Skip to main content

Posts

Showing posts from November 10, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

HOMBOLO THEMATIC CITY KUCHOCHEA AJIRA NA UWEKEZAJI DODOMA

WANANCHI wa Kata ya Hombolo jijini Dodoma wameeleza matumaini makubwa kuhusu ujenzi wa Hombolo Thematic City, wakitarajia mradi huo kuwa chachu ya ukuaji wa uchumi, upatikanaji wa ajira, upanuzi wa biashara na uboreshaji wa huduma za kijamii. Wananchi hao wamesema ujio wa mji huo wa kisasa unafungua ukurasa mpya wa maendeleo kwa wakazi wa Hombolo, huku wakisisitiza umuhimu wa kushirikishwa ili wanufaike na fursa zitakazotokana na uwekezaji huo. Mmoja wa wananchi hao, Ndugu Magawa ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji Cha Mkoyo hombolo, amesema matarajio yao ni kuona vijana wakipata ajira na wafanyabiashara wadogo wakipanua shughuli zao, sambamba na kuimarika kwa uchumi wa eneo hilo. Matarajio hayo yanafuatia Halmashauri ya Jiji la Dodoma kusaini mkataba na kampuni ya kimataifa ya Heerim Architecture & Planning kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa Hombolo Thematic City. Akishuhudia utiaji saini wa mkataba huo Novemba 9, 2026, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyemu...

BARAKA LEONARD: BUNGE LA VIJANA NI JUKWAA LA KUANDAA VIONGOZI BORA

 KATIBU wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Baraka Leonard, amesema Bunge la Vijana ni jukwaa muhimu la kuwaandaa vijana kuwa viongozi bora wa sasa na baadaye kwa kuwajengea maarifa, uadilifu, uzalendo na uwezo wa kushiriki katika ujenzi wa jamii na taifa. Leonard ameyasema hayo wakati akifungua rasmi Bunge la Vijana kwa mwaka 2026, akieleza kuwa jukwaa hilo lina malengo mbalimbali ikiwemo kuwawezesha vijana kuelewa taratibu na kanuni za kuendesha Bunge pamoja na majukumu ya viongozi na wabunge katika kutekeleza shughuli za kibunge. Amesema lengo jingine ni kujenga utamaduni wa kujadiliana kwa hoja, kuvumiliana na kuheshimu mawazo tofauti, akisisitiza kuwa tofauti za kimawazo ni sehemu muhimu ya demokrasia na zinapaswa kupewa nafasi katika mijadala. Aidha, amesema Bunge hilo linalenga kuwawezesha vijana kujiamini, kujenga na kuwasilisha hoja zao kwa ufasaha kwa kuzingatia ushahidi, mantiki na maslahi mapana ya jamii, huku likiwapa elimu kuhusu masuala na changamoto mbalimb...

MIRADI YA BOOST YA SHILINGI BILIONI 4.2 YACHOCHEA UFAULU WA DARASA LA SABA SENGEREMA

*MWANZA:*  Uwekezaji wa Serikali kupitia programu ya BOOST wenye thamani ya shilingi bilioni 4.2 katika kuboresha miundombinu ya elimu umeanza kuonesha matokeo chanya, baada ya Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza kushika nafasi ya tatu kimkoa katika matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba mwaka 2026. Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI anayeshughulikia elimu, Dkt. Festo Ndugange, wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani humo, ambapo alikutana na walimu, wanafunzi, wazazi, viongozi na wananchi, baada ya kukagua ujenzi wa Shule mpya ya Awali na Msingi ya Isamilo. Mradi huo uliogharimu zaidi ya shilingi milioni 540.3 unahusisha ujenzi wa vyumba 14 vya madarasa, jengo moja la utawala, matundu ya vyoo pamoja na upatikanaji wa samani za shule. Akizungumza katika ziara hiyo, Dkt. Ndugange amesema Serikali imewekeza kwa kiasi kikubwa katika sekta ya elimu kuanzia mwaka 2021 hadi 2026, kwa kujenga miundombinu na kuwezesha upatikanaji wa vifaa vya kujifunzia ...

