*Na John Mapepele – WAF**Washington, D.C.* Serikali ya Tanzania imekubaliana na Chama cha Wafanyabiashara cha Marekani (U.S. Chamber of Commerce) mjini Washington, D.C na Serikali ya Marekani kufanya utekelezaji wa kimkakati wa mkataba wa sekta ya afya ulioingiwa hivi karibuni ili kuzinufaisha pande zote mbili,huku wakiifanya Tanzania kuwa muhimili wa uzalishaji na usambazaji dawa na vifaa tiba katika bara la Afrika. Akizungumza katika leo kwenye Mkutano wa Wadau wa Ushirikiano wa Afya kati ya Marekani na Tanzania uliofanyika leo kati ya Serikali ya Tanzania na Chama cha Wafanyabiashara cha Marekani (U.S. Chamber of Commerce) mjini Washington, D.C., na baadaye kufanya kikao viongozi waandamizi Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Waziri wa Afya wa Tanzania, Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa, alifafanua kuwa tayari Tanzania imejipanga vema kuhakikisha mkataba unatekelezwa kikamilifu. Akielezea zaidi kuhusu mazingira rafiki ya uwekezaji kwenye sekta ya dawa amesema Tanzania inafanya k...
Marato tv - Sauti ya Jamii