Skip to main content

Posts

Showing posts from April 30, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Watumishi wa Tume ya Madini washiriki Maadhimisho ya mei mosi kitaifa Njombe

📍Njombe Watumishi wa Tume ya Madini kwa kushirikiana na Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Njombe wameshiriki kikamilifu katika Maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) yaliyofanyika kitaifa Mei 1, 2026 katika Viwanja vya Lunyanywi, Halmashauri ya Mji wa Njombe. Maadhimisho hayo yanayofunguliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, yanahusisha wafanyakazi kutoka sekta mbalimbali nchini waliokusanyika kuenzi mchango wa wafanyakazi katika maendeleo ya taifa pamoja na kujadili ustawi wao na kuboresha mazingira ya kazi. Watumishi wa Tume ya Madini wameshiriki katika maandamano rasmi pamoja na taasisi nyingine za umma na binafsi, wakionesha mshikamano wa wafanyakazi wa Sekta ya Madini katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kukuza uchumi kupitia rasilimali madini. Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu isemayo, “Kazi zenye staha ni nguzo imara kwa maendeleo endelevu katika utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050,” imelenga kuhamasisha a...

Uchaguzi mdogo EALA kufanyika Mei 5,2016

  KATIBU wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Baraka Leonard, ametangaza rasmi kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa kuchagua wajumbe watatu watakaoiwakilisha Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA), utakaofanyika Mei 4, 2026. Akizungumza na Waandishi wa Habari Leo April 30,2026 katika Ofisi za Bungeni Jijini Dodoma, katibu wa Bunge Baraka Leonard Amesema uchaguzi huo unalenga kujaza nafasi zilizoachwa wazi kufuatia James Kinyasi Millya, Dkt. Ng’waru Jumanne Maghembe, na Angela Charles Kizigha kuwa wabunge wa Bunge la Tanzania. “Kwa mujibu wa sheria, wabunge hawa wamekoma kuwa wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki mara baada ya kuapishwa kuwa wabunge wa Bunge la Tanzania,” amesema. Ameeleza kuwa uchaguzi huo unafanyika kwa kuzingatia kanuni na sheria mbalimbali za Bunge pamoja na Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, huku ukilenga kuhakikisha nafasi zilizo wazi zinajazwa kwa wakati na kwa kuzingatia uwakilishi wa makundi maalum. “Uchaguzi huu unafanyika kwa mujibu wa ta...

Jokate atoa mwanga Mpya Kwa Wanafunzi wa Sayansi kupitia mafunzo ya Vitendo

MWANZILISHI wa Kidoti Foundation, Jokate Mwegelo, ameendelea kuonesha kwa vitendo dhamira yake ya kuinua elimu ya sayansi nchini baada ya kufanikisha ziara ya wanafunzi 110 wa masomo ya sayansi kutoka Shule ya Sekondari Jokate Mwegelo, Kisarawe mkoani Pwani, waliotembelea STEM Park jijini Dar es Salaam. Ziara hiyo imekuwa daraja muhimu la kuwaunganisha wanafunzi na ulimwengu halisi wa teknolojia, ikilenga kuwapa uzoefu wa moja kwa moja nje ya darasa. Kupitia mpango huo, wanafunzi wamepata fursa ya kuona, kugusa na kujifunza kwa vitendo dhana za kisayansi, jambo linalochochea uelewa wa kina, ubunifu na ari ya kujifunza zaidi. Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Jokate amesema kuwa lengo kuu la Kidoti Foundation ni kuhakikisha vijana wanapata elimu inayogusa uhalisia wa maisha ya sasa, hususan katika nyanja za sayansi na teknolojia. Ameeleza kuwa kuwapeleka wanafunzi katika mazingira kama hayo ni njia bora ya kuwajengea uwezo wa kufikiri kwa ubunifu na kutatua changamoto kwa kutumia maarif...

Dkt.Mwigulu Awasili Njombe,kushiriki Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Mei 1, 2026 amewasili mkoani Njombe kushiriki Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi). Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Kaulimbiu ya Maadhimisho hayo ni : _“Kazi zenye Staha ni Nguzo Imara kwa Maendeleo Endelevu katika Utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050”_

From Blueprints to Bridge Decks: UDSM CoET Students Learn On-Site with CRJE

  By Staff Writer  CRJE (East Africa) Ltd opened the gates of its Mbezi Beach project site on Thursday to host faculty and students from the University of Dar es Salaam’s College of Engineering and Technology (CoET) for a full-day Site Open Day and Youth Bridge Skills Challenge.  The event, organized by CRJE as part of its commitment to skills transfer and China-Tanzania cooperation, brought together over 200 future engineers, government officials, regulators, and industry professionals for practical learning, competition, and mentorship. The Open Day showcased CRJE’s active construction operations, giving participants direct exposure to large-scale infrastructure delivery, safety management, and technical problem-solving. Through live demonstrations, guided site tours, and the “Future Star” competition, CRJE created a platform where classroom theory met field practice — reinforcing its role in developing Tanzania’s next generation of engineering talent. In his opening re...

