Na Mashaka Mhando, MWANZA SERIKALI kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, imeahidi kumaliza changamoto ya ukosefu wa taa katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, ili kuwezesha uwanja huo mkongwe kutumika kwa mechi na matamasha nyakati za usiku. Ahadi hiyo nzito imetolewa leo, Agosti 8, 2026, na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Hamis Mwinjuma (maarufu Mwana FA), wakati alipofanya ziara maalum ya kukagua miundombinu ya uwanja huo, huku akisisitiza kushirikiana na wadau wa michezo kutatua kero hiyo. Mhe. Mwinjuma amebainisha kuwa dhamira kuu ya Serikali ni kuhakikisha miundombinu yote ya michezo nchini inaboreshwa na kufikia viwango vinavyokidhi mahitaji ya sasa. "Moja ya changamoto kubwa iliyopo hapa Kirumba ni ukosefu wa mfumo wa taa unaowezesha uwanja kutumika kwa ufanisi nyakati za usiku. Hali hii imekuwa ikipunguza fursa za kufanyika kwa baadhi ya shughuli za michezo, hususan mechi na matukio yanayohitaji matumizi ya uwanja wakati wa usiku, naahidi hili nita...
Marato tv - Sauti ya Jamii