Kijana huyu alizaliwa Julai 4, 1983 huko Mtwara. Akasoma shule ya msingi Shangani iliyopo Mtwara Mjini kuanzia 1992 hadi 1998. Mtihani wa darasa la Saba akashika nafasi ya tatu kiMkoa. Akachaguliwa kujiunga kidato cha kwanza shule ya sekondari ya vipaji maalumu Kibaha, Pwani. Mwaka 2000 akafanikiwa kuingia kumi bora mtihani wa kidato cha pili kwa kanda ya mashariki, akaongoza masomo mawili ikiwemo Hisabati. Mwaka 2002 akahitimu kidato cha Nne kwa kupata alama “A” katika masomo tisa kati ya kumi aliyofanya katika mtihani wa taifa. Baraza la Mitihani “NECTA” likamtangaza Joel kuwa Mwanafunzi bora kitaifa. Akachaguliwa kuendelea sekondari Kibaha, Mchepuo wa PCB. Akahitimu kidato cha sita na kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es salaam kusomea shahada ya Biashara na Uongozi. Baadae akasoma stashahada ya juu ya Diplomasia ya Uchumi (post-graduate in economic diplomacy). Badae akasoma shahada ya uzamili ya maendeleo na uhusiano wa kimataifa (International cooperation and development). Anaju...
Marato tv - Sauti ya Jamii