Skip to main content

Posts

Showing posts from November 4, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri mkuu ameagiza Taasisi za utafiti nchini kuingia katika sekta ya afya,mazingira na wanyama

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameziagiza idara na taasisi za utafiti na elimu ya juu ziendelee kufanya tafiti za kisayansi ili kutafuta suluhisho za changamoto zenye mwingiliano wa afya ya binadamu, afya ya wanyama, na afya ya mazingira.  Ameongeza kuwa idara na taasisi za Serikali zinapaswa kutumia matokeo ya tafiti hizo katika utekelezaji wa mipango mbalimbali ya kitaifa. Ametoa maagizo  hayo jana (Jumatatu, Novemba 04, 2024)  alipofungua Mkutano wa Kitaifa wa Afya Moja katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa  Arusha (AICC) Jijini Arusha. Aidha, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa Taasisi zinazohusika na masuala ya afya ya jamii, wanyama na mazingira zitenge fedha na kuweka katika mipango ya taasisi hizo afua za kuthibiti magonjwa ya kizonotiki, usugu wa vimelea dhidi ya dawa, magonjwa yasiyoambukiza, mabadiliko ya tabia nchi, na usalama wa chakula. “Wizara za kisekta, na Mamlaka za Serikali za Mitaa, andaeni mipango kazi na taratibu za usimamizi kwa ajili ya utekeza...

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Cuba na Tanzania wakutana

Havana, Novemba 4, 2024.- Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba, Bruno Rodríguez Parrilla, amempokea leo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa. Mheshimiwa Mahmoud Thabit Kombo. Katika hali ya udugu, uhusiano wa kihistoria baina ya mataifa hayo mawili ulibadilishana, kwa kuzingatia urafiki wa viongozi wa kihistoria Fidel Castro Ruz na Julius Nyerere, na nia ya kuendelea kuimarisha uhusiano na ushirikiano katika maeneo yenye maslahi ya pamoja ilionyeshwa. Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba aliishukuru Tanzania kwa uungaji mkono wake, ndani ya Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa, kwa matakwa ya serikali ya Cuba na wananchi kwa kuondoa vikwazo vya kiuchumi, kibiashara na kifedha vilivyowekwa na Marekani.      Mgeni huyo mashuhuri aliambatana na Mhe. Mheshimiwa Humphrey H. Polepole, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Jamhuri ya Cuba; na Balozi Swahiba H. Mndeme, mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika wa Wiz...

Esther Malleko aiomba serikali kuendelea kuboresha bajeti za Tawa, Ncaa na Tanapa

  Serikali itaendelea kuboresha bajeti ya Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori(TAWA), Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kutegemeana na hali ya ukusanyaji wa mapato ya Serikali ili kuimarisha shughuli za ulinzi na kuboresha miundombinu ya utalii. Haya yamebaishwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dunstan Kitandula (Mb) alipokuwa akijibu swali la Mhe. Esther Edwin Malleko (Mb) aliyetaka kujua kuna mkakati gani wa kuwaongezea bajeti TANAPA na TAWA kwani majukumu yao ni makubwa ikilinganishwa na bajeti inayotengwa. "Je, kuna mkakati gani wa kuwaongezea bajeti TANAPA na TAWA kwani majukumu yao ni makubwa ikilinganishwa na bajeti inayotengwa?" - Mhe. Esther Edwin Malleko, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro  "Sekta ya Utalii imekuwa sana hasa baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kutengeneza Filamu ya Royal Tour. Je, Serikali haioni umuhimu wa kurejesha utaratibu wa zamani ili

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi ashiriki dhifa ya chakula cha usiku nchini china

   04 Novemba 2024 📍Shanghai China Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, pamoja na Mke wake, Mama Mariam Mwinyi, wamehudhuria dhifa ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na Waziri Mkuu wa China, Mhe. Li Qiang, katika Ukumbi wa Grand Hall. Dhifa hiyo maalum ni sehemu ya mapokezi ya viongozi na wafanyabiashara kutoka mataifa mbalimbali, ambao wanatarajiwa kuhudhuria ufunguzi rasmi wa Maonesho ya 7 ya China International Import Expo (CIIE) kesho, tarehe 5 Novemba 2024

Wafanyabiashara soko la kimataifa la mwaloni kirumba walia na hatua ya sehemu ya soko hilo kugeuzwa bandari

  Siku chache baada ya Mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanzania(TPA)kuanza kusimamia utendaji kazi wa kibandari katika mwalo wa kirumba manispaa ya ilemela Jijini Mwanza,wafanyabiashara wa soko la kimataifa la mwaloni kirumba wamepinga uamuzi huo. Wafanyabiashara hao wanadai kuwa hatua ya Tpa kuchukua usukani wa shughuli za kibandari katika eneo hilo imeanza kuathiri shughuli zao zikiwemo za usafirishaji. Wakizungumza na waandishi wa habari,baadhi ya watoa huduma za usafirishaji katika eneo hilo wameiomba serikali kupitia upya uamuzi wake ili kuongeza ufanisi kwenye uendeshaji wa shughuli zao. Wamedai kuwa kabla Mamlaka ya usimamizi wa bandari kuanza kusimamia utendaji kazi wa mwalo wa kirumba,mitumbwi inayosafirisha abiria iliruhusiwa kubeba mizigo kidogo tofautina sasa. ‘’Tokea bandari waingie eneo hili,mitumbwi ya abiria hairuhusiwi kubeba mzigo wowote,hili linatuathiri na hatupati faida kutokana na abiria kupatikana wakati wa giza ikilinganishwa na wakati wa mbalamwezi’’alisema...

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...