Skip to main content

Posts

Showing posts from July 27, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Ridhiwani Kikwete Azindua Project ya Kuwaandaa Vijana Kiujuzi na Stadi za Maisha Baada ya Kumaliza Masomo

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amezindua PROJECT AMINI iliyo chini ya Bright Africans inayolenga kuwaandaa vijana kwa maisha baada ya masomo kwa kuwajengea stadi za maisha, ujuzi wa ushindani katika soko la ajira na uwezo wa kuleta mageuzi Chanya ya kiuchumi kwa ujumla.  Akizungumza wakati wa uzinduzi huo leo Julai 27, 2025 Mhe. Ridhiwani amesema kuwa serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetekeleza mikakati thabiti ya kuwawezesha vijana kushiriki kimakimilifu katika maendeleo ya Taifa kijamii na kiuchumi Amesema kuwa serikali imetengeneza mazingira bora kwa vijana kwa kuandaa mipango na programu mbalimbali zinazohusu maendeleo ya vijana ikiwemo programu ya Taifa ya kukuza Ujuzi ambayo inasaidia kutoa ujuzi kwa vijana kwa nadharia na vitendo, programu ya Uanagenzi na Mikopo kwa vijana kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana. Aidha Mhe. Ridhiwani amet...

Kamati ya maadili yakesha kukata mzizi wa fitina kwa watia nia ubunge ccm

Kikao cha Kamati ya Maadili ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kikiendelea muda huu majira ya saa nane usiku chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia na kuchuja majina ya wagombea Jijini Dodoma tarehe 28 Julai, 2025.

Waziri Mkuu kumwakilisha Rais Dkt Samia katika mkutano wa ACTIF 2025 nchini Grenada

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa Julai 27, 2025 amewasili mjini St. George’s, nchini Grenada ambapo atamwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Jukwaa la nne wa Kibiashara na Uwekezaji kati ya Afrika na Karibiani (Afri-Caribbean Trade and Investment Forum - ACTIF 2025) unaotarajiwa kufanyika Julai 28–30, 2025 katika kituo cha mikutano cha Radisson. Mkutano huo mkubwa unaolenga kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya mataifa ya Afrika na visiwa vya Karibiani una kaulimbiu inayosema: _“Uhimilivu na Mabadiliko: Kuimarisha Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Afrika na Karibiani katika Kipindi cha Changamoto za Kidunia.”_ Katika mkutano huo, Waziri Mkuu anatarajiwa kushiriki mjadala wa Mjadala wa Wakuu wa Nchi na Serikali, kukutana na viongozi wa mataifa mengine, pamoja na kushiriki katika mikutano ya uwili na wawekezaji wakubwa, ikiwa ni dhamira ya Tanzania ya kuendeleza juhudi zake za kuvutia wawekezaji wa kimataifa ili kusaidia katika kujenga uchumi wa kisasa na shindani duniani. Ushir...

Ccm inatoa Somo Duniani Uimara Wake, Kujibadilisha Kuendana na Wakati

_Kudijitilize Chama, kurekebisha Katiba kuendana na mahitaji ya sasa._ Na Bwanku M Bwanku. Moja ya sifa kubwa inayoweza kuifanya taasisi yoyote duniani kuendelea kuishi, kuwa imara na kushawishi kundi kubwa la watu basi ni uwezo wake wa kubadilikabadilika kulingana na muda na mahitaji ya wakati uliopo wa watu inaowahudumia. Lazima ubadilike kwenda na muda (dynamic) na sio kung'ang'ania ujima (static). Mtaalamu wa masuala ya taasisi (Organizational Structure) Mjerumani Max Weber aliwahi kusema kwamba taasisi isiyobadilika na inayokumbatia uhafidhina (conservative) inajiandalia kifo chake yenyewe. CCM ni moja ya Chama kikongwe na kikubwa sana sio tu Afrika bali duniani kikishiba utajiri mkubwa wa kihistoria na kitaasisi. Ni Chama cha Pili kwa ukubwa, cha muda mrefu na kikongwe zaidi Barani Afrika baada ya Chama Cha True Whig Cha Liberia kikiwa na miaka 48 toka kiasisiwe Februari 05, 1977 baada ya kuunganika kwa Vyama viwili vya Tanganyika African National Union (TANU) cha Tangany...

Vyama vya siasa vyahakikishiwa uwanja sawa Uchaguzi Mkuu 2025

Na. Mwandishi Wetu  Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imewahakikishia viongozi wa vyama vya siasa kuwa kutakuwa na uwanja sawa kwa vyama vyote wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka huu kwa kuhakikisha kila chama kinafanya mikutano yake kwa mujibu wa ratiba. Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani, Jacobs Mwambegele ameyasema hayo leo tarehe 27 Julai, 2025 wakati akifungua mkutano wa Tume na Viongozi wa Vyama vya Siasa jijini Dodoma. ”Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, inawahakikishia kuwepo kwa uwanja sawa kwa vyama vyote wakati wa kampeni kwa kuhakikisha kila chama kitafanya mikutano yake kwa mujibu wa ratiba itakayokuwa imepitishwa na kamati ya ratiba ngazi ya Taifa inayoratibu ratiba ya kampeni ya wagombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais, kamati ya jimbo inayoratibu ratiba ya wagombea wa ubunge na kamati ya kata inayoratibu ratiba ya wagombe wa udiwani,” amesema Jaji Mwambegele.  Amewasisitiza viongozi hao wa vyama vya siasa kuwasihi wago...