*📌Fursa lukuki za kiuchumi zaibuliwa* *📌Wananchi waeleza namna maisha yao yalivyobadilika* Wananchi wa Kijiji cha Mapili Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwawezesha kubadili maisha yao kupitia mradi wa umeme uliotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Wametoa shukrani hizo kwa nyakati tofauti kijijini hapo Agosti 13, 2025 wakati wa kampeni maalum ya uhamasishaji wa matumizi ya umeme kwa ajili ya shughuli za kiuchumi inayotekelezwa na REA katika maeneo mbalimbali kote nchini. “Tunaishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kabla ya kupata nishati hii ya umeme mazingira hayakuwa mazuri, usiku hatukuwa na mwanga sasa hivi tunaishi kwa amani na hata baadhi ya shughuli za kimaendeleo zinafanyika hadi muda wa usiku lakini pia tunapata habari kwa kutazama luninga muda wowote tunaotaka pia baadhi ya vijana wamepata ajira kupitia umeme,” alisema Mwalimu Mstaafu, Mkazi wa Ki...
Marato tv - Sauti ya Jamii