Skip to main content

Posts

Showing posts from November 18, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais Samia amelipa viingilio vyote kuiona stars leo kea mkapa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan awalipia viingilio watanzania wote kwenda uwanjani na kushuhudia mchezo wa Tanzania dhidi ya Guinea unatarajia kuchezwa leo Novemba 20-2024 uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Mechi hiyo ya kufuzu kwa Mashindano ya Mataifa Afrika (AFCON) itachezwa leo jioni katika Uwanja huo wa Benjamin Mkapa, Jijini Dar es Salaam. Akiwasilisha taarifa hiyo, Dkt. Doto Biteko amesema Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza kuwa watu wote waingie uwanjani bure na hivyo wananchi wajitokeze kwa wingi kwenda kuitia moyo timu yetu ya Taifa Stars na kwakweli imefanya vizuri sana kwenye mechi iliyopita na tunaamini mechi hii tutashinda ili tuweze kusonga mbele.

Waziri Mkuu amwakilisha Rais Dkt. Samia Mkutano wa Kimataifa wa Madini na Uwekezaji 2024

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Novemba 19, 2024 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa Kimataifa wa Madini na Uwekezaji Tanzania, kwenye kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo unawakutanisha wadau wa madini wanaojishughulisha na utafutaji, uchimbaji, uchenjuaji, uongezaji thamani madini, wasimamizi wa Sekta kutoka Serikalini, watoa huduma migodini na wafanyabiashara. Pamoja na malengo mengine, mkutano huo umelenga kuweka mipango ya kuvutia uwekezaji  wa nje ya nchi, kukuza usimamizi bora wa rasilimali za Madini pamoja na kubadilishana uzoefu na washiriki kutoka maeneo mbalimbali duniani. Kaulimbiu ya mkutano huo ni _Uongezaji wa Thamani ya Madini kwa Maendeleo ya Kiuchumi

Waziri Kombo aongoza Mkutano wa dharura wa kamati ya Mawaziri wa asasi ya siasa, ulinzi na usalama ya Sadc

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), ameongoza Mkutano wa Dharura wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC-Organ) uliofanyika tarehe 17 Novemba , 2024 jijini Harare, Zimbabwe. Waziri Kombo ameungana na Mawaziri wenzake wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kujadili hali ya usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) pamoja na njia mbalimbali za kurejesha amani nchini humo. Akizungumza katika Mkutano huo, Balozi Kombo amebainisha kuwa Tanzania inaunga mkono juhudi zote zinazofanyika katika kurejesha amani Mashariki mwa DRC.  Aidha, Balozi Kombo amezisisitiza Nchi za SADC kushirikiana ili kutafuta suluhu ya kudumu ya kurejesha amani Mashariki mwa Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). “Ni jukumu la kila Nchi Mwanachama kushirikiana kwa pamoja katika kurejesha amani na usalama kwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (...

Dkt. Biteko amesema hataki kusikia visingizio kwa mashirika ya umma kushiriki kwenye michezo

*📌 Asema haiwezekani kutenga bajeti ya michezo kisha kuitumia vinginevyo* *📌 Amtaka Msajili wa Hazina kushiriki ufungaji bila kuwakilishwa* *📌 Shimmuta yashukuru kwa ushirikiano wa Serikali kuongeza wanachama* *Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati* Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mheshimiwa Dkt. Doto Biteko amemwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Phillip Mpango kufungua mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Mashirika ya Umma nchini SHIMMUTA na kuagiza mashirika kuondokana na visingizio visivyo na msingi ili kutimiza azma ya mashindano hayo. Dkt. Biteko ametoa maelekezo hayo Jijini Tanga ambapo amesema kumekuwa na visingizio vya kuwakosesha watumishi wa umma kushiriki mashindano ilhali ni suala linalofahamika na liko kwenye kalenda ya kila mwaka ya mashirika husika. “Utaratibu huu wa kukubaliana jambo lakini jambo tulilokubaliana halifanyiki inatufanya tukose uhalali wa kuwasimamia wengine, nilitaka kujua kwanini hatupeleki wa...

