Skip to main content

Posts

Showing posts from March 19, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais Samia alivyoitoa Wizara Maji kutoka kuwa ya kero na lawama hadi ya faraja

  Na: Dk. Reubeni Lumbagala Maji ni miongoni mwa huduma muhimu ya kijamii. Maji ni huduma ambayo kila mtu anahitaji tena kila siku. Utahitaji maji kwa kuoga, kupikia, kufulia, kupigia mswaki, kunyweshea mifugo, kumwagilia maua au bustani. Mambo yanayohitaji maji ni mengi. Maji haya yanapaswa kusambazwa kutoka katika vyanzo vyake mathalani mito, maziwa na mabwawa hadi katika makazi ya watu ili yaweze kutumiwa. Wananchi wanataka maji yawafikie katika makazi yao, hiyo ndiyo kiu na hitaji lao. Waziri wa Maji, Jumaa Aweso anatoa ushuhuda wa hali ya maji iliyokuwa hapo nyuma. "Kitendo cha wananchi wa maeneo mbalimbali nchini kukosa maji kuliifanya Wizara ya Maji kuwa ni Wizara ya kero na lawama, lakini kwa kazi kubwa alizofanya Rais Dk. Samia, leo Wizara imekuwa faraja kwa wananchi," anasema Aweso. Maneno  ya Waziri Aweso yanatokana na ukweli kuwa katika maeneo mengi nchini, wananchi walikabiliwa na shida ya maji, hivyo walikuwa na lawama nyingi kwa Wizara ya Maji kwani ndiyo yenye...

Wananchi wa Kijiji Cha Kiriba Wajitolea Kujenga Shule ya Sekondari

 MARA KATIKA kuunga Mkono jitihada za Serikali kwenye Sekta ya Elimu nchini, Wananchi wa kijiji cha Kiriba, mkoani Mara kwa Kushirikiana na Benki ya NMB,CRDB pamoja na ofisi ya Mbunge wamejitolea kujenga shule ya ufundi ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuwafanya vijana kuwa na Ujuzi. Hatua hiyo imeifanya Familia ya Mashenene kuanza kujenga chumba kimoja cha darasa ikiwa ni mchango wa familia hiyo kwenye ujenzi wa sekondari hiyo ambapo Familia hiyo inaanza kupau chumba chao cha darasa wiki ijayo. Akiambatana na Wananchi katika eneo la ujenzi huo leo March 19,2026 Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo katika kuunga jitihada hizo za ujenzi wa "Mwigombe Technical Secondary School" kijijini Kiriba. Kadhalika, Michango ya ujenzi imeshaanza ambapo imeanza kutolewa na,Wakazi wa Kijiji cha Kiriba,Wazaliwa wa Kijiji cha Kiriba,Mbunge wa Jimbo, Wadau wa Maendeleo zikiwemo Benki za NMB na CRDB. "Sisi wananchi wa Kiriba Tunakuomba mchango wako uchangie ujenzi wa s...

Dede awafuturisha wanahabari Mwanza

Mwenyekiti wa Chama cha Madereva wa Malori na Mabasi Tanzania (TLDTA), Hassan Dede amehimiza waandishi wa habari kufanya kazi kwa uzalendo kwa manufaa ya nchi yao, Tanzania. Dede ameyasema hayo Alhamisi Machi 19, 2026 wakati wa Iftar aliyoiandaa kwa ajili ya waandishi wa habari jijini Mwanza. Amesema waandishi wa habari wana mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi yao hivyo ameona ni vyema kujumuika nao pamoja kama ishara ya umoja, mshikamano na upendo katika mwezi mtukufu wa Ramadhani na Kwaresma. Naye mmoja wa waandishi wa habari jijini Mwanza, George Binagi amemshukuru Dede kwa kuthamini mchango wao kwani Iftar hiyo imeimarisha umoja na mshikamano kwa wanahabari na wadau mbalimbali wa maendeleo jijini Mwanza

Kanali Mtambi aipongeza Takukuru Mkoa wa Mara

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo tarehe 19 Machi, 2026 amefanya mahojiano ya vipindi vya televisheni vinavyoratibiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU katika Jijini Dodoma.  Akizungumza katika mahojiano hayo Mhe. Mtambi ameipongeza TAKUKURU Mkoa wa Mara kwa ushirikiano wanaoutoa katika usimamizi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Mkoa wa Mara.  ' TAKUKURU inatusaidia sana kufanya ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo, ni jicho letu katika kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa wakati na katika ubora unaotakiwa" amesema Mhe. Mtambi.  Mhe. Mtambi amesema kutokana na kazi inayofanywa na TAKUKURU wananchi wa Mkoa wa Mara wanauhakika wa miradi yao inatekelezwa vizuri, kupata huduma bora, kupunguza mianya ya rushwa.  Mhe. Mtambi ametoa mfano wa TAKUKURU kufuatilia Shule ya Sekondari ya Kasoma Halmashauri ya Wilaya ya Musoma ambapo awali shule hiyo ilikuwa inatumia kuni kupika chakula lakini baada ya ufuatiliaji wa TAKUKURU na ...