SEKTA YA MADINI KUENDELEA KUTOA AJIRA KWA VIJANA.

 Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga. SEKTA ya madini mkoani Tanga imeendelea kuimarisha mchango wake katika uchumi wa mkoa na taifa, huku uwekezaji mpya ukitarajiwa kuongeza mapato ya Serikali, ajira na fursa za biashara kwa wananchi. Afisa Madini wa Mkoa wa Tanga, Mhandisi Laurent Bujashi, amesema katika mwaka wa fedha uliopita mkoa ulikusanya Sh13.9 bilioni kupitia tozo na maduhuli yanayosimamiwa na mamlaka za madini, kiasi kilichovuka lengo la Sh11 bilioni kwa asilimia 27.4. Amesema makusanyo hayo yalifikia asilimia 127.4 ya lengo, bila kujumuisha kodi zilizokusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). “Ukiunganisha makusanyo haya na kodi zinazokusanywa na TRA, mchango wa sekta ya madini katika mapato ya Mkoa wa Tanga ni mkubwa,” amesema Bujashi  Ameeleza kuwa mchango huo unatarajiwa kuongezeka kadiri shughuli za uchimbaji zinavyopanuka na miradi mipya ya uwekezaji inavyoanza kufanya kazi. Sambamba na hayo pia amesema Mbali na mapato ya Serikali na ajira, kampuni za madini zinat...

SERIKALI YAIPONGEZA TIA KWA KONGAMANO LA BIASHARA

Na Mwandishi Wetu, Dodoma SERIKALI imewataka watafiti nchini wafanye tafiti zinazojibu maswali ya wananchi na zinazoonyesha namna ya kuongeza ajira, kuongeza uzalishaji, kupanua soko, na kuboresha maisha ya watu. Hayo yamesemwa leo mkoani Dodoma na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Dk Pius Chaya kwenye ufunguzi wa kongamano la tano la kimataifa la usimamizi wa biashara na maendeleo ya kiuchumi lililoandaliwa na Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA). Alisema ukuaji wa uchumi una maana tu pale unapogusa maisha ya Mtanzania wa kawaida kwa hiyo ni vyema mikakati ikajikita kujenga uchumi shindani na jumuishi na kuhakikisha kila Mtanzania anashiriki na kunufaika na ukuaji wa uchumi, kupitia ajira, biashara na uzalishaji. Alisema tafiti zinapaswa kujikita kuangalia namna ya kukuza viwanda na kilimo tija, kuongeza thamani ya mazao yetu hapa nchini, kuongeza ajira vijijini na mijini, na kupunguza utegemezi wa kuuza malighafi. Alisema kuna umuhimu mkubwa kuendeleza rasilimali w...

DC ITUNDA AMWAKILISHA RC SAGINI KWENYE MAHAFALI YA TIA MBEYA

📍Awahimiza wahitimu kuwa wabunifu na wazalendo Na Mwandishi Wetu, Mbeya MKUU wa Wilaya ya Mbeya, Mhe. Solomon Itunda, amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Jumanne Sagini, katika mahafali ya Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA), Kampasi ya Mbeya, ambapo amewapongeza wahitimu kwa kuhitimu mafanikio ya masomo yao na kuwataka kutumia elimu na ujuzi walioupata kuleta mabadiliko chanya katika jamii na taifa kwa ujumla. Akizungumza wakati wa mahafali hayo, Mhe. Itunda amewahimiza wahitimu hao kuwa wabunifu, wazalendo na wenye maadili mema katika utekelezaji wa majukumu yao, akisisitiza kuwa elimu waliyoipata inapaswa kuwa nyenzo thabiti ya kutatua changamoto za kijamii, kuongeza tija mahali pa kazi, na kutumia fursa zilizopo kujiajiri badala ya kusubiri ajira pekee. Aidha, aliwataka waendelee kuendana na kasi ya mabadiliko ya sayansi na teknolojia pamoja na mahitaji ya soko la ajira la sasa kwa kujifunza bila kuchoka, akibainisha kuwa mafanikio ya kijana mmoja mmoja na taifa kwa ujumla yanat...