Skip to main content

Posts

Showing posts from February 9, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Twcc Mara Wapongeza Mfumo Jumuishi wa TRA Kwa Kuokoa Muda Kwa Wafanyabiashara Nchini.

Na Mwandishi wetu Jovina Massano. Katibu wa Chemba ya Wanawake Wafanyabiashara Tanzania TWCC Mkoa Wa Mara Anastazia Maximilian ameipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa kuiboresha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kuweka mfumo bora wa huduma za mapato hapa nchini. Akizungumza mwandishi wetu katibu huyo amesema mpango wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) wa kuja na Mfumo Jumuishi wa Utawala wa Mapato ya Ndani(IDRAS) utawezesha kuokoa muda kwa wafanyabiashara sambamba na kuondoa usumbufu kutoka sehemu moja kwenda nyingine ikiwemo kupunguza ghalama kwa walipa Kodi. "Mfumo huu unamanufaa makubwa kwetu sisi wafanyabiashara kwa kuwa umetuondolea adha ya kutembea na nyaraka wakati wa kuwasilisha ritani na kulipia Mapato hii inatusaidia kuepuka upotevu wa nyaraka lakini pia utatuwezesha kujihudumia mwenyewe kupitia mfumo huo wa IDRAS"amesema Anastazia. Aidha ameipongeza TRA kwa kutambua thamani ya lugha ya Kiswahili kwa kuwezesha kuwa mojawapo ya lugha zinazotumika katika Mfumo wa I...

Waziri Sangu Azindua Sera ya Taifa ya Kinga ya Jamii

Arusha, Februari 9, 2026 Mkutano wa siku mbili wa Wadau wa Sekta ya Kinga ya Jamii, umeanza leo Februari 9, 2026 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano AICC jijini Arusha, ambapo Sera ya Taifa ya Kinga ya Jamii imezinduliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano na uzinduzi wa Sera hiyo, Mhe. Sangu alisema, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, iliahadi kuwa na Sera hii, ambayo lengo lake ni kuhakikisha hakuna Mtanzania anayebaki nyuma anapokumbwa na changamoto kama umaskini, uzee, ulemavu, magonjwa, ukosefu wa ajira, majanga ya asili. Miongoni mwa wadau wakubwa wa Sekta ya Kinga ya Jamii wanaoshiriki katika mkutano huo ni Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF). Akizungumzia mchango wa Mfuko huo katika utekelezaji wa Sera ya Kinga ya Jamii, Mhe. Sangu alisema, PSSSF imeweza kuongeza idadi ya wanachama kutoka 6...

TR meets Jeune Afrique Media Group head to explore Tanzania investment opportunities

By the OTR Reporter Dar es Salaam. The Treasury Registrar, Mr. Nehemiah Mchechu, on Monday, February 9, 2026, held discussions with Mr Frederic Van de Vyver, Head of Anglophone Africa Jeune Afrique Media Group, a leading Pan-African news company headquartered in Paris, France. The talks, held at the Office of the Treasury Registrar in Dar es Salaam, focused on ways to collaborate and highlight the investment opportunities available in Tanzania. Mr Mchechu assured Mr Van de Vyver that Tanzania offers a favourable investment environment and that he would receive strong support. “In the public sector, you will have full cooperation from the Office of the Treasury Registrar, and in the private sector, support will be available through the Tanzania CEO Roundtable (CEOrt),” Mr. Mchechu said. Mr Van de Vyver, for his part, expressed his commitment to strengthening collaboration with Tanzania. “We must find the best ways to work together,” he said, agreeing with the Treasury Registrar that Tan...

Nemc Yakifungia Kiwanda Cha Hoota Mkuranga

Na Mwandishi Wetu BARAZA la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limekifungia kiwanda cha HOOTA kilichoko Mkuranga Mkoa wa Pwani kutokana na kuchafua mazingira na kuhatarisha afya za wakazi wa eneo hilo. Kiwanda hicho cha kurejeleza taka za plastiki kilichoko  Vikindu Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani kilifungwa jana na maofisa wa baraza  hilo waliofika kiwandani hapo na kufanya ukaguzi. Baada ya kufika kiwandani hapo maofisa wa NEMC walifanya ukaguzi na kujiridhisha kuwa kiwanda hicho kimeshindwa kuzingatia sheria ya mazingira kwa kushindwa kutibu majitaka yanayozalishwa. Akizungumza mara baada ya kufunga kiwanda hicho, Meneja wa Utekelezaji wa Sheria wa (NEMC),  Luvilo Mwamila alisema kiwanda hiko kiko kwenye makazi ya watu na kimekuwa kikitiririsha majitaka kwa wananchi na kuhatarisha afya zao. Alisema kwa kawaida kiwanda hicho kinazalisha majitaka ambayo yanatakiwa kutibiwa kabla ya kwenda kwenye makazi ya watu lakini wamekuwa hawafanyi hivyo Alisema mba...

Dkt. Mwigulu Aiagiza Wizara ya Nishati Kuongeza Kasi Usambazaji Gesi Asilia

_▪️Asema gesi asilia ni kichocheo cha maendeleo ya viwanda, usafiri na uzalishaji wa umeme_ WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba ameiagiza Wizara ya Nishati kuongeza kasi ya kupanua mtandao wa usambazaji wa gesi asilia ili kukidhi mahitaji ya Taifa. Amesema kwa kufanya hivyo kutawawezesha wananchi kupata nafuu ya gharama katika uendeshaji wa vyombo vya moto na matumizi mengine ya nishati pamoja na Serikali kupunguza matumizi ya fedha za kigeni kuagiza mafuta. Amesema hayo leo Jumatatu (Februari 09, 2026) alipozindua kituo Mama cha Gesi Asilia Iliyosindikwa (CNG) cha Puma Energies kilichopo Salasala jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa kituo hicho umegarimu takriban shilingi bilioni 13. “Wizara ya Nishati pia endeleeni kuongeza kasi ya utafutaji wa gesi asilia ili iwe nishati ya kawaida ya maisha ya kila siku ya Mtanzania, Watanzania wote jitokezeni kwa wingi kutumia fursa ya uwepo wa gesi asilia iliyoshindiliwa”. Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amesema kuwa uzinduzi wa mradi huo unaakisi utekelezaji w...

Makamu wa Rais Azindua Mpango wa Ushirikiano Kati ya Taasisi za Elimu na Viwanda

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ametoa wito kwa sekta binafsi kushirikiana na Vyuo, kuwekeza katika tafiti hususan za sayansi na teknolojia ili kuinua viwango vya tafiti na ubora wa elimu nchini. Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa uzinduzi wa mpango wa ushirikiano kati ya Taasisi za Elimu na Waajiri, uliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam. Amesema Kupitia Mpango huo, sekta binafsi inaweza kuchangia maendeleo ya elimu kwa kufadhili tafiti na kutoa ufadhili kwa wanafunzi wa fani mbalimbali kulingana na mahitaji ya soko la ajira. Aidha, Makamu wa Rais ametoa wito kwa Taasisi za elimu na Sekta binafsi nchini kuzingatia maendeleo ya kasi ya sayansi na teknolojia duniani katika utekelezaji wa Mpango huo. Amesema Vyuo na Sekta binafsi vishirikiane kubaini ujuzi muhimu unaohitajika sasa na siku zijazo hususan katika fani za sayansi, teknolojia, ubunifu, tiba, uhandisi na hesabu i...

Serikali Yalipa Asilimia 95 Ya Deni la Kihistoria Mifuko ya Hifadhi, Waziri Sangu Aipongeza Awamu ya Sita

Na OWM-KAM,Arusha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Mheshimiwa Deus Clement Sangu, ametoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Awamu ya Sita kwa utaratibu wake wa kishujaa wa kulipa deni la kihistoria la shilingi trilioni 4 nukta 46 lililokuwa linaikabili mifuko ya hifadhi ya jamii nchini.  Akizungumza jijini Arusha wakati wa uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Kinga ya Jamii ya Mwaka 2023, Waziri Sangu amebainisha kuwa hadi sasa Serikali imefanikiwa kulipa asilimia 95 ya deni hilo ambalo lilirithiwa kutoka kipindi cha kabla ya mwaka 1999, hatua ambayo imesaidia kuimarisha ukwasi na ufanisi wa mifuko hiyo katika kuwahudumia wanachama. Mheshimiwa Sangu ameeleza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya safari ndefu ya maboresho ya Sekta ya Kinga ya Jamii yaliyoanza mwaka 2018 kwa lengo la kutekeleza Ibara ya 11 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayoiagiza mamlaka kuweka taratibu za kusaidia wananchi wakati wa uzee, maradhi na ulemavu. Waziri amesisitiza kuwa kuli...