Angela Sebastian ;Bukoba Viongozi wa sekta mbalimbali za Serikali,dini na watoa huduma za Afya mkoani Kagera wamejengewa uelewa juu ya utekelezaji wa sheria ya mfuko wa bima ya Afya kwa wote, ikiwa ni kuanza kutekelezaji wa ahadi ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ya siku 100 aliyoitoa wakati wa kampeini za uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu. Mafunzo hayo yametolewa leo katika ukumbi wa mkuu wa mkoa wa kagera ambapo wamesisitizwa kutoea elimu juu ya sheria hiyo kwa nguvu zote kwa wananchi huku wahudumu wa Afya wakitakiwa kuondokana na mazoea katika utoaji wa huduma. Said Makola ni mratibu wa mpango wa Elimu ya Bima ya Afya kwa Wote kutoka Wizara ya Afya akizungumza katika mafunzo hayo alisema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya wanao wajibu wa kutoa miongozo na tafsiri ya sheria ya bima ya afya pamoja na kanuni zake ili ziweze kutekelezwa kwa urahisi katika mikoa yote Tanzania Bara. Alisema zaidi kaya laki 9.3 sawa na asilimia 23.7 kwa hawamu ya kwanza zimetambuliwa...
Marato tv - Sauti ya Jamii