Skip to main content

Posts

Showing posts from March 1, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Balozi Nchimbi Ashiriki Mazishi ya Dk. Sam Nujoma Namibia

Picha mbalimbali zikimuonesha Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akishiriki shughuli ya mazishi ya kitaifa ya aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Namibia, Baba wa Taifa hilo na kiongozi wa mapambano ya kupata uhuru wa nchi hiyo, Dkt. Sam Shafiishuna Nujoma, yaliyofanyika katika eneo la makaburi ya mashujaa, jijini Windhoek, na kuhudhuriwa na maelfu ya waombolezaji, kutoka ndani na nje ya Namibia, wakiongozwa na Rais wa Namibia, Nangolo Mbumba, pamoja na viongozi wengine wa Chama na Serikali wa Namibia, tarehe 1 Machi 2025.

Mhe. Rais Samia Azungumzia Uwekezaji wa Bandari Nchini

  Na Mashaka Mhando, Tanga  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amesisitiza umuhimu wa uwekezaji katika bandari za nchi kama njia ya kukuza uchumi, kuongeza ajira, na kuboresha biashara ya kimataifa. Akizungumza kuhusu maendeleo ya sekta ya bandari, Mhe. Rais ameeleza kuwa serikali inaendelea na juhudi za kuboresha miundombinu ya bandari ili kuongeza ufanisi na kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.  Ameeleza kuwa uwekezaji huu utasaidia kuongeza mapato ya taifa kupitia biashara na usafirishaji wa bidhaa. Aidha, Mhe. Rais amesisitiza kuwa serikali inahakikisha kuwa uwekezaji katika bandari unazingatia maslahi ya taifa kwa kuhakikisha kuwa mikataba ya uwekezaji inakuwa yenye manufaa kwa Watanzania wote.  Amebainisha kuwa ushirikiano kati ya sekta binafsi na serikali ni muhimu katika kuleta maendeleo endelevu katika sekta ya uchukuzi na usafirishaji. Serikali inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya upanuzi wa bandari, ikiwemo Band...

Rc Mtambi Aongoza Hafla ya Jeshi La Polisi Utoaji Tuzo Kwa Askari na Wadau Kuhusu Ulinzi na Usalama

  Na Shomari Binda-Musoma MKUU wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi ameongoza hafla ya Polisi Family Day mkoa wa Mara iliyoambatana na utoaji tuzo kwa askari na wadau kwa mchango wao wa ulinzi na usalama. Hafla hiyo imefanyika leo machi mosi kwenye viwanja vya kikosi cha Kuzuia na Kutuliza Ghasia( FFU) mkoani Mara Katika hafla hiyo,Maafisa,Wakaguzi na askari polisi waliofanya vizuri katika kutimiza majukumu yao ya ulinzi na usalama kwa raia na mali zao wamekabidhiwa tuzo na kiasi cha shilingi laki tano. Licha ya tuzo na kiasi hicho cha fedha kwa askari ,wadau mbalimbali walioshirikiana na jeshi hilo mkoani Mara nao wametambuliwa kwa kupewa vyeti vya pongezi. Akizungumza kwenye hafla hiyo,Mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi amewapongeza askari waliofanya vizuri na kuwataka kuendelea kuzingatia maadili na kufuata maelekezo ya kutimiza majukumu. Amesema maadili kwa askari ni jambo muhimu na la msingi kuhakikisha usalama unakuwepo kwenye jamii kuanzia raia na mali zao. Kwa upande w...

Mgendi wa Azam Media Mara Ashinda Ujumbe Wa Tff Mara

 Mwandishi Mwandamizi wa Azam Media Ltd Mkoa wa Mara Augustine Mgendi ameshinda ujumbe wa Mkutano Mkuu TFF kutoka Mkoa wa Mara Mgendi ameshinda nafasi hiyo kwa kupata Kura 5 Kati ya 9  huku moja ikiharibika na hivyo Kula halali kuwa Kura tisa.  Katika uchaguzi huo wa Chama cha Soka Mkoa wa Mara FAM uliofanyika Leo March 1,2025 katika ukumbi wa Mkuu wa mkoa ambapo Mussa Nyamandege aliyekuwa mgombea pekee katika nafasi ya uenyekiti amethibitishwa kuwa Mwenyekiti na wajumbe wa Mkutano huo. Aidha baada ya uchaguzi huo Mwenyekiti mteule wa FAM amemchagua Haroub Salum kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho. Katika nafasi ya ujumbe wa Mkutano Mkuu TFF waliokuwa wakigombea nafasi hiyo ni pamoja na Augustine Mgendi, Revocatus kuboja aliyepata Kura 4 na Mecksedek Mtobesha akipata Kura sifuri

Waziri Mkuu Aongoza Kikao Cha Kitaifa Cha Dira ya Maendeleo 2050

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Kitaifa ya Dira ya Taifa ya Maendeleo  2050,  leo Machi 01, 2025 ameongoza kikao  cha  tano cha Kamati hiyo kwenye ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam. Katika kikao hicho, Mheshimiwa Majaliwa aliimkabidhi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Profesa Kitila Mkumbo, Rasimu ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 ili aipeleke kwenye Baraza la Mawaziri na Bungeni kwa ajili ya kujadiliwıa na kutungiwa sheria.