Serikali yatoa wito Kwa vyuo vikuu kufanya mawasiliano kabla kuunda program za masoko kutatua changamoto ya ajira

Maelekezo hayo yametolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora , Mh. Ridhiwani Jakaya Kikwete alipokuwa anajibu swali la nyongeza lililoulizwa na Mbunge wa Viti maalum Bi. Asha Juma Feruzi alipotaka kufahamu serikali imejipangaje kutatua tatizo la wahitimu wengi wa vyuo kukosa ajira kwa kuwa wamesoma kozi ambazo hazipo katika mfumo wa Ajira Nchini.  Mheshimiwa Waziri Kikwete amelihakikishia Bunge na mheshimiwa Mbunge Feruzi kuwa serikali inafanya juhudi kubwa kuhakikisha kuwa changamoto iyo inatoweka kwa kuelekeza vyuo kushirikiana na wizara mama na Taasisi mbalimbali za serikali kuwasiliana kabla ya kupitishwa kwa Miundo ya Maendeleo ya Utumishi ya kada husika.  Akizungumza Bungeni, Mheshimiwa Waziri aligusia mfano wa hatua iliyofanywa na serikali na chuo cha Mzumbe Morogoro kutatua changamoto ya kada ya Maafisa wa Maendeleo ya Vijana. 

Handeni wajipanga kupokea wanafunzi wa elimu ya Amali

  Na Mashaka Mhando, Mkata HALMASHAURI ya Wilaya ya Handeni imetangaza mpango mkakati wa kukabiliana na ongezeko la kihistoria la wanafunzi wa kidato cha kwanza unaotarajiwa mwaka 2028, huku Jeshi la Polisi na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) wakitakiwa kuimarisha usalama wa miundombinu. Akizungumza katika mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika Leo Aprili 30, 2026, katika ukumbi wa Mbweni Mkata, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Saitoti Stephen, amesema mwaka 2028 utashuhudia changamoto ya kipekee ya kimfumo. Msongamano wa Wahitimu 2027 Saitoti amefafanua kuwa mabadiliko ya mtaala wa elimu yatasababisha makundi mawili ya wahitimu kwa mwaka 2027; kundi la darasa la saba (mfumo wa zamani) na darasa la sita (mfumo mpya). Hali hiyo inazua hitaji la dharura la upanuzi wa miundombinu ya shule ili kupokea 'Double Intake' hiyo. "Tunapaswa kuanza maandalizi ya miundombinu ya vyumba vya madarasa na samani sasa kupitia Kamati za Maendeleo ya Kata (WDC), ili...

Timu ya bweni yaifunga Tungamaa,Robo fainali Aweso Vijana Cup

NA: MWANDISHI WETU, PANGANI  Timu kutoka Kata ya Bweni imefanikiwa kuifunga timu ya Kata ya Tungamaa kwa ushindi wa (1-0), mechi iliyochezwa Aprili 29, 2026, katika uwanja wa Kikokwe, Kata ya Bweni, wilayani Pangani mkoani Tanga. Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa, timu ya Bweni ilipata goli kupitia kwa mchezaji wake Marino Junior katika dakika ya 35 ya mchezo, jambo lililoiwezesha Bweni kuondoka na alama tatu muhimu. Mratibu wa mashindano hayo, Ramadhani Kibendera amesema mashindano ya Aweso Vijana Cup yamevuka matarajio kwani wananchi wanajitokeza kwa wingi viwanjani na kila timu inacheza kana kwamba inacheza fainali. Sambamba na hilo, Kibendera amesema ligi ni ya kipekee kwani haki na sheria za mpira wa miguu zinazingatiwa na waamuzi.  "Kwa kweli ligi ni moto, tangu ligi ianze, hamasa ni kubwa na katika jambo ambalo limekuwa nguzo kubwa ya ligi hii ni uzingatiaji wa sheria na kanuni za mchezo wa mpira wa miguu, na hakujatokea malalamiko yeyote tangu ligi izindul...

Kutoka Darasani Hadi Ujenzi Halisi: Wanafunzi wa UDSM Wajifunza CRJE

  Na Mwandishi Wetu Kampuni ya CRJE (East Africa) Ltd imefanya Shindano la kukuza Ujuzi kwa wanafunzi wa Chuo cha Uhandisi na Teknolojia (CoET) cha UDSM. Shindano hilo lilifanyika kupitia _Site Open Day_ katika mradi mkubwa wa Kampuni hiyo uliopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam. Lengo likiwa ni kuhamisha ujuzi kwa vitendo kutoka kwa wataalamu wa Kichina kwenda kwa wanafunzi wa uhandisi wa Kitanzania ili kuimarisha ushirikiano kati ya China na Tanzania. Kwa mara ya kwanza, wanafunzi wa CoET walitoka kwenye madaftari na slaidi za darasani na kuingia moja kwa moja kwenye uhalisia wa ujenzi. Tukio hilo liliwapa fursa ya kushuhudia ujenzi halisi, usimamizi wa usalama, na utatuzi wa changamoto katika eneo la ujenzi. Kupitia ziara ya mradi, na shindano la “Nyota wa Baadaye”, CRJE iliweza kuwaonyesha wanafunzi wa uhandisi tofauti kati ya nadharia ya darasani na uhalisia wa kazi. Hii ni hatua inayoziba pengo kati ya taaluma na sekta. Akizungumza katika hafla hiyo, Bw. Zhang Cuishan, Naibu ...