Skip to main content

Posts

Showing posts from June 23, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu Azindua Mitambo ya Uchorongaji Na Vifaa Vya Utafiti Kwa Wachimbaji Wadogo

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo Juni 24, 2025 amezindua mitambo ya uchorongaji na vifaa vya utafiti kwa wachimbaji wadogo kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma. Utoaji wa mitambo hiyo ni utekelezaji wa maono na msukumo wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwawezesha wachimbaji wadogo kutokana na mchango wao katika kuzalisha ajira, kuboresha kipato cha mtu mmoja mmoja na kukuza uchumi wa Taifa.

Ma- Rc Watano Waenda Kufanya Majaribio Kwenye Ubunge

 Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na kuwahamisha watendaji wake, ambapo amewaweka kando wakuu wa mikoa (RC) watano akiwemo Paul Makonda wa Arusha. Mbali na Makonda aliyeachwa, wengine na mikoa yao kwenye mabano ni, Peter Serukamba (Iringa), Thobias Andengenye (Kigoma), Dk Juma Homera (Mbeya) na Daniel Chongolo wa Songwe. Mkeka huo umetolewa Jana Jumatatu, Juni 23, 2025 na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu ikimnukuu Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Moses Kisiluka. Uteuzi huo umefanyika siku nne zimesalia kabla ya dirisha la uchukuaji na urejeshaji fomu ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kufunguliwa saa 2 asubuhi ya Juni 28, 2025. Duru za siasa zinawataja baadhi ya wakuu hao wa mikoa kwenda kuwania ubunge katika majimbo mbalimbali nchini. Mathalani, Makonda anatajwva kujitosa Arusha Mjini, Serukamba inaelezwa anakwenda Kigoma Kaskazini, Dk Homera anakwenda Namtumbo huku Chongolo ikielezwa anajitosa Makambako. Mabadiliko hayo pia yamegusa Wakuu wa wilaya, Wakurugenzi pamoja ...

Majaliwa Azipa Wiki Tano Taasisi za Serikali Kujiunga na Mfumo Unaowezesha Serikali Kuwasiliana

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameziagiza taasisi za Serikali ambazo hazijajiunga na mfumo wa kielektroni utakaowezesha mifumo ya Serikali kuwasiliana (GovESB) kujiunga na mfumo huo ifikapo Julai 30 mwaka huu ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia  katika kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi. Ametoa maagizo hayo leo Jumatatu (Juni 23, 2025) alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika katika viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma. “Taasisi zote za umma ambazo hazijajiunga na mfumo huu mwisho ni Julai 30 mwaka huu, wote muwe mmeshaingia pale GovESB, huu ni msisitizo ambao ulitolewa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia pindi eGA watakapokamilisha kila taasisi ipeleke mfumo wake, idadi ya taasisi zilizounganishwa ni chache, hakuna gharama na hutakiwi kupanga bajeti” Ameongeza kuwa mfumo huo unafaida kubwa katika utumishi wa umma kwani utasaidia kurahisisha utendaji, kutoa taarifa kwa wakati, kuondoa makosa ...

Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini ahimiza ubunifu, weledi kwa watumishi

- _Atembelea Banda la Tume ya Madini Katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma_ *Dodoma, Juni 23, 2025* KATIBU Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo, na Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu na Utawala, Nsajigwa Kabigi, wametembelea banda la Tume ya Madini katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayohitimishwa leo katika viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma. Katika ziara hiyo, viongozi hao wamejionea namna Tume ya Madini inavyoshiriki kikamilifu katika utoaji wa elimu kwa umma kuhusu majukumu yake, huduma mbalimbali zinazotolewa na mafanikio yaliyopatikana katika usimamizi wa rasilimali za madini nchini. Mhandisi Lwamo sambamba na kuwapongeza wataalam waliopo kwenye banda hilo, amewataka kuendelea kutoa huduma kwa weledi, uwazi na  ubunifu kwa kuzingatia mabadiliko ya kidijitali ili kuwawezesha wananchi kupata taarifa kwa haraka na kwa usahihi. Kaulimbiu ya mwaka huu ni: “Himiza Matumizi ya Mifumo ya Kidijitali ili Kuongeza Upatikanaji wa Taarifa na Kuchagiza U...

Majaliwa Amwakilisha Rais Dkt. Samia Kwenye Kilele cha Siku ya Utumishi wa Umma

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Juni 23, 2025 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma.  Katika hafla hiyo, Mheshimiwa Majaliwa atazindua mifumo miwili ambayo ni Mfumo wa kielektroni unaowezesha mifumo ya Serikali kuwasiliana na kubadilishana taarifa, ujulikanao kama _*Government Enterprises Service Bus (GovESB)_* na Mfumo wa pili ni wa *_e-Wekeza_* unaomuwezesha Mtumishi wa Umma kuwekeza katika Mfuko wa Faida (Faida Fund). Siku ya Utumishi wa Umma husherehekewa kila Juni 23 kila mwaka na nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kwa lengo la kutambua mchango wa Watumishi wa Umma katika maendeleo ya nchi zao na Bara la Afrika kwa ujumla. Kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni _“*Himiza Matumizi ya Mifumo ya Kidijiti ili Kuongeza Upatikanaji wa Taarifa na Kuchagiza Uwajibikaji*”