Skip to main content

Posts

Showing posts from February 14, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu Atembelea Ofisi za CCM Mkoa wa Tanga

 Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba ametembelea Ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga kwa lengo la kusalimia Viongozi wa Chama hicho kabla ya kuendelea na ziara zake za kikazi leo tarehe 15 Februari, 2026.

Nyansaho Foundation Yazidi Kunyoosha Mkono Kwa Wahitaji

Na Mwandishi Wetu, Serengeti Shirika la NYANSAHO FOUNDATION limeandika historia mpya katika sekta ya elimu Wilayani Serengeti baada ya kukabidhi zawadi mbalimbali kwa wanafunzi na walimu wa Shule ya Msingi Maganana, Kata ya Nyambureti, kufuatia kufanya vizuri kwa kiwango cha juu katika Mtihani wa Taifa wa Darasa la Nne mwaka 2025 kimkoa. Katika matokeo hayo, shule hiyo ilipata daraja la “A”, hatua iliyoiweka miongoni mwa shule kinara katika mkoa na kuleta fahari kubwa kwa jamii ya Nyambureti na Wilaya ya Serengeti kwa ujumla. Hafla ya utoaji zawadi ilifanyika katika viwanja vya shule hiyo huku ikiambatana na shamrashamra za wanafunzi waliokuwa wakishangilia mafanikio yao.  Baadhi ya Wazazi, viongozi wa kijiji, kamati ya shule na wadau wa elimu walihudhuria kushuhudia tukio hilo lililojaa furaha na matumaini mapya. Akizungumza mbele ya hadhira, mwakilishi wa NYANSAHO FOUNDATION alisema taasisi hiyo inaamini kuwa elimu ndiyo msingi wa maendeleo endelevu, na kwamba kuwazawadia wanafun...

Waziri Mkuu aagiza mkandarasi aliyekula fedha za maji, akamatwe

NA MASHAKA MHANDO, Korogwe WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, amemwagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga (RPC), ACP Almachius Mchunguzi, kumsaka na kumkamata mkandarasi aliyekimbia baada ya kulipwa Shilingi Milioni 934 kwa ajili ya ukarabati wa mradi wa maji katika mji wa Mombo, wilayani Korogwe. Dkt. Mwigulu ametoa agizo hilo Leo February 14 mara baada ya kukagua mradi wa maji wa Miji 28 unaotekelezwa katika wilaya nne za mkoa wa Tanga, ambapo ameeleza kukerwa na mkandarasi huyo aliyepokea fedha za umma na kutoweka bila kutekeleza mradi, huku wananchi wakiendelea kutaabika na ukosefu wa maji. "Ameondoka na fedha wakati wananchi wanapata shida; haya ndiyo mambo yanayokera na kuchukiza. RPC, huyu mtu atafutwe popote alipo, akamatwe na awekwe ndani mpaka arejeshe fedha za umma. Sijateuliwa ili nipendwe, na sitakuwa na huruma na watu wanaohujumu miradi ya Serikali," alisisitiza Waziri Mkuu. Mradi wa Miji 28 Kufikia Asilimia 75 Mapema, Wazi...

Waziri Mchengerwa Afanya Mazungumzo Ya Kuokoa Vifo Vya Mama na Mtoto na Bosi wa Stbf

Na John Mapepele, Addis Abbaba  Waziri wa Afya,  Mheshimiwa Mohamed Omari Mchengelwa, leo  Februari 14, 2026 amekutana na  Makamu wa Rais wa Susan Thompson Buffet Foundation (STBF), Prof Senait Fisseha, jijini Addis Ababa kwenye Mkutano wa pembezoni mwa kilele cha Kongamano la 39 la Umoja wa Afrika na kufanya mazungumzo ya kimkakati katika  kukabiliana na changamoto ya vifo vya mama na mtoto. STBF ni miongoni  mwa wafadhili wakubwa wa Serikali katika uimarishaji wa mifumo ya afya hususani katika kupunguza vifo vitokanavyo uzazi. Aidha,  Mheshimiwa Waziri Mchengerwa akiwa na Katibu Mkuu, Dkt. Seif Shekalaghe amelishukuru STBF kwa msaada wa fedha wa kiasi cha Dola za Marekani milioni 36.8 zilizotolewa kati ya 2021 - 2025 ambazo zimesaidia katika kuimarisha mifumo ya afya na hivyo kuchangia katika kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi, watoto na vijana.  Mheshimiwa Mchengerwa alichukuwa fursa hii kumuomba Prof. Sinait kuangalia mpango wa Tanzania wenye...

