Skip to main content

Posts

Showing posts from July 22, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dhehebu Potofu Laibuka Kilifi Nchini Kenya

POLISI katika Kaunti ya Kilifi Nchini Kenya wanachunguza iwapo kundi la imani potovu lililonaswa mwanzoni mwa Wiki katika eneo la Binzaro, lina uhusiano na dhehebu la Shakahola ambalo lilisababisha vifo vya zaidi ya watu 400. Boma ambalo mwanamume alipatikana amefariki na watu wengine wanne wakiwa katika hali dhaifu Jumatatu, liko karibu kilomita saba kutoka barabara kuu ya Malindi–Sala Gate. Ndani ya boma hilo kuna nyumba tatu zilizojengwa kwa udongo na paa za mabati lakini hazina madirisha yoyote.  Kuna bwawa la maji ambalo halijakamilika kujengwa, banda la kuku, na eneo la kupikia nje. Mahali hapo hakuna vitanda, jambo ambalo linaashiria kuwa wakazi walilala sakafuni.  Choo kinachoonekana kama banda dogo kilichofichwa katika vichaka karibu na lango kuu, kuashiria mazingira magumu kwa wakazi. Sehemu mbalimbali za ardhi zilikuwa zimevurugwa na hivyo kuibua hofu ya kuwepo kwa makaburi, jambo ambalo maafisa wa polisi sasa wanajaribu kuthibitisha. Wapelelezi walimkamata mshukiwa...

Mahakama yaamuru Kukatwa Pensheni ya Mzee aliyegoma kutoa pesa za Malezi

 MZEE Mmoja Mstaafu amejipata pabaya baada ya Mahakama Kuu  Nchini Kenya kukataa kusitisha utekelezaji wa amri inayomtaka kugawana pensheni yake ya uzeeni na mpenzi wake wa zamani ili kugharamia mahitaji ya watoto wao. Mahakama hiyo pia iliunga mkono uamuzi wa hakimu wa mahakama ya watoto uliomwelekeza mwajiri wa zamani wa mstaafu huyo kulipa deni la matunzo ya watoto linalofikia Sh178,790 kutoka kwa pensheni yake. Mzee huyo, aliyejulikana kwa kifupi kama Bw MST, aliacha kulipa matunzo mwaka jana baada ya kuugua maradhi ya mfumo wa neva ambayo, kulingana naye, yanahitaji matibabu ya gharama kubwa. Alisema aliomba mkopo kufadhili matibabu hayo. Mbali na deni hilo, mahakama ya watoto pia iliagiza mwajiri wake wa zamani kuachilia thuluthi moja ya pensheni yake kwa mpenzi wake wa zamani, Bi LNK, ili kufadhili masomo ya watoto. Bw MST alikuwa ameomba Mahakama Kuu isimamishe utekelezaji wa amri hiyo akidai hakimu hakuzingatia kuwa wazazi wote wawili wana jukumu la kushiriki katika m...

Mkenya Stephen Munyakho aliyeepuka kunyongwa Saudia kurejea Kenya

STEVEN Bertrand Munyakho, Mkenya ambaye alikuwa akikabiliwa na hukumu ya kifo nchini Saudi Arabia, sasa ameachiliwa rasmi kutoka kizuizini. Munyakho, kwa jina maarufu la Stevo, mwana wa kwanza wa mwandishi mkongwe Dorothy Kweyu, aliachiwa huru Jumanne saa nne asubuhi, kwa mujibu wa Katibu wa Wizara ya Masuala ya Kigeni, Korir Sing’oei. Tukio hilo liliashiria mwisho wa zaidi ya muongo mmoja gerezani. “Steve Abdukareem Munyakho, raia wa Kenya ambaye alikuwa katika hatari ya kunyongwa katika Ufalme wa Saudi Arabia, sasa ni huru kuanzia saa nne asubuhi leo, kufuatia kutimizwa kwa masharti ya mahakama kikamilifu,” alisema Bw Korir Sing’oei kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter). “Ubalozi wetu mjini Riyadh umethibitisha kuwa Steve alitekeleza ibada ya Umra mara tu baada ya kuachiliwa. Tutatoa taarifa zaidi kuhusu kurejea kwake nchini,” akaongeza, akiwasifu wote waliotoa mchango wao kuhakikisha mafanikio haya. Kwa miaka mingi, hatari ya kunyongwa ilimwandama Munyakho. Kila alfajiri ndani ...

Majaliwa akutana na Waziri Mkuu wa Belarus

*_Washuhudia utiaji saini hati tatu za makubaliano na mkataba mmoja_* WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na Waziri Mkuu wa Belarus, Alexander Turchin na kujadiliana naye masuala ya uwekezaji, biashara, nishati, madini, elimu, afya, teknolojia na kilimo kwenye kikao kilichofanyika leo (Jumanne, Julai 22, 2025) ofisini kwa mwenyeji wake, mtaa wa Sovetskaya, jijini Minsk. Katika mazungumzo hayo, Waziri Mkuu Majaliwa alimweleza mwenyeji wake kuwa, mbali na kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia anataraji kuwa ziara hiyo itaongeza chachu ya nchi hiyo kushirikiana na Tanzania kwenye masuala mbalimbali ikiwemo uwekezaji, elimu, afya na upatikanaji wa zana za kisasa kwenye kilimo kutokana na fursa mbalimbali zilizoko nchini. Alisema mazungumzo yao yamefungua milango ya kuimarisha uwekezaji, fursa za biashara na masomo katika vyuo vya elimu ya juu, na kwamba wamekubaliana na mwenyeji wake kuwa Mawaziri wake na Naibu Makatibu Wakuu walioko kwenye ziara hiyo wakutane ili kuanza majadiliano rasm...

