Skip to main content

Posts

Showing posts from September 17, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Uyovu Wamkubali Dkt. Samia, Kumpigia Kura Nyingi Oktoba 29

📌 *Dkt. Biteko kuifanya Uyovu kuwa kitovu cha biashara Bukombe* Mgombea Ubunge wa Jimbo la Bukombe kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Doto Mashaka Biteko amesema kuwa mgombe Urais kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameiwezesha Kata ya Uyovu kimaendeleo hivyo wananchi hao hawana budi kumpigia kura nyingi Oktoba 29  mwaka huu. Dkt. Biteko amesema hayo Septemba 17, 2025 wakati wa mkutano wa kampeni katika Kata ya Uyovu wilayani Bukombe mkoani Geita ikiwa ni sehemu Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba 29, mwaka huu. “ Hakuna siku ambayo nilimuomba maendeleo Dkt. Samia kwa ajili ya watu wa Uyovu na Geita akatunyima, ametupa fedha za ujenzi wa barabara nyingi ikiwemo ya kutoka Ushirombo hadi Katoro hata juzi tulimuomba barabara ya Geita kwenda Nzela hadi Sengerema kwa kiwango cha lami yote haya atatusaidia huyu ni mama ni msikivu,” amesema Dkt. Biteko. Ameongeza kuwa katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wa Dkt. Samia chini ya CCM kati...

Kongole Takukuru Kuikumbusha Jamii Kukataa Rushwa Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Na: Dkt. Reubeni Lumbagala, Tanga Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Oktoba 29, 2025 ni siku ambayo Taifa letu litafanya Uchaguzi Mkuu ili kuchagua viongozi katika nafasi za urais, ubunge na udiwani. Agosti 28, 2025, kampeni zilizinduliwa rasmi ambapo wagombea walianza kunadi Ilani za vyama vyao na sera zao kwa ujumla katika kipindi cha miaka mitano ijayo 2025-2030 ili kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo. Rushwa ni moja ya tatizo kubwa hasa kipindi hiki cha uchaguzi kwani baadhi ya wagombea wasio na maadili hutoa rushwa ili kushawishi wapigakura wawapigie kura kuwachagua katika nafasi mbalimbali za uongozi. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) haijalala, ipo macho kuhakikisha wananchi wanapata elimu ya mapambano dhidi ya rushwa kwa kutumia njia mbalimbali za utoaji elimu ili kuhakikisha nchi yetu inapata viongozi bora wasiotokana na rushwa. Sanjari na hilo, Takukuru imedhamiria kuwachukulia hatua kali wale wote watakaobainika n...

Tutalinda Kwa Bidii Kubwa Tunu za Muungano Wetu -Dkt Samia

 17 Septemba 2025- Kusini Unguja Mgombea wa Urais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan Leo ameendelea na kampeni zake kuinadi Ilani ya CCM Makunduchi, Zanzibar, Katika mkutano wake Dkt. Samia alielezea kuhusu kulinda tunu kuu, muhimu na msingi wa Muungano, Amani na utulivu ili tufikie malengo makubwa kama Taifa. Muungano wetu wa Tanzania ni hazina kubwa na ya kipekee barani Afrika. Ni daraja linalotuunganisha kutoka Visiwani hadi Bara, likitufanya tuwe taifa lenye mshikamano, upendo na ushirikiano wa kweli. Tuwalinde na kuuenzi Muungano huu kwa vitendo, kwani ni urithi wa vizazi vilivyopita na ni dhamana ya vizazi vijavyo.