Jwtz imeshauri iwepo Mitaala ya Mafunzo ya amani na usalama

 Mkuu wa Kamandi ya Vikosi chini ya Makao Makuu Meja Jenerali Iddi Said Nkambi amevishauri Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Taasisi za Serikali na Kiraia zinazohusika na Ulinzi wa Amani chini ya Mwavuli wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika ( SADC) kuhakikisha zinandaa mitaala ya kuendeshea mafunzo ya Ulinzi wa Amani kwa kuzingatia matishio yanayozikabili nchi wanachama. Meja Jenerali Nkambi ameyasema hayo leo tarehe 18 Novemba 2024 wakati wa ufunguzi wa Semina fupi ya siku 5 inayohusu uwasilishaji wa mitaala mipya ya mafunzo itakayotumika kuandaa Majeshi ya SADC, semina inayofanyika katika Kituo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani (PTC) kilichopo Kunduchi Jijini Dar es salaam. Semina hiyo inayoendeshwa na Chuo cha Ulinzi wa Amani cha Kikanda chenye Makao Makuu yake nchini Zimbabwe inahudhuriwa na washiriki kutoka nchi wanachama wa SADC ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo katika kukabiliana na matishio pindi wanapokuwa katika majukumu ya Ulinzi wa Amani ndani ya ukanda wa S...

Jwtz imetaka Kuwepo kwa Mitaala ya Mafunzo ya amani na usalama

Mkuu wa Kamandi ya Vikosi chini ya Makao Makuu Meja Jenerali Iddi Said Nkambi amevitaka Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Taasisi za Serikali na Kiraia zinazohusika na Ulinzi wa Amani chini ya Mwavuli wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika ( SADC) kuhakikisha zinandaa mitaala ya kuendeshea mafunzo ya Ulinzi wa Amani kwa kuzingatia matishio yanayozikabili nchi wanachama. Meja Jenerali Nkambi ameyasema hayo leo tarehe 18 Novemba 2024 wakati wa ufunguzi wa Semina fupi ya siku 5 inayohusu  uwasilishaji wa mitaala mipya ya mafunzo itakayotumika kuandaa  Majeshi ya SADC, semina inayofanyika katika Kituo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani (PTC) kilichopo Kunduchi Jijini Dar es salaam. Semina hiyo inayoendeshwa na Chuo cha Ulinzi wa Amani cha Kikanda chenye Makao Makuu yake nchini Zimbabwe inahudhuriwa na washiriki kutoka nchi wanachama wa SADC ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo katika kukabiliana na matishio pindi wanapokuwa katika majukumu ya Ulinzi wa Amani ndani ya ukanda wa...

Waziri Mkuu aongoza Waombolezaji Kuaga Miili ya waliofariki Kariakoo

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiongoza waombolezaji kuaga miili ya watu waliofariki baada ya kudondokewa na jengo katika eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam. Tukio hilo limefanyika leo Novemba 18, 2024 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Wananchi wa Kijiji cha Nyasaungu Kuanza Kupata Huduma za afya Disemba 2024 Kwenye Zahanati yao

Na Shomari Binda-Musoma WANANCHI wa Kijiji cha Nyasaungu chenye vitongoji 5 kilichopo jimbo la Musoma vijijini wataanza kupata huduma za afya kwenye zahanati yao ifikapo mwezi disemba. Kijiji hiki ni moja ya vijiji vitatu vya Kata ya Ifulifu huku vijiji vingine ni Kabegi na Kiemba ambavyo kila kimoja kina zahanati yake. Ujenzi wa zahanati hiyo ulianza kwa kutumia michango ya fedha kutoka kwa wanakijiji na mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo.  Mbunge huyo aliendesha harambee mbili za kupata fedha za kuanza ujenzi wa zahanati hiyo ambazo zilikuwa na mafanikio makubwa. Licha ya harambe hizo za mbunge wanakijiji wanachangia nguvukazi kwenye ujenzi wa zahanati yao. Hadi sasa serikali kuu imeshatoa kiasi cha milioni 100 kwaajili ya kuendelea na ujenzi huo Jengo kuu la zahanati linakamilishwa,choo chenye matundu matatu kinajengwa huku Mkandarasi akipewa mkataba wa kukamilisha ujenzi wa zahanati hiyo upande jengo kuu na choo unaoishia tarehe 30 Novemba 2024. Kujitol...

Waziri Chana akutana na Balozi wa Italia Nchini

Na Happiness Shayo - Dar es Salaam  Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Italia nchini Tanzania, Mhe. Giuseppe Sean Coppola ambapo pamoja na mambo mengine wamekubaliana  kushirikiana kwenye nyanja mbalimbali za Sekta ya Maliasili na Utalii. Kikao hicho kimefanyika leo Novemba 18,2024 katika ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) jijini Dar es Salaam.  Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Chana amesema kuwa Tanzania na Italia zinaweza kuimarisha mashirikiano ili kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea nchini huku akisisitiza kuwa ukuaji wa Sekta ya Maliasili na Utalii nchini unatokana na jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kutangaza utalii hasa kupitia filamu za “Tanzania The Royal Tour” na “Amazing Tanzania”. "Tuimarishe ushirikiano katika Taasisi zetu za Sekta ya Maliasili na Utalii kati ya Tanzania na Italia katika utangazaji utalii , kufanya tafiti...