Skip to main content

Posts

Showing posts from January 15, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Kikwete awasilisha Muswada wa Sheria ya Kazi

   Nimewasilisha Muswada wa Sheria ya marekebisho ya sheria za Kazi (The Labour Laws (Amendments) (No. 13) Bill, 2024), Bungeni Dodoma tarehe 14 Januari, 2025. Nimetumia kikao hicho kuwahabarisha wajumbe jitihada zinazofanya na serikali kutatua changamoto zinazowakabiri Watumishi Tanzania wakiwemo wale wanaojifungua watoto NJITI na changamoto za utatuzi wa migogoro ya Ajira Nchini. #KaziInaendelea #KaziNiUtu

Ccm Musoma Mjini yampongeza Rais Dkt.Samia utoaji Fidia Bilioni 3.9 Kwa Wananchi

Na Shomari Binda-Musoma CHAMA cha Mapinduzi( CCM) Wilaya ya Musoma mjini kimempongeza na kumshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kiasi cha biliini 3.9 kwa wananchi wa Musoma. Kiasi hicho cha fedha kimetolewa kwa wananchi wa Kata ya Nyasho na Kamnyonge kwaajili ya kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege wa Musoma. Katibu wa CCM Wilaya ya Musoma mjini Burhani Ruta amesema fedha hizo zitawasaidia wananchi kwenda kupata makazi mengine na kupisha upanuzi wa uwanja. Amesema serikali ya Rais Dkt.Samia ni sikivu na lilikuwa suala la muda na tayari fedha hizo zimefika kwaajili ya wananchi hao. Katibu Burhani amesema wananchi watakaopata fidia hiyo ya kupisha eneo la upanuzi wa uwanja wakatumie fedha hizo kwa malengo mazuri ikiwa ni kupata makazi mapya. Amesema si vyema kuingiza fedha hizo kwenye matumizi yasiyofaa na baadae kuziacha familia zikiangaika. " CCM Wilaya ya Musoma mjini tunamshukuru Rais Dkt.Samia kwa kutoa fidia ya bilioni 3.9 kwa wananchi wa Nyasho na Kamnyonge. ...

Rais Mwinyi awapa ZNZ Heroes zawadi milioni 50

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk,Hussein Ali Mwinyi ameizawadia Timu ya Taifa ya Zanzibar, ZANZIBAR HEROES Shilingi Milioni 50 baada ya kulitwaa Kombe la Mapinduzi 2025 . Akizungumza katika Hafla Maalum ya Chakula cha Mchana aliyoiandaa kwa ajili ya Wachezaji wa Timu hiyo katika Viwanja Vya Ikulu, Rais Dk.Mwinyi ameeeleza kuwa timu hiyo imeiletea Heshima kubwa Zanzibar na Kudhihirisha Kuwa kuna Vipaji vingi vya Soka hapa nchini vinavopaswa Kuendelezwa katika Maeneo mbalimbali.. Aidha Rais Dk.Mwinyi amefahamisha kuwa kwa mafanikio ya Zanzibar Heroes kuna kila sababu kwa Serikali Kuendelea na ujenzi wa Academy za Soka Kila Mkoa kwa lengo la kuviibua Vipaji vya Vijana. Rais Dk.Mwinyi ametangaza Dhamira ya Kuunda Kamati Maalum ya Kitaifa hivi karibuni itakayokuwa na Jukumu la Kumshauri namna bora ya kuuendeleza Mpira wa Miguu hapa nchini. Halikadhalika Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa hatua za Timu za Zanzibar kulibakisha Kombe la Mapinduzi kwa ...

Tume ya Rais Maboresho ya Kodi Yawafikia Wana Mara Kwa Kupokea Maoni yao

  Na Shomari Binda-Musoma TUME ya Rais ya maboresho ya kodi imetua mkoani Mara na kupokea maoni ya wadau wakiwemo wafanyabiashara kwa kufanya nao kikao. Kikao hicho kilichofanyika leo januari 15 kwenye ukumbi wa Mwembeni Complex kikiongozwa na Balozi Maimuna Tarishi. Akizungumza kwenye kikao hicho Balozi Tarishi amewataka wadau wa kodi hapa nchini kushiriki kutoa maoni na mapendekezo ili kuboresha mfumo wa kodi. Amesema wadau wa kodi na wananchi wote kushiriki kutoa maoni kwa njia ya simu, barua Pepe, kujaza dodoso lililopo mtandaoni na tovuti ya Tume hiyo.  Balozi Tarishi amesema mapendekezo yatakayotolewa na wadau yataiwezesha serikali kuwa na mfumo mzuri wa ukusanyaji wa kodi ambao utasaidia katika maendeleo ya nchi. " Jambo hili ni muhimu lililoanzishwa na mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan na tumewafika wana Mara kwaajili ya maoni yenu. " Tumetoa njia mbalimbali za kutoa maoni tuzitumie kufikisha maoni ili lengo la mheshimiwa Rais liweze kufanikiwa",amesema. Kw...

Watanzania Kunufaika na Mashindano ya Chan 2025, Afcon 2027

*📌 Mashindano yameipa heshima Tanzania kimataifa* *📌 Rais Samia kinara wa Michezo nchini* *Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati* Watanzania watanufaika na fursa mbalimbali za kiuchumi na kijamii zitakazopatikana kuelekea katika mashindano wa CHAN 2025 na AFCON 2027. Hayo yamebainishwa leo Januari 15, 2025 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko wakati akifungua Kongamano la Wadau wa Michezo kuelekea CHAN 2025 na AFCON 2027 jijini Dar es Salaam.  "Nchi yetu imepata heshima kubwa kimataifa na hii haiji kwa bahati mbaya imesababishwa na ukuaji wa demokrasia iliyojengwa na Rais Samia kwenye mataifa mbalimbali duniani," amesema Dkt. Biteko. Aidha, Dkt. Biteko amewapongeza wadau wa michezo waliotoa mawazo ya kuanzishwa kwa kongamano hilo ili kutangaziana fursa zitakazotokea wakati wa mashindano hayo.  Ameeleza kuwa, mashindano yatawakutanisha wageni wengi kutoka mataifa mbalimbali na kuna wajibu wa kufanya maandalizi kwa ufanisi mkubwa ili k...

Maandalizi ya Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi Afrika ( Missiion 300 ) yafikia asilimia 95 - Dkt Biteko

  📌 *Watanzania milioni 13.5 kusambaziwa umeme ifikapo 2030 kutoka milioni 5.2 ya sasa* 📌 *Asema Mkutano wa Mission 300 umekuwa kivutio duniani; Taasisi za Kimataifa zaonesha nia ya kushiriki* 📌 *Ataja sababu za mkutano wa M300 kufanyika Tanzania* *Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati* Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa maandalizi ya Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika wenye lengo la kuharakisha upatikanaji umeme kwa Waafrika milioni 300 ifikapo 2030 (Mission 300) utakaofanyika tarehe 27 na 28 Januari jijini Dar es Salaam yamefikia asilimia 95. Dkt. Biteko amesema hayo tarehe 15 Januari 2025 mara baada ya kukagua maandalizi ya Mkutano huo katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam akiwa ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila. mesema Wakuu wa Nchi 54 kutoka Bara la Afrika wanatarajiwa kushiriki pamoja na viongozi wengine ambao ni Mawaziri wa Fedha n...