Mfalme wa Sweden amuaga Balozi Matinyi

Mfalme Carl XVI Gustaf wa Sweden, amemuaga aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mhe. Mobhare Matinyi, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Jumba la Kifalme jijini Stockholm, leo tarehe 19 Machi, 2026. Katika mazungumzo yao mafupi, viongozi hao walijadiliana namna ya kuendelea kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizi mbili katika sekta za nishati, mazingira, kilimo, utalii, miundombinu, madini na teknolojia. Mfalme Gustaf aliipongeza Tanzania kwa kuweka utulivu nchini na kubuni mipango thabiti ya kutafuta maendeleo na kukuza uchumi wake licha ya changamoto nyingi zinazoikabili dunia nzima hivi sasa. Balozi Matinyi alimshukuru Mfalme Gustaf kwa ushirikiano mzuri alioupata katika kipindi alichohudumu nchini Sweden ambapo Tanzania imefaidika katika sekta za nishati, kilimo, miundombinu, teknolojia na elimu ya juu. Hii ilikuwa mara ya tatu kwa Balozi Matinyi kukutana na Mfalme Gustaf tangu awasili nchini Sweden mwezi Mei 2025. Mara ya kwanza ilikuwa wakati wa kukabidhi hati zake za...

Hospitali ya JWTZ Tabora Yatoa Msaada

Maafisa na Askari wa Hospitali ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania  Kanda ya Tabora (ZMH-Tabora)iliyopo Kambi ya Mirambo wametembelea vituo vya kutunza watu wasiojiweza vya Igambiro na Charity Missionary Sisters of Tabora vilivyopo katika Halmashauri ya Manispaa Tabora, Mkoani Tabora tarehe 18 Machi 2026. Ziara hiyo imefanyika kwa dhumuni la  kuwafariji  watoto wanaotunzwa kwenye kituo cha  Igambiro ambao walipata Janga la Kuunguliwa  Bweni katika kituo hicho na kusababisha watoto idadi 04  kupoteza maisha.  Licha ya kutembelea Watoto hao, pia walitembelea  wazee, watoto na wenye uhitaji maalumu  katika kituo cha Charity Missionary Sisters of Tabora. Akizungumza kwa niaba ya Kamanda Kikosi Luteni Kanali Fredrick Maeda, Afisa Ugavi wa Kikosi cha ZMH Tabora Meja Stadius Rwiza alisema dhumuni la kutembelea vituo hivyo ni kuwaona, kutoa salamu na  kuwapa mkono wa pole na kuwatia moyo kwa changamoto wanazopitia watoto hao baada ya bwen...

Makamu wa Rais aongoza maadhimisho ya siku ya misitu na kampeni ya upandaji miti kitaifa

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ameelekeza uongozi wa Mikoa yote nchini kuhakikisha jitihada za upandaji miti zinaendelezwa kwa kuwekewa mkakati mahsusi unaojumuisha makundi yote katika jamii na kuzingatia ikolojia ya maeneo husika, ikiwa ni pamoja na kuzuia uvamizi na uharibifu wa maeneo yote ya hifadhi ya misitu. Makamu wa Rais, ametoa maelekezo hayo, wakati akifungua Maadhimisho ya Siku ya Misitu Duniani na Siku ya Upandaji Miti Kitaifa, iliyofanyika katika Uwanja wa Ilulu mkoani Lindi, leo tarehe 19 Machi 2026. Amesema ni muhimu kuhakikisha wananchi wanaoishi jirani na misitu ya asili na mashamba ya miti wanapatiwa elimu endelevu kuhusu matumizi bora ya ardhi, udhibiti wa uchomaji moto holela, na usimamizi shirikishi wa misitu ya vijiji. Aidha, Makamu wa Rais amehimiza umuhimu wa Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) kufanya tafiti zitakazojibu changamoto mbalimbali ambazo wakulima wa ...