Skip to main content

Posts

Showing posts from April 4, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Serikali kuboresha Reli ya Tazara - Katambi

Katika kuendeleza Ushirikiano kati ya Tanzania,Zambia na China ulioanzishwa na Viongozi wa nchi hizo akiwemo Rais wa Awamu ya Kwanza na Baba wa Taifa,Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,Kenneth David Kaunda wa Zambia na Rais wa Awamu ya kwanza wa Jamhuri ya Watu wa China,Mao Ze Dong,serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imeingia makubaliano na China ili kuweza kujenga na kuiboresha Reli ya TAZARA iliyojengwa  kutoka mwaka  1970 hadi 1975. Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mheshimiwa Patrobas Katambi wakati wa Kumbukumbu ya Kuwakumbuka Wataalamu 65  wa Kichina walioshiriki Ujenzi wa Reli ya TAZARA. Akizungumza katika eneo la makaburi lililopo katika eneo la Gongolamboto Jeshini,jijini Dar es Salaam,Waziri Katambi amesema msingi wa ushirikiano ulioanzishwa na waasisi wa nchi hizo katika Nyanja ya Uchumi,Siasa,Teknolojia na Utamaduni imeendelezwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo watanzania wameshuhudia miradi mbalimbali iliyojen...

Mradi wa umwagiliaji Bugwema wapewa msukumo mpya kukabidhiwa mkandarasi Aprili 18

MRADI Mkubwa wa umwagiliaji katika bonde la Bugwema, wilayani Musoma, katika halmashauri ya Musoma Vijijini mkoani Mara, umeanza kupata uhai mpya baada ya Serikali kuridhia kutolewa kwa shilingi bilioni 48 kwa ajili ya utekelezaji wake. Hatua hii inalenga kuimarisha kilimo cha kisasa na kuinua uchumi wa wananchi wa eneo hilo. Uamuzi huo umefikiwa chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Samia Suluhu Hassan, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali katika kuendeleza sekta ya kilimo na kupunguza umasikini kwa wananchi. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Aprili 4, 2026 na Ofisi ya Mbunge wa Musoma Vijijini, mradi huo unatarajiwa kukabidhiwa rasmi kwa mkandarasi, China Railway Bureau Ltd, Aprili 18, 2026 katika kijiji cha Bugwema, kata ya Bugwema kuanzia saa 4:00 asubuhi. Mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini, Sospeter Muhongo, ametajwa kuwa mstari wa mbele katika kufanikisha kufufuliwa kwa mradi huo, baada ya kuupigania kwa muda mrefu tangu alipochaguliwa. Lengo lake kuu ...

HESLB yavuka malengo ya makusanyo Januari - Machi

Na: Mwandishi Wetu, Dar Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imefanikiwa kuvuka malengo yake ya makusanyo kutoka kwa wanufaika wa mikopo hiyo katika kipindi cha miezi mitatu Januari hadi Machi, 2026, hali inayoongeza fursa ya waombaji wa mikopo hiyo kuongezeka. Kwa mujibu wa taarifa ya HESLB, makusanyo yameongezeka kutoka kwa wanufaika wake, jambo linaloleta faraja kwa taasisi hiyo.  "Miezi mitatu ya Januari hadi Machi, Bodi ililenga kukusanya shilingi bilioni 18.3 kwa kila mwezi, lakini mwezi Januari zimekusanywa shilingi bilioni 20.4, mwezi Februari bilioni 19.4 na mwezi Machi bilioni 20.9," imeeleza taarifa hiyo. Mafanikio ya makusanyo hayo yametokana wa mwamko wa wanufaika wa mikopo ya elimu kuanza kulipa mikopo yao kwa hiari, baada ya kuhitimu na kuwa na vipato kwa kuajiriwa au kujiajiri wenyewe. Vilevile, waajiri kutoa taarifa za wanufaika pindi wanapoanza kazi katika taasisi wanazozisimamia, jambo linaloiwezesha Bodi kuongeza makusanyo yake.  Sanjari na ...