Skip to main content

Posts

Showing posts from November 17, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Naibu Waziri Mkuu akagua Miradi ya Csr Msimbati Mkoani Mtwara

  *📌 Ahoji matumizi ya Shilingi milioni 159 nje ya bajeti Ujenzi wa Kituo cha Afya Msimbati* *📌 Mkurugenzi wa Halmashauri na Wataamu watofautiana Majibu* *📌 Aiagiza TAKUKURU Kufanya Uchunguzi Ujenzi wa Kituo cha Afya*   *Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati* Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo Novemba 17, 2024 amefanya ziara Wilayani Mtwara na kukagua ujenzi wa miradi inayotekelezwa kwa fedha zinazotolewa na wawekezaji mbalimbali kwa ajili ya kuboresha maendeleo kama njia ya kurejesha rasilimali kwa wananchi kupitia (CSR). Akikagua Kiktuo cha Afya Msimbati, Dkt. Biteko ameeleza kutoridhishwa na matumizi ya fedha iliyokuwa imepangwa kutumika katika ujenzi wa kituo hicho na kupelekea ongezeko la kiasi cha shilingi milioni 159. Kituo hicho cha Afya awali kilikadiriwa kujengwa kwa gharama ya shilingi milioni 600 lakini gharama za ujenzi huo ziliongezeka hadi kufikia shilingi milioni 759 na hivyo kuibua maswali ambayo Mkurugenzi wa Hal...

Uokoaji Kariakoo ni Ushuhuda wa Moyo wa Watanzania:Nchimbi

_Apongeza wananchi wa kawaida  kwa kujitokeza haraka kuokoa watu_ _Serikali, vyombo vyake na taasisi binafsi zapewa heko kwa mwitikio wa mfano_ KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amepongeza utayari na mshikamano ulioonyeshwa na Watanzania mara baada ya tukio la kuanguka kwa jengo Kariakoo, akisema kuwa hatua hizo zimeonesha uzalendo na moyo wa udugu uliojengwa ndani ya Taifa letu. Akizungumza leo, tarehe 17 Novemba 2024, alipotembelea eneo la tukio, Balozi Nchimbi alitoa pole kwa familia za waliopoteza maisha na kuwapa faraja waliojeruhiwa, huku akisisitiza umuhimu wa mshikamano katika nyakati za dharura. “Kwa namna ya pekee, napenda kutoa pole zangu za dhati kwa familia za wenzetu waliopoteza maisha. Maisha ya kila Mtanzania yana thamani kubwa. Tunaomba Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi,” alisema Balozi Nchimbi. Aidha, aliwafariji majeruhi akisema:,’Kwa walioumia, walioko hospitali na hata waliotoka, tunawaombea up...