WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Rhimo Nyansaho, amesema ujenzi wa Kituo cha Pamoja cha Forodha Manyovu, kilichopo Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, ni hatua muhimu katika kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya Serikali, kurahisisha huduma za forodha pamoja na kuongeza ufanisi katika usimamizi wa shughuli za mpakani. Dkt. Nyansaho ameyasema hayo wakati wa ziara yake mkoani Kigoma, ambapo amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo ya kimkakati, ikiwemo Kituo cha Pamoja cha Forodha Manyovu na ujenzi wa Barabara ya Kabingo–Kasulu Manyovu. Amesema kukamilika kwa kituo hicho kutakuwa na manufaa makubwa kwa Serikali na wananchi kwa kuwa kitaweka pamoja huduma mbalimbali zinazohusiana na shughuli za forodha, hivyo kupunguza usumbufu na kurahisisha utoaji wa huduma kwa watu wanaotumia mpaka huo. Waziri Nyansaho, amesema uwepo wa kituo hicho unatarajiwa pia kuongeza ufanisi katika udhibiti wa shughuli zinazofanyika mpakani, sambamba na kuhakikisha Serikali inapata mapato yanay...
Marato tv - Sauti ya Jamii