Dkt. Mwigulu Akagua Mradi wa Maji Korogwe

_Asema ni mradi unaoipa hadhi nchi, unaojali utu_ WAZIRI MKUU Dkt Mwigulu Nchemba amekagua Mradi wa Maji wa Miji 28 unaoendelea kujengwa wilayani Korogwe mkoani Tanga kwa thamani ya sh. bilioni 171. Akizungumza na viongozi na wananchi waliofika kwenye eneo la tukio katika kijiji cha Mswaha Darajani, kata ya Mswaha leo jioni (Jumamosi, Februari 14, 2026), Waziri Mkuu amesema ameridhishwa na utekelezaji wa mradi huo na akasisitiza kuwa wananchi wanaoishi Mswaha ambalo ni jirani kabisa na eneo la mradi, wapewe kipaumbele cha kupata maji pindi utakapokamilka.  Waziri Mkuu ambaye yuko mkoani Tanga kwa ziara ya kikazi ya siku tano, amesema kuwa uwekezaji mkubwa umefanyika maeneo yote nchini kwa dhamiria ya kumaliza changamoto ya huduma ya maji kwa Watanzania wote. “Leo tunakuja kuuona mradi ambao hata kwa kuungalia tu unafurahisha, ni mradi wenye hadhi ya kiongozi anayejali mambo ya maendeleo. Mheshimiwa Rais Dkt. Samia ameweka fedha hapa ili zisaidie wananchi wa Muheza, Handeni, Korogwe...

Dkt. Mwigulu Akagua Mradi wa Maji Kwamaligwa.

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Februari 14, 2026 amekagua mradi wa maji wa Kwamaligwa uliopo wilaya ya Kilindi Mkoani Tanga ambao utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 6.98 hadi kukamilika kwake. Mradi huo unaotekelezwa kwa fedha za Mfuko wa Maji chini ya usimamizi wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) unatoka kwenye  bwawa lenye uwezo wa kuhifadhi maji kiasi cha lita 670,902,360 kwa mwaka. Mradi huo unatarajiwa kuhudumia jumla ya wananchi 36,263, wakiwemo wananchi 32,641 wa Kata ya Kibirashi (vijiji sita) na wananchi 3,622 wa Kata ya Kisangasa, Kijiji cha Kwediswati. Mpaka sasa Mkandarasi amelipwa jumla ya shilingi bilioni 4.61 kwa kazi alizotekeleza.

Wazuri mkuu aagiza waliosababisha mifuko ya saruji kuganda kuchukuliwa hatua

NA MASHAKA MHANDO, Handeni WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, amemwagiza Katibu Mkuu Wizara ya elimu, sayansi na teklonojia, kuwachukulia hatua watumishi wa Wizara hiyo waliosimamia ujenzi wa Chuo Cha Veta wilayani hapa na kusababisha mifuko 1,262 ya saruji kuganda. Sambamba na agizo hilo Waziri Mkuu pia amemwagiza Kamanda wa Takukuru  mkoani Tanga, kwenda kufanya uchunguzi wa matumizi mabaya ya fedha katika jengo la kituo cha afya Sindeni ambako milango 34 ipo chini baada ya mkandarasi kuweka milango hiyo kwa kiwango cha chini. Akizungumza jana jioni katika ziara yake ya siku ya kwanza mkoani hapa, Waziri Mkuu amemwagiza Mkuu wa mkoa kufuatilia la matumizi mabaya ya fedha kwenye miradi hiyo ambayo. Alisema wilayani Handeni kuna miradi imekuwa na kasoro ambapo jengo la mama na mtoto katika kituo cha afya Sindeni milango ipo chini ya kiwango kutokana na watu kufanya kazi kwa mazoea. "Kamanda wa Takukuru wote waliohusika wachukuliwe hatua za k...