Waziri Mavunde Akagua Ujenzi wa Jengo la Ghorofa Nane la Mafunzo ya Uongezaji Thamani Madini Vito

▪️Bilioni 33 kukutumika kukamilisha Jengo la ghorofa pacha-TGC Arusha ▪️Biashara ya madini kufanyika kwenye Jengo ▪️Ni mkakati wa uongezaji thamani madini ya vito ▪️Wachimbaji Arusha wamshukuru Rais Samia kwa miundombinu ya jengo Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, leo Julai 22, 2025 ametembelea eneo la ujenzi wa jengo la kisasa la ghorofa nane la Kituo cha Jeomolojia Tanzania (TGC), linaloendelea kujengwa jijini Arusha, kwa lengo la kukagua maendeleo ya mradi huo muhimu kwa Sekta ya Madini nchini. Katika ziara hiyo, Waziri Mavunde amepata fursa ya kujionea hatua mbalimbali za ujenzi na kupokea taarifa ya maendeleo kutoka kwa Mhandisi Julian Mosha wa Kampuni ya Skywards Lumocons Joint Venture pamoja na msimamizi wa mradi Jumanne Nshimba kutoka TGC ambapo baada ya kukamilika kwake unatarajiwa kuwa kitovu cha huduma za utambuzi wa madini, tafiti na mafunzo kuhusu vito vya thamani na madini mengine nchini, na hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi kupitia mnyororo wa thamani wa Sekta ya Mad...

Waziri Mkuu atembelea kiwanda cha dawa na zana za kilimo nchini Belarus

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa, leo tarehe 22 Julai 2025, ameendelea na ziara yake rasmi nchini Belarus kwa kutembelea maeneo muhimu ya uzalishaji na ushirikiano wa kimkakati.  Akiwa katika mji wa Minsk, Mheshimiwa Majaliwa alitembelea kiwanda cha Belmedpreparaty, ambacho ni maarufu kwa utengenezaji wa dawa za binadamu. Aidha, Waziri Mkuu pia alitembelea kiwanda cha Minsk Tractor Plant, ambacho kinajihusisha na utengenezaji wa matrekta na mitambo ya kisasa ya zana za kilimo. Ujumbe wa Tanzania ulijionea teknolojia ya hali ya juu inayotumika katika uzalishaji wa vifaa hivyo. Wakati wa ziara hiyo, pamoja na viongozi wengine, Waziri Mkuu aliambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Cosato Chumi. Mheshimiwa Majaliwa pia aliweka shada la maua katika mnara wa mashujaa wa Jamhuri ya Beralus. Kwa ujumla, ziara hiyo ni sehemu ya jitihada za Serikali ya Tanzania kuimarisha mahusiano ya kimataifa kwa manufaa ya wananchi, hasa katika sekta muhimu za m...

Polisi yakamata shehena ya mirungi, wamiliki wajitosa baharini

Na Mwandishi Wetu, Tanga JESHI la polisi mkoani Tanga, limefanikiwa kukamata shehena ya mirungi usiku wa kuamkia jana iliyokuwa ikisafirishwa na boti na watuhumiwa kujitosa baharini kabla ya kukamatwa.  Boti hiyo aina ya fibre yenye rangi nyeupe ilikuwa Ikitokea nchi jirani ya Kenya na ilikuwa na watu wawili ambao kabla ya kutia nanga kwenye ufukwe wa kijiji cha Kwale kilichopo wilayani Mkinga, walijitosa majini kukwepa kukamatwa. Akizungumza ofisini wake Leo Julai 22 Kamanda wa polisi mkoani Tanga Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Almachius Mchunguzi alisema tukio hilo limetokea  alifajiri ya kuamkia leo katika kijiji hicho ambacho kipo mpakani na Jiji la Tanga eneo la Mawe mawili.  Alisema boti hiyo iliyokamatwa na askari wa kikosi cha wanamaji baada ya kupata taarifa kwamba kuna watu watapitisha mirungi kupitia bahari ya Hindi kuyaingiza Jiji Tanga. "Tulipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema kwamba kuna watu na tumia boti kuingiza mirungi katika Jiji la Tanga, tulifu...

Dkt. Biteko Ahani Msiba wa Mzee Mganga Ngeleja

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ahani msiba wa Baba Mzazi wa William Ngeleja, Mzee Mganga Ngeleja aliyefariki Julai 16, 2025 na kuzikwa jana (Julai 21, 2025) Kijijini kwake Bitoto, wilayani Sengerema, mkoani Mwanza.