Skip to main content

Posts

Showing posts from July 3, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

WAZIRI MKUU AZINDUA SHULE YA MSINGI KASOMA, AIPONGEZA MUSOMA VIJIJINI KWA USIMAMIZI WA MIRADI

 Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba ameizindua Shule ya Msingi Kasoma iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, mkoani Mara na kuipongeza halmashauri hiyo kwa kusimamia miradi ya maendeleo kwa kuzingatia thamani ya fedha pamoja na kuendelea kuboresha huduma za elimu kwa wananchi. Akizungumza baada ya kuzindua shule hiyo leo (Jumamosi, Julai 4, 2026), Dkt. Mwigulu alisema Serikali itaendelea kuwekeza katika sekta ya elimu ili kuhakikisha watoto wengi zaidi wanapata fursa ya kusoma katika mazingira bora na karibu na makazi yao. "Nimeona usimamizi mzuri wa miradi unaozingatia thamani ya fedha. Hicho ndicho ambacho Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekikusudia kiwafikie wananchi. Hongereni sana," alisema Dkt. Mwigulu. Waziri Mkuu alisema Halmashauri ya Wilaya ya Musoma imeanza mapema kutekeleza mwelekeo wa Serikali wa kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na shule ya sekondari, hatua ambayo itawezesha utekelezaji wa sera ya elimu ya lazima kwa miaka 10 kuanzia shule ya msingi ha...

MISSAMA: HAKUNA HAKI BILA WAJIBU, WATUMISHI FANYENI KAZI KWA BIDII

 MISUNGWI, MWANZA  Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza wamehimizwa kuchangamkia fursa zilizopo katika sekta za kilimo na mifugo kwa kuanzisha shughuli za uzalishaji zitakazowaongezea kipato, kuimarisha uchumi wa familia na kuwaandaa kwa maisha bora baada ya kustaafu. Wito huo ulitolewa katika kikao cha kawaida cha watumishi kilichoongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Bw. Addo Missama, mwishoni mwa wiki, wakati wa kujadili utekelezaji wa mipango ya mwaka wa fedha 2026/2027 ulioanza Julai 1, 2026. Akichangia mjadala huo, Afisa Mifugo wa Halmashauri, Philimon Katabazi, aliwataka watumishi kutumia fursa mbalimbali za mikopo kuwekeza katika ufugaji na kilimo cha kisasa ili kuongeza kipato chao. "Watumishi tusisubiri muda wa kustaafu ndipo tuanze kufikiria chanzo kingine cha kipato. Tumejaliwa wataalamu wa kilimo na mifugo ndani ya halmashauri; watumieni kupata ushauri wa kitaalamu na anzeni kuwekeza mapema," alisema Katabazi. Alisema hatua h...

RAIS SAMIA KALETA BILIONI 1.2 ZA UJENZI WA SHULE ZA MSINGI MLIMBA- PROF. SHEMDOE

 •Akagua miradi ya maendeleo, ahimiza ikamilike kwa wakati Na OWM - TAMISEMI, Mlimba Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe amesema Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu, amewaletea wananchi wa Mlimba kiasi cha Shilingi Bilioni 1.2 za kitanzania kwa ajili ya ujenzi wa shule mbili za msingi zitakazoongeza fursa za elimu na kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji. Prof. Shemdoe amesema hayo Julai 3, 2026 katika Uwanja wa Tandare, Kata ya Igima, wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi hao, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuhimiza uwajibikaji wa watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba. "Leo nimekuja na habari njema kutoka kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewaletea Shilingi  Bilioni 1.2 kwa ajili ya ujenzi wa Shule za Msingi Mgeta na Nganyangira. Nimejiridhisha kuwa fedha hizo tayari zimeingizwa kwenye akaunti ya halmashauri ili ...

RAIS SAMIA ASEMA MAONESHO YA SABASABA NI KIELELEZO CHA TANZANIA KUWA LANGO LA BIASHARA AFRIKA MASHARIKI

 Rais Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa maonesho ya Sabasaba ni jukwaa muhimu la biashara na ni ishara muhimu ya uaminifu kwa Tanzania kuwa ni kituo kikuu cha biashara katika lango la Afrika Mashariki. Akizungumza leo Jijini Dar es salaam, katika maadhimisho ya miaka 50 ya maonesho ya Sabasaba, Rais Samia amesema katika kuadhimisha miaka 50 ya maonesho ni hatua muhimu kwa Tanzania katika kufurahia juhudi za wafanyabiashara, ubinifu wa sekta binafsi  pamoja na mchango wa viwanda na nafasi ya Tanzania katika biashara kikanda na kimataifa. Aidha, Rais Samia, amewataka wadau wa biashara na uwekezaji kujikita katika ubunifu ili kuimarisha maendeleo na ushindani katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba). Sambamba na hilo, Rais Samia amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Dkt. Daniel Chapo, kwa kukubali kuwa mgeni rasmi na kufungua maadhimisho hayo ya miaka 50 ya Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam. Aidha, Waziri wa Viwanda na Biashara, Jud...

ZIARA YA WAZIRI MKUU MARA: MATUKIO YALIYOACHA GUMZO MUSOMA

  *Matukio mbalimbali yaliyojiri katika mkutano wa hadhara wa Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, uliofanyika katika Uwanja wa Mara Sekondari, Manispaa ya Musoma, mkoani Mara, leo Julai 3, 2026, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani Mara.*