Skip to main content

Posts

Showing posts from November 11, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais Dkt. Samia amewaongoza Wajumbe wa Tume ya Mipango kusimama kwa dakika moja kutoa heshima kufuatia kifo cha aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Tume hiyo

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwaongoza Wajumbe wa Tume ya Mipango kusimama kwa dakika moja kutoa heshima kufuatia kifo cha aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Ndugu Lawrence Mafuru aliyefariki nchini India Novemba 9, 2024 alipokuwa akipatiwa matibabu, kabla ya kuanza kikao leo tarehe 11 Novemba,2024 Ikulu jijini Dar es Salaam.

Mnec Manguzo amwaga ajira 200

  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Chamapinduzi(CCM)Taifa LEONARD QWIHAYA Maarufu kwa Jina la Manguzo ametangaza ajira Mia mbili za udreva wa Magari Makubwa.  Kwa mujibu wa Tangazo la ajira lilitolewa na Kampuni ya QWIHAYA GENERAL ENTERPRISES COMPANY LTD inayomilikiwa na MNEC huyo,imeeleza kuwa Mchakato wa Maombi ya ajira ni bure na waombaji wasikubali kuhadaiwa na Matapeli. "Nachukua fursa hii kuwatangazia Watanzania wenzangu kuwa, kupitia Kampuni yetu ya Qwihaya tumetangaza fursa za Ajira kwa Maafisa Usafirishaji (Dreva) 200 wa Magari Makubwa ya Mizigo,Kutokana na maombi maalum kwa Wakazi wa Mkoa wa Mwanza tumeweka utaratibu rafiki kwa ambao hawana wadhamini wa serikali  hivyo, wataambatanisha barua tatu za wadhamini wa Chama Cha Mapinduzi ikiwemo uthibitisho wa Balozi wa Shina analotoka, kiongozi wa Chama Cha Mapinduzi ngazi ya Tawi pamoja na Kata"Manguzo ameeleza katika Taarifa yake.  Kwa Mujibu wa Manguzo,Dhamira ya Kampuni yake ya QWIHAYA GENERAL INTEPRISES C...

Tumieni Mapato ya ndani kutekeleza Miradi

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - TAMISEMI chini ya Mwneyekiti wake Mhe. Justin Nyamoga imeelekeza Uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kutekeleza miradi mbalimbali kupitia mapato ya ndani kwani ni miongoni mwa Halmashauri zenye mapato makubwa  nchini. Rai hiyo imetolewa na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Jafari Wambura Chege kwaniaba ya mwenyekiti wa kamati mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa ghorofa sita wa Hospitali ya Mbagala Rangi Tatu Katika kata ya Mbagala kuu. “kamati inaamini kuwa kupitia mapato ya ndani ya Manispaa ya Temeke mnauwezo wa kukamilisha mradi huu kwa kutumia fedha za ndani na mkawa mfano kwa Halmashauri nyingine zenye mapato makubwa nazo zikaweza kupata somo kupitia Temeke” Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Nyamoga hiyo kwa usimamizi mzuri wa miradi mbalimbali ya marndeleo ambayo thamini ya fedha inaonekana katika miradi hiyo. Kamati hiyo ambayo imefanya ziara yake mkoani Dar es salaam kat...

Rais Samia akutana na kufanya Mazungumzo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo  na Katibu  Mkuu wa Jumuiya ya Afrika  Mashariki, Bi. Veronika Mueni Nduva, alipofika Ikulu, Jijini Dar es Salaam leo tarehe 11 Novemba, 2024 ikiwa ni mara ya kwanza kukutana nae tangu Katibu Mkuu huyo aliposhika nafasi hiyo  mwezi Juni, 2024.

Biden na Trump Kukutana Jumatano Wiki hii

 Bideni na Trump watakutana Jumatano Hii na kuzungumza maswala Mbali Mbali kuhusu Nchi na Kuachiana Madaraka kutoka Utawala wa Biden kwenda Trump Ikumbukwe kumekua kuna Shutuma Nyingi Sana kutoka kwa Trump kwenda kwa Utawala wa Biden Ambao amekuwa akijaribu kutoa Shutuma na hoja nyingi kwamba Biden Ameshindwa kushughulikia maswala mbali mbali ya kiuchumi na Sera ya Mambo ya Nje pamoja na Uhamiaji ambazo Zimekuwa ni Sera za Msingi kwa Trump ambapo imepelekea Nchi kwenda Mrama Hiki kinachoenda kutokea Kesho kutwa Dunia Nzima itakuwa ina Subiri kwa hamu kubwa kuona ni namna gani Viongozi hawa Wenye Ushindani mkubwa watakavyozungumza Tukumbuke kwamba Trump amekuwa akiweka maoni yake wazi ya kihafidhina na kitaifa zaidi pale ambapo anapozungumzia maswala ya kitaifa Zaidi Kuna Vitu vinawatofautisha Viongozi wa Marekani katika falsafa ,Mitazamo,Sera na Vipaumbele lakini kuna vitu vinawaunganisha ambayo ni maslahi ya Taifa lao kwa Kiasi kikubwa

Waziri Mkuu amesema Baraza la Mawaziri sasa Kufanyika Kwa Kidijitali

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa matumizi ya mfumo wa kielektroniki wa Baraza la Mawaziri utasaidia kuboresha utendaji kazi na kuleta ufanisi zaidi katika kuwahudumia wananchi. Amesema kuwa maboresho hayo ya matumizi ya mfumo wa kielektroniki yatasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza matumizi ya karatasi katika vikao vya Serikali, hususan Baraza la Mawaziri, hivyo kupunguza changamoto ikiwemo kuchelewa kwa taarifa, gharama kubwa za uchapaji na hatari ya upotevu wa taarifa muhimu. Amesema hayo leo (Jumatatu, Novemba 11, 2024) wakati akifunga Mkutano wa Kazi wa Mawaziri na Naibu Mawaziri kuhusu matumizi ya mfumo wa kielektroniki wa Baraza La Mawaziri (e-CABINET), kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma. Ameongeza kuwa hatua hiyo inatokana na jitihada na malengo ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kusisitiza umuhimu wa Mawaziri na watumishi wa umma kuzingatia mabadiliko ya kiteknolojia katika utendaji kazi,  “Matokeo ya mwaka 2023 ya ulinganifu baina ya nchi katika mukt...