Skip to main content

Posts

Showing posts from July 1, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Simbachawene Achukua Fomu Kutetea Ubunge Wake Jimbo la Kibakwe

 George Simbachawene jana Julai mosi mwaka 2025 alifika katika ofisi za chama hicho zilizopo Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma, kwa ajili ya kuchukua fomu ya Kuomba ridhaa ya kuteuliwa na chama chake kuwania kiti cha Ubunge katika Jimbo la Kibakwe. Akizungumza na Waandishi wa habari Mhe. Simbachawene amesema kuwa bado ana nafasi ya kuendelea kuwatumikia Wananchi wa Kibakwe kwa kuendeleza mafanikio makubwa ya maendeleo yaliyopatikana katika jimbo hilo. ",Bado nina nguvu za kushirikiana na wananchi wenzangu wa Kibakwe kuendeleza mafanikio yetu ya maendeleo tuliyoyapata'alisena Simbachawene  Aidha Simbachawene, amekipongeza Chama cha mapinduzi kwa kuonyesha Demokrasia ya kila Mtu mwenye Sifa kupata nafasi ya Kuwania nafasi mbalimmbali za Uongozi.

Msama Arejesha Fomu ya Kugombea Ubunge Jimbo la Ukonga

Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama leo July 01, 2025 amefika katika Ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam na kurejesha Fomu ya Kugombea Ubunge Jimbo la Ukonga baada ya kuijaza kikamilifu. Fomu hiyo imepokelewa na Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Ilala, Chief Sylvester Yaredi.