Skip to main content

Posts

Showing posts from September 11, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Serikali Yasajili Miradi ya Dola Bilioni 8.65 Ndani ya Mwaka Mmoja-Majaliwa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ndani ya mwaka mmoja, Serikali imefanikiwa kusajili miradi 9,678 yenye thamani ya dola za Marekani milioni 8,658 hali ambayo inaonesha matokeo chanya ya uwekezaji nchini. Miradi 9,678 yenye thamani ya dola za Marekani milioni 8,658 ilisajiliwa mwaka 2023 ikilinganishwa na miradi 8,401 yenye thamani ya dola za Marekani milioni 5,558.47 iliyosajiliwa mwaka 2022, amesema.  Alitoa kauli hiyo jana usiku (Jumatano, Septemba 11, 2024) wakati akizungumza na wadau mbalimbali walioshiriki hafla ya uzinduzi wa Taarifa tano za Maboresho ya Mazingira ya Biashara na Uwekezaji na Nyenzo za Usimamizi wa Uwekezaji nchini iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.  Akifafanua kuhusu taarifa ya kwanza ya uwekezaji ya mwaka 2023 ambayo inaonesha takwimu za matokeo chanya ya uwekezaji nchini, Waziri Mkuu alisema miradi hiyo imeweza kuzalisha ajira za moja kwa moja 195,803 ikilinganishwa na ajira 76,841 zilizozalishwa mwaka 2022.  Akie...

WAZIRI MAVUNDE ASEMA VITA DHIDI YA WATOROSHAJI MADINI NI YA KUFA NA KUPONA.

●Watuhumiwa watatu wakamatwa_ ●Waziri Mavunde asisitiza kufuta leseni zao za kufanya biashara ya madini ●Atoa rai kwa wadau kuzingatia sheria na taratibu *Dar es Salaam* Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde ametangaza kukamatwa kwa madini ya dhahabu kilo 15.78 bandarini yalipokuwa yakitoroshwa. Waziri Mavunde amesema hayo leo tarehe 11 Septemba, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na vyombo vya habari. "Nchi yetu inazo sekta kadhaa za uzalishaji ambazo mapato yake ndiyo msingi wa maendeleo ya uchumi wetu ikiwemo sekta ya madini. Sasa basi, tunapokuwa na watu wachache ambao wanajihusisha na vitendo vya utoroshaji wa madini kuikosesha Serikali mapato hatuwezi kuwavumilia" amesema Mavunde "Kilo hizo 15.78 kwa bei ya leo zina thamani ya takribani *bilioni 3.4* fedha ambazo kwa sasa zote watoroshaji hawa wanakwenda kuzipoteza. Serikali tunakwenda kufuta leseni zao wakitiwa hatiani na mahakama na kuwaweka kwenye orodha ambayo hawataruhusiwa kumiliki Leseni ya...

Waziri Mkuu Kuzindua Taarifa za Maboresho ya Mazingira ya Uwekezaji na Biashara

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Septemba 11, 2024 atazindua Taarifa za Maboresho ya Mazingira ya Uwekezaji na Biashara pamoja na  Nyenzo za Usimamizi wa Uwekezaji, katika Ukumbi wa mikutano wa Mlimani City, Jijini Dar es salaam.  Taarifa na nyenzo hizo zitasaidia  katika kuimarisha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini kwa kutoa mwongozo, kuboresha taratibu na kuongeza ufanisi.  Aidha, Nyenzo hizo zitasaidia katika kupima maendeleo, kutatua changamoto na kuhakikisha kwamba uwekezaji unakua katika mazingira rafiki na yenye ushindani. Viongozi wengine wanaoshiriki katika tukio hilo ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Stanslaus Nyongo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila.

Mwenyekiti wa Machifu Mkoa wa Mara Ashauri Vyama Vya Siasa Kujiepusha na Rushwa Wakati wa Uchaguzi

Na Shomari Binda-Musoma MWENYEKITi wa Machifu mkoa wa Mara Chifu Deus Masanja  ametoa ushauri kwa Chama cha Mapinduzi ( CCM ) kujiepusha na Rushwa wakati wa uchaguzi wa ndani wa chama hicho. Kauli hiyo ameitoa leo mbele ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa chama hicho Taifa Fadhil Maganya leo septemba 11 alipopita kuwasalimia machifu hao walipokuwa wakifanya kikao ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mara. Amesema Rushwa inapelekea kupata viongozi wasiofaa na ambao hawatakuwa na moyo wa kuweza kuwatumikia wananchi. Chifu Masanja amesema eneo ambalo wanapaswa kuliangalia ni kuhakikisha wanawake hawakatwi majina yao wanapojitokeza kugombea. Amesema wanawake wameonyesha kusimamia vizuri masuala ya uongozi kama anavyofanya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan hivyo wanastahili kupewa nafasi. Kiongozi huyo wa machifu mkoa wa Mara amesema Rushwa isiwe kikwazo kwa wanawake kupata nafasi za uongozi pale wanapojitokeza kuomba nafasi. " Nashukuru Mwenyekiti wa Wazazi kuja kutusalimia na kwa niaba ya machifu w...

Sekta ya Uvuvi Inaingiza Mapato ya Shilingi Trilioni 2.94 Kwa Mwaka

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema sekta ya uvuvi inaingiza mapato ya sh. trilioni 2.94 kwa mwaka na imekuwa ikikua kwa wastani wa asilimia 1.9 kwa mwaka. “Wastani wa uzalishaji wa samaki kwa mwaka hapa nchini unafikia tani 472,579, huku tani 429,168 sawa na asilimia 91 zikitokana na uvuvi wa kawaida wa kutumia vyanzo vya asili ndani ya bahari, mito na maziwa na tani 43,411 sawa na asilimia tisa zikitokana na ufugaji wa samaki.” Ameyasema hayo leo (Jumatano, Septemba 11, 2024) wakati akifungua Mkutano wa Nane wa Mawaziri wa Umoja wa Nchi za Afrika, Caribbean na Pasifiki (OACPS) wanaohusika na masuala ya Uvuvi, Bahari, Maziwa na Mito ulioanza leo kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.  Akizungumza kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu amesema kila siku watu 230,000 wanajishughulisha na uvuvi mdogo na Watanzania takriban milioni sita wamepata ajira zisizo za moja kwa moja kwenye sekta hiyo. “Uvuvi mdogo mdogo unachangia zaidi ya asilimia 95 ya mavu...

Waziri Mkuu Amuwakilisha Rais Dkt. Samia Mkutano wa Nane wa OACPS

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Septemba 11, 2024 amemuwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Nane wa Mawaziri wa Umoja wa Nchi za Afrika, Karibian na Pasifiki (OACPS) wanaohusika na masuala ya Uvuvi, Bahari, Maziwa na Mito, kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Malengo ya mkutano huo ni kuimarisha utekelezaji wa Makubaliano yaliyofikiwa; kuimarisha utekelezaji wa vipaumbele vya kimkakati vya umoja; kubadilishana uzoefu; kuweka mikakati ya pamoja; na kuimarisha ushirikiano na washirika ili kuboresha usimamizi wa bahari, uchumi wa buluu, na maendeleo endelevu ya uvuvi. Aidha, Mkutano huo unatarajiwa kutoa mwongozo wa kimkakati kwenye vikao vya juu vya maamuzi vya Umoja wa Nchi za Afrika, Karibian na Pasifiki ili kuboresha usimamizi wa bahari, uvuvi na ufugaji wa samaki endelevu.