Skip to main content

Posts

Showing posts from June 24, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

MTUHUMIWA WIZI WA MTOTO MCHANGA AKAMATWA LUSHOTO

 Na Mwanamkuu Mwandoro,Lushoto. Jeshi la polisi mkoani Tanga limemtia mbaroni mtuhumiwa wizi wa mtoto mchanga katika hospitali ya wilaya ya Lushoto aliyefahamika Kwa jina la Habiba Fundi. Akizungumza na waandshi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Tanga Almachius Mchunguzi amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa Juni 21,2026,saa Moja usiku katika kitongoji Cha Gerekaya,Kijiji Cha kwemashai wilayani Lushoto akiwa na mtoto huyo.  Mchunguzi amesema Juni 19,majira ya saa Moja jioni mama mzazi wa mtoto huyo Mwanaidi Nyaki ,mkazi wa Kijiji Cha Kwemakame aliripoti kupotelewa na mtoto wake wa siku Moja. Kamanda mchunguzi amesema uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa mwanamke huyo ambaye hakufahamika Kwa wakati huo alijenga ukaribu na mama mzazi pamoja na ndugu walikuwa wakimuhudumia hospitalini,na baada ya kujenga urafiki na kuaminiwa alitumia fursa hiyo kumchukuwa mtoto huyo mchanga na kumuweka kwenye beseni lenye nguo na kutoweka nae. Aidha kamanda huyo pia aliongeza kuwa aliidanganya f...

MHANDISI SAMAMBA AWATAKA WATENDAJI WA TUME YA MADINI KUIMARISHA USIMAMIZI WA SEKTA YA MADINI*

Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa watakiwa kuharakisha utatuzi wa migogoro na kusimamia matumizi bora ya leseni za madini_ 📍MOROGORO Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba, amewataka watendaji wa Tume ya Madini nchini kuendelea kuimarisha usimamizi wa Sekta ya Madini kupitia usimamizi madhubuti wa leseni za madini, utatuzi wa migogoro kwenye uchimbaji wa madini pamoja na kuongeza ushiriki wa Watanzania katika shughuli za mnyororo wa thamani wa madini ili sekta hiyo iendelee kutoa mchango mkubwa katika Pato la Taifa. Akizungumza katika kikao cha Menejimenti ya Tume ya Madini kilichofanyika mkoani Morogoro, Mhandisi Samamba amesisitiza umuhimu wa Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa kuhakikisha leseni zinazotolewa kwa wachimbaji zinaendelezwa kwa mujibu wa masharti ya leseni hizo, akibainisha kuwa Serikali haitasita kufuta leseni zisizoendelezwa na kuzipatia kwa wawekezaji au waombaji wenye uwezo na dhamira ya kuziendeleza. Aidha, amewataka Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa kushugh...

RAIS DKT. MWINYI: TAASISI ZA KIFEDHA ZA NDANI ZIIMARISHE USHIRIKIANO NA SERIKALI KATIKA MIRADI YA MAENDELEO

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema bado yapo maeneo mengi ya ushirikiano ambayo taasisi za kifedha za ndani zinaweza kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 24 Juni 2026, alipokutana na ujumbe wa Benki ya Absa Tanzania ulioongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo, Ndugu Obeid Laizer, uliofika Ikulu Zanzibar kwa ajili ya kujitambulisha. Amesema Serikali iko tayari kushirikiana na benki za ndani zinazoonesha dhamira ya kuunga mkono juhudi za maendeleo, hususan katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya kiuchumi na ustawi wa jamii katika sekta mbalimbali. Rais Dkt. Mwinyi ameipongeza Benki ya Absa Tanzania kwa utayari wake wa kushirikiana na Serikali na kuchangia maendeleo ya Zanzibar.  Aidha, ameeleza kuwa Serikali imeboresha mifumo ya kugharamia miradi ya maendeleo kwa kupanua vyanzo vya fedha zaidi ya bajeti ya kawaida, h...

JWTZ KUKAMILISHA HOSPITALI YENYE HADHI SAWA NA MUHIMBILI

 Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) liko katika hatua za mwisho za kukamilisha ujenzi wa hospitali yenye hadhi sawa na Hospitali ya Taifa Muhimbili inayojengwa katika eneo la Msalato, jijini Dodoma. Kauli hiyo imetolewa na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Salum Haji Othman mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) wakati kamati hiyo ilipotembelea hospitali hiyo kwa lengo la kujionea maendeleo ya ujenzi wa mradi huo mkubwa wa afya. Luteni Jenerali Othman amesema hospitali hiyo itakuwa na miundombinu ya kisasa pamoja na uwezo wa kutoa huduma za kibingwa na ubingwa bobezi, hatua ambayo itasaidia kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa wanajeshi na wananchi kwa ujumla. Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU),Mheshimiwa  Paschal Inyasi Chinyele, amepongeza maendeleo ya ujenzi wa hospitali hiyo na kueleza kuwa mradi huo ni muhimu kwa kuimarisha hud...