Skip to main content

Posts

Showing posts from October 16, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Eng Magesa Mwita Aipongeza Shule ya Sekondari ya Morembe-Musoma Mjini

  Mhandisi Mwandamizi katika Sekta ya Ujenzi, Eng. Magesa Mwita amesema hatua ambayo inachukuliwa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya ujenzi wa shule za mchepua wa Sayansi na ufundi nchi nzima itawezesha kutoa jawabu la tatizo kubwa la ajira kwa vijana nchini. Mhandisi Magesa ametoa kauli hiyo Oktoba 16 mwaka huu 2025 mjini Musoma  wakati akihutubia wanafunzi,walimu na wazazi wa shule ya Sekondari ya Morembe katika mahafali ya kidato cha nne ya wanafunzi wa shule hiyo. Amesema Serikali imefanya uwekezaji mkubwa wa shule hizo kwa kila mkoa nchini  kama moja ya mkakati wa kuwawezesha vijana kupata ujuzi wa kukabiliana na tatizo la ukisefu wa ajira kwa vijana  Kwa sababu hiyo amewapongeza wahitimu katika mahafali hayo, huku akitoa wito kwa wanafunzi wote kuweka mkazo kwa masomo ya mchupua wa Sayansi kwani amesema kufanya hivyo kutawawezesha kufika mbali na kumudu changamoto za kimaisha. "Wanafunzi wote wekeni mkazo kwenye masomo ya Saya...

Edwin Soko asema ahadi za mgombea wa CCM zinagusa Dira ya Taifa ya maendeleo 2050

Mwandishi wetu ;Mwanza  Mwandishi wa habari Mwandamizi na mtetezi wa haki za biinadamu Edwin Soko ameweka bayana kuwa, mgombea wa CCM katika nafasi ya urais  amejitahidi kugusa dira ya Taifa ya maendeleo 2050 pale   anapotoa ahadi kwenye mikutano  ya kisiasa inayoendelea. Soko amesema  hayo Leo Jijini Mwanza kuwa, amekuwa  akifuatilia kwa umakini mikutano yote ya wagombea wa nafasi ya urais kwa vyama vyote kumi na Saba vilivyosimamisha wagombea kwa nafasi ya urais  na kubaini Chama Cha Mapinduzi kupitia mgombea wake Samia Suluhu na Makamu wake Dakatari Emmanuel  Nchimbi wamekuwa wakitoa ahadi  zinazogusa mwelekeo wa dira ya Taifa ya Maendeleo  2050 . " Ni vizuri  wagombea wengine  toka vyama vyote vya siasa  watambue kuwa dira ya maendeleo ya Taifa sio nyaraka ya Chama Cha Mapinduzi peke yake bali ni nyaraka ya watanzania vikiwemo  vyama vyote vya siasa  iliyoandaliwa na wataalamu wa Nchi kwa gharama  y...

Msama-watanzania Epukeni Maandamano Yasiyo na Tija Kwa Taifa Letu

 MKUGENZI WA DIRA TV, DIRA REDIO, MSAMA PROMOTIONS NA KADA WA CCM Alex Msama Mwita ametoa wito kwa Watanzania kuzidi kupuuza minong'ono ya baadhi ya watu wanaotaja maandamano siku ya Uchaguzi Mkuu, Oktoba 29 mwaka huu na badala yake wajitokeze kwa wingi kupiga kura, kuchagua viongozi bora watakaowaletea maendeleo ya huduma za kijamii. Akizungumza leo Oktoba 16, 2025, katika mahojiano maalum na baadhi ya waandishi wa habari alipotakiwa kutoa maoni yake juu ya uzushi wa maandamano siku ya Oktoba 29, Msama aliwataka Watanzania kuziba pamba masikioni juu ya upotoshaji huo. "Siku zote sisi Watanzania tumekuwa tukijivunia uungwana, utu, mshikamano, umoja, usikivu na Amani yetu, hayo mambo mengine yanabaki kuwa propaganda za watu wachache wasiopenda utulivu tulionao kama Watanzania. "Niendelee kuwaomba Watanzania wenzangu, maana nimekuwa nikisema kila mara, kwamba katika kipindi hiki cha Uchaguzi Mkuu, maneno mengi ya kuzusha yatakuwa mengi tuyapuuze," alisema Msama na kuon...

