Na mwandishi wetu Jovina Massano. Chemba ya Taifa ya Biashara (TNCC) ambayo hapo awali ilifahamika kama TCCIA kuunganisha mifumo yake na Serikali ili iweze kusomana na kubadilishana taarifa kwa ufanisi hapa nchini. Hatua hiyo inalenga kupunguza urasimu katika utoaji wa huduma na kuimarisha mazingira ya Biashara kupitia maboresho ya teknolojia hiyo. Katika kuhakikisha mageuzi hayo yanafanikiwa kwa kiasi kikubwa, Chemba ya Taifa ya Biashara(TNCC) imezindua mafunzo ya wiki moja mkoani Mbeya yanayohusu matumizi ya mfumo mpya wa utoaji wa Vyeti vya Uasili (Certificate of Origin) kupitia Tanzania Chamber Portal (TCP). Mafunzo hayo yanahusisha mikoa 14 ikiwemo Ruvuma, Morogoro na Dodoma, yakilenga kuwajengea uwezo viongozi wa TNCC pamoja na wafanyabiashara ili waweze kutumia mfumo huo kwa ufanisi. Mfumo huo utaongeza uwazi, kupunguza urasimu na kuharakisha utoaji wa huduma kwa wafanyabiashara, huku ukiunganisha moja kwa moja mifumo ya TNCC na Serikali kwa ufanisi zaidi. Akiongea ka...
Marato tv - Sauti ya Jamii