Rea yaendelea na Usambazaji Wa Mitungi Ya Gesi ya Kilo Sita Kwa Bei ya Ruzuku Mkoani Tanga

  📌Mitungi ya gesi ya 26,040 kusambazwa  📌Kila wilaya kupatiwa mitungi ya gesi 3,255  Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeingia mkataba na mtoa huduma kampuni ya Manjis Logistics Limited  ambaye atahudumia wilaya zilizopo ndani ya Mkoa wa Tanga kwa kuuza kwa bei ya ruzuku mitungi ya gesi ya kilo sita pamoja na vifaa vyake katika maeneo ya vijijini na pembezoni mwa miji. Hayo yamebainishwa Machi 01 , 2025 mkoani Tanga na Msimamizi wa mradi kutoka REA, ndugu Abdulrazack Mkomi wakati wa usimamizi na utekelezaji  wa mradi wa usambazaji mitungi ya gesi ya  kilo sita kwa bei ya ruzuku wilaya ya  Muheza mkoani Tanga.  Mkomi amesema kuwa mitungi ya gesi 26,040 itakayosambazwa mkoani Tanga itachochea kwa kiasi kikubwa matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia.  "Lengo la mradi ni kukuza, kuchochea, kuwezesha na kuboresha upatikanaji wa huduma za nishati safi ya kupikia ili kulinda afya za watanzania, kuboresha uchumi na kutunza mazingira  ...

Askofu "Dao" Kutumia Redio Mpya Musoma Tetemo Fm Kuinua Vipaji vya Sanaa ya Vijana

Na Shomari Binda-Musoma  ASKOFU Mkuu wa Kanisa la New Life Gospel Commonity Church Tanzania( NLGCCT) Daniel Ouma maarufu kama (Askofu Dao) amesema ataitumia redio mpya itakayowashwa Musoma mwishoni mwa mwezi huu wa 3 kuinua vipaji vya sanaa ya vijana. Kauli hiyo ameitoa jana februari 28 wakati akifungua fainali za mashindano ya kusaka vipaji vya sanaa ya vijana ya Musoma Samia Talent Search msimu wa kwanza 2025. Mashindano hayo yaliyodumu kwa wiki 5 yalikuwa yakihusisha kuibua vipaji vya uimbaji,uchekeshaji pamoja na uchezaji. Akizungumza na washiriki walioingia hatua hiyo ya fainali na watazamaji kwenye ukumbi wa Serengeti Resort amesema kupitia sanaa ya vijana hao wanaweza kuikumbusha jamii kumkumbuka Mungu kupitia kile wanachokionyesha jukwaani. Amesema yeye kwa kuwa ni mkurugenzi wa kituo cha redio kinachokwenda kuanzishwa kutakuwa na kipindi cha kuibua na kuendeleza vipaji. Askofu huyo amesema wapo wasanii wenye vipaji vya uimbaji wa nyimbo za dini ambao utumia vipaji vyao kui...

Tume ya Madini yatoa bei mpya madini ya vito

* Kutumika kwa miezi mitatu* TUME ya Madini kupitia Kurugenzi ya Ukaguzi na Biashara ya Madini, imekutana na wadau wa madini ikiwemo Wathaminishaji wa Madini, Wachimbaji Wadogo na Wanunuzi ili kupanga bei elekezi ya madini ya vito. Akizungumza jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Ukaguzi na Biashara ya Madini, Venance Kasiki amesema lengo la kukutana na wadau hao ni kufanya tathmini na kupanga bei mpya ya madini ya vito ambayo itatumika katika kipindi cha miezi mitatu na kuhakikisha biashara ya Vito inakwenda vizuri.  “FEMATA ni mzalishaji wa madini, CHAMMATA  na TAMIDA ni wanunuzi wa madini ya vito, tumekutana ili kutengeneza bei elekezi, ambayo itatumika kwa kipindi cha miezi mitatu, ili pande zote ziweze kunufaika....; “Kikao kimeenda vizuri, bei zilizowekwa ni rafiki, zitanufaisha pande zote kwa maana ya wachimbaji, wanunuzi na serikali itapata stahiki zake ikiwemo Mrabaha na  Ada ya Ukaguzi,”amesema Kasiki na kuongeza  “Bei zilizopendekezwa ni za wazi na zitapatikana kw...