Serikali Itaendelea Kufanya Mageuzi Sekta ya Kilimo-Majaliwa

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali imedhamiria kuendelea kufanya mageuzi katika sekta ya kilimo ili kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwa kitovu cha uzalishaji wa chakula katika ukanda wa Afrika Mashariki. Amesema lengo la Serikali ni kuendelea kuimarisha usalama wa chakula, kupunguza utapiamlo na kuijenga Tanzania yenye wananchi wenye afya bora, nguvu kazi imara na uchumi unaojitegemea. Amesema hayo leo Alhamisi (Oktoba 16, 2025) wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Mkoani Tanga, kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Usagara. “Pamoja na mipango hiyo, Serikali itaendelea kuimarisha mazingira rafiki ya uwekezaji, ushirikiano, na ubunifu, ili kuhakikisha nchi inakuwa na chakula cha kutosha kwa matumizi ya ndani na ziada kwa mauzo ya nje” Amesema kuwa Serikali katika kuhakikisha imefanya mageuzi makubwa katika sekta ya kilimo, iliongeza bajeti ya sekta hiyo kutoka shilingi bilioni 246 mwaka 2020/2021 hadi kufikia shilingitrili...

Korttin kwa kulawiti mtoto wa miaka 8 - Mwanza

Mkazi wa Luchelele na mfanyabiashara, Seif Msumari Hozza (26), amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza leo Oktoba16, 2025 kwa tuhuma za kulawiti mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 8 (jina limehifadhiwa kwa sababu za kisheria). Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Mhe. Aman Sumari, Wakili wa Serikali Rose Kimaro ameieleza mahakama kuwa tukio hilo lilitokea kati ya mwezi Agosti na Septemba 2025 katika eneo la Siluvin, Kata ya Luchelele jijini humo, ambapo mshtakiwa anadaiwa kutenda kitendo hicho cha ukatili dhidi ya mtoto huyo. Katika kesi hiyo ya jinai yenye namba 25168/2025, mshtakiwa anakabiliwa na shtaka moja la kulawiti, kinyume na Kifungu cha 154(1)(a)(2) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16, marejeo ya mwaka 2023. Hata hivyo, mshtakiwa amekana shtaka hilo. Hakimu Sumari anayesikiliza kesi hiyo ameeleza kuwa kosa hilo linadhaminika kwa masharti, ikiwemo kuwa na wadhamini wawili wenye vitambulisho halali vya taifa, barua za utambu...

Majaliwa Mgeni Rasmi Siku ya Chakula Duniani

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Oktoba 16, 2025 ni mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Mkoani Tanga, kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Usagara. Madhimisho hayo ambayo hufanyika kila mwaka yanalenga kuamsha ari ya uzalishaji wa mazao ya chakula ikiwemo yaliyoongezewa virutubishi; kuhimiza ulaji bora na kuongeza tija ya uzalishaji wa chakula ili kujihakikishia usalama wa chakula na lishe kuanzia ngazi ya kaya hadi Taifa. Maadhimisho hayo yanakaulimbiu isemayo _“Tuungane Pamoja Kupata Chakula Bora Kwa Maisha Bora Ya Baadaye.”_

Dkt.Nchimbi Ndani ya Jimbo la Mpwapwa Muda Huu Mkoani Dodoma

Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emmanuel John Nchimbi tayari amewasili  katika uwanja wa mji mpya,Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma leo Oktoba 16,2025 kuendelea na mikutano yake ya hadhara ya kampeni ya kusaka kura za ushindi wa kishindo wa CCM baada ya kuhitimisha kampeni zake  jana mkoani Singida.