maana nilikuwa bado hata sijaripoti wizarani na kweli niliamini falsafa yake ya Hapa Kazi tu na kwamba Rais alihitaji kuona mageuzi ya haraka" - Luhaga Mpina "Nilijipanga kufanya kazi za wizara mimi na wenzangu wakati mwingine tulikaa ofisini hadi saa 7 za usiku na baadaye akaanza kutusifia hadharani ikiwemo kutetea msimamo wa kupima samaki kwa rula na kwamba aliamua kutafuta Waziri ambaye atakuwa na kichaa kichaa kama yeye akampata Luhaga Mpina" - Luhaga Mpina Aidha, Mpina amesema wakati Magufuli anafanya zia...

Makamu wa Rais Akiwa Ndani ya Treni ya SGR Kuelekea Morogoro

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akisafiri kwa Treni ya Kisasa ya Umeme ya SGR kutoka Dar es Salaam kuelekea Morogoro leo tarehe 21 Machi 2026. Makamu wa Rais anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Maji, yatakayofanyika mkoani Morogoro, kesho tarehe 22 Machi 2026.

Waziri wa Ulinzi na Jkt Ashiriki Kikao cha 42 cha Mawaziri wa Sekta ya Ulinzi wa Afrika Mashariki

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Mhe.Dkt.Rhimo Nyansaho (Mb), tarehe 20 Machi, 2026 amewhiriki katika kilele Cha mkutano wa 42 wa Mawaziri wa sekta ya Ulinzi wa jumuiya ya Afrika mashariki kilichofanyika jijini Arusha. Mkutano huu muhimu wa kisekta wa ulinzi umefanyika katika makao makuu ya Afrika mashariki jijini Arusha ukiwa ni muendelezo wa jitihada za kikanda wa kuimarisha ulinzi na usalama miongoni mwa Nchi mwanachama. Ushiriki wa Dkt.Rhimo Nyansaho unadhihirisha dhamira ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha Tanzania inatoa mchango mkubwa katika kuchangia amani ya kudumu ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki, jumuiya za kikanda na kimataifa kwa ujumla , huku ikiweka msisitizo na kipaumbele katika ushirikiano wa kijeshi katika kukabiliana na changamoto za kiusalama zinazovuka mipaka.  Serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa Rais Samia Su...