Waziri wa Ulinzi na Jkt Akutana na Kufanya Mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Rhimo Nyansaho (Mb) tarehe 09 April, 2026, amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mheshimiwa Guy Kabombo Muadiamvita aliyefanya ziara ya kikazi nchini Tanzania. Mazungumzo hayo ya Kikazi baina ya Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yalifanyika katika Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa, Kikombo jijini Dodoma, yalilenga kuimarisha ushirikiano na uhusiano wa muda mrefu na kihistoria baina ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika Diplomasia ya Ulinzi. Katika kikao hicho, Waziri wa Ulinzi na JKT, Dkt Rhimo Nyansaho amemhakikishia Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kongo,utayari wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Ulinzi na JKT, kushi...