Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Mbunge Jimbo la Mbeya Mjini Mhe.Dkt.Tulia Ackson amekabidhi Bima za Afya Kwa Wananchi takribani 9000. Hafla ya Makabidhiano ya Human hizo zap afya imefanyika katika Uwanja wa Ruanda Nzovwe Jijini Mbeya na kuhuduriwa na viongozi mbalimbali ikiwemo kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa Mbeya Mh.Juma Zuberi Homera, Naibu Meya Mh.Kephafas, madiwani pamoja na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya Jiji la Mbeya. Akizungumza wakati wa kukabidhi Kadi za Bima ya afya kwa Walengwa,Dokta Tulia amesema uamuzi huo umelenga kuwezesha Wananchi kupata matibabu katika Vituo Vya Afya , zahanati na hospital bila kuwepo kwa kikwazo chochote cha fedha.
Marato tv - Sauti